LUKU inakula umeme sio poa

LUKU inakula umeme sio poa

Pole sana au friji limekuwa bovu.
Nipo kigamboni pia, Sizimi friji, Taa za nje 6 bado za ndani, pasi, tv, na tangu nimeweka unit 56 ni wiki imeisha sasa na hazijaisha
Hizo unit natumia miezi 4 na nina pata hizo kwa 9000 tu
 
Sasa wewe ndio unatumia umeme mwingi, mimi 4units x 30 = 120units kwa mwezi, sawa na 40k hadi 50k, usizime fridge hasa kama lina upya bado(coz ukizima na kuwasha ni kama unalipa kazi upya na litakula umeme zaidi)
Friji mpya,zile hisense zenye dispenser ya mchongo,naona inanizingua tu,maana kipindi iko nawasha 24 hrs unit ndio zilikua zinaenda balaa
 
Hili tatizo watu wengi wanalilalamikia.
Asubuhi nilikuwa nasikiliza Clouds watu wanalalamika hadi mtangazaji akahojiwa hadi meneja wa Tanesco.Alichosema huu mwezi watu matumizi yamekuwa mengi kwakuwa wengi wapo nyumbani na watoto wako likizo hivo matumizi yamekuwa mengi.
Hii nikutokana na malalamiko ya watu wengi kwa huu mwezi units kutumika nyingi kuliko miez mingine
Halafu mtu anasema et anafuta shule za bweni
 
Toka tarehe 22/12 umeme unaenda kwenye luku sio poa. Wastan wa units 28 Kwa siku Kwa nyumba ya kutumia balbu 5 na friji, TV
Ni kweli kabisa. Yaani hawa akina Makamba sijui waliacha nini TANESCO, yaani wizi mtupu. Hata mi juzi tu nimenunua luku kibao ila nimekuja kushangaa eti unit zimebaki kidogo. Wanasheria mtusaidie
 
Toka tarehe 22/12 umeme unaenda kwenye luku sio poa. Wastan wa units 28 Kwa siku Kwa nyumba ya kutumia balbu 5 na friji, TV
Kwanza kata bima ya nyumba haraka sana. Pili muite fundi akague wiring ya nyumba yote pamoja na vifaa vyote vinavyotumia umeme, inavyoonekana kuna shoti ya umeme kubwa sana inayosababisha umeme kupotea. Kumbuka bill ya umeme inatokana na jumla ya umeme unaotumia(active power) na umeme unaopotea(reactive power). Kama hakuna shida kwenye wiring ya nyumba au vifaa vinavyotumia umeme basi cheki na tanesco wakague mita yao. Hili tatizo ni kubwa sana chukua hatua mapema na usipuuzie la sivyo utaunguza nyumba yako.
 
Friji mpya,zile hisense zenye dispenser ya mchongo,naona inanizingua tu,maana kipindi iko nawasha 24 hrs unit ndio zilikua zinaenda balaa
Mara nyingi fridges ndio zinaumiza, unakuta fridge tu inakula 2-3units kwa siku,hapo bado TV, feni, pasi, majiko na vifaa vya jikoni, taa etc
 
Jaribu kukagua Earthroad, kile chuma kinachozamishwa chini kama kipo au kimeisha. Na Earthwire pia ni muhimu kukaguliwa.
 
31.12.2023 niliweka wa 20,000 (56 units) Jana tarehe 02.01 umeisha
Wee friji lako bovu ebooooh, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hata km matumizi, sio kwa style hiyo lol
 
Toka tarehe 22/12 umeme unaenda kwenye luku sio poa. Wastan wa units 28 Kwa siku Kwa nyumba ya kutumia balbu 5 na friji, TV
Nyumba yako ima miaka mingapi toka ijengwe? Tatizo limeanza lini?,
zungumza na watoto wako mara kwa mara juu ya matumizi sahihi ya umeme waambie ya kwamba,kila wanapomaliza wazime vifaa , kama pasi, jiko, nk.

Hakikisha kama unatumia jiko mwambie asiwashe jiko ikiwa hajandaa cha kupika

Amenunua nyama , anaikata kata anawasha jiko nyama inakuja wekwa jikoni dk 10 baadae muda huu wote jiko lilikuwa linawaka bila kitu , ndani hakuna mtu feni imewashwa,

Umemaliza kunyoosha nguo haujazima pasi hii ni changamoto kubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka tarehe 22/12 umeme unaenda kwenye luku sio poa. Wastan wa units 28 Kwa siku Kwa nyumba ya kutumia balbu 5 na friji, TV
Angalia meter yako ina balance ya unit ngapi za Luku, andika pembeni Kisha zima main switch na circuit breaker Kwa lisaa limoja halafu washa, then Angalia balance ya meter yako ya luku ukiona unit zimepunguwa basi hapo umeme una leakage sehemu, ita fundi akufanyie check up.

Panya ni tatizo kubwa Sana kwenye kukata waya Kwa waya ambazo hazijapita kwenye pipe, na earthrod huwa zinaoza, kwa kifupi zinahitaji kubadirishwa pia.
 
pole sana wasiliana na Tanesco... waje waangalie tatizo... kuna kipindi walikuwa wanafanya operation ya kubadilisha meter ulibadilishiwa...?​
 
Back
Top Bottom