Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kwa upande mmoja uvumbuzi wa umeme kwa kujaza namba-LUKU inaonekana ni ukombozi kwa shirika kama Tanesco ambalo kwa mfumo wa mita za kukopesha limeshaingia hasara ya mabilioni ya shilingi.Hata hivyo kwa kuangalia mambo yanavyokwenda hii huduma baadae itakuwa kero kwa wateja wa umeme.
Sijui kabla ya Tanzania ni nchi gani zilikwishatumia huduma hii,na pamoja nayo ni akina nani wanaotumia Luku.
Hii leo kwa mfano mitambo ya LUKU kama kwamba imezimwa kabisa.Watu wenye shida mbali mbali za umeme wamekuwa wakizunguka mijini na majijini kama vile watu wanavyosaka maji siku za ukame.Wamefadhaika wanapigiana simu kila mji kutaraji huko ndiko uliko,lakini wapi!..Wengine wanasema leo watakosa kuangalia fainali ya kombe la dunia,wengine wanasema samaki wao wa biashara wako hatarini kuoza na huku umeme ukiwaka nyumba za jirani na wao wenyewe fedha za kununulia wanazo mifukoni,hawana haja ya kuwakopa Tanesco.
Sasa jee LUKU ni ukombozi au imekuwa kero?.