Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Fakii Lulandala, Katibu Mkuu Uvccm amesema kuwa "CCM ni chama kikubwa chenye watu wengi wenye sifa na uwezo na karama za uongozi, hakina historia ya kuruhusu ung'ang'anizi kwenye nafasi za uongozi kama kule kwa kwa jirani ,nakishukuru sana Chama changu (CCM) kuona kwamba kwa muda huu ninafaa kukitumikia kwenye nafasi hii kwa muda ambao itakipendeza, baada ya kuteuliwa nimesoma mitandaoni kuna wengine wanasema mimi ni mzanzibari, hata ningekuwa mzanzibari nisingejisikia vibaya lakini mimi nimezaliwa Ilembula wilayani Wanging'ombe Mkoa wa Njombe ndio ninapotoka"