Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Hili ni swali. Naungana na bwana Pascal Mayala kuwa swaki siyo statement.
Ukitaka kummaliza adui yako ni vizuri umpate kibaraka wa kupandikiza kwa adui yako.
Unasikia huko Ukraine, makamanda kadhaa wa kirusi wa ngazi za juu walivyouawa kwa makombora ya Ukraine. Hatujawahi kusikia makamanda wakubwa wa Ukraine wakitunguliwa kwa makombora. Swali la kujiuliza, hao wapigaji wa makombora wa Ukraine wanajuaje kwamba leo kuna kamanda mkubwa wa majeshi ya Ukraine anatembelea komandi fulani? Jibu ni rahisi. Ni lazima Ukraine imepenyeza watu wake ndani ya jeshi la Russia.
DP walipojua kuwa mkataba wao ja Tanzania ni mbaya, na hakuna mwenye akili anaweza kuukubali, ilitumia mbinu ya kuwapenyeza watu wake ndani ya vyombo vya maamuzi vya Tanzania na vyombo vya habari. Ndiyo maana watanzania wakilalamika dhidi ya maamuzi hayo ya hovyo, tayari kuna watu wa mwarabu waliopandikizwa kwenye jamii yetu, watapiga kelele kutetea na kutoa sifa juu ya DP, sifa ambazo hata DP wenyewe wanazisikia kwa mara ya kwanza.
Ni ukweli kuwa kelele za hao makywadi wa mwarabu hazijaweza kubadili msimamo wa watanzania wengi wenye akili, uelewa na mapenzi mema kwa nchi yao.
Huko nyuma, licha ya bwana Lukuvi kuhangaika sana akizunguka nchi nzima kutatua migogoro ya ardhi, kwa mshangao wa wengi, aliwekwa pembeni, na wananchi bila shaka waludanganywa kuwa eti amepewa nafasi maalum ya ushauri.
Hivi majuzi, katikati ya kashfa ya kuigawa bandari yetu kwa mwarabu, tunaambiwa kuwa eti Lukuvi ameteuliwa kuwa mshauri. Mara ya kwanza tuliambiwa ameondolewa kwenye uwaziri na kupewa nafasi ya ushauri. Kama alikwishapewa nafasi ya ushauri wakati anaondolewa kwenye uwaziri, imekuwaje tena na safari hii apewe nafasi ya kuwa mshauri wakati tayari alikwishakuwa mshauri? Au dhamira ni kumfanya kuwa mpini wa MTi kwenye shoka ili ukakate MITI?
Maswali ni mengi, muda ni kidogo.