Lulu akubali kukaa jela, awaambia ndugu zake wasikate rufaa kilichotokea ni mipango ya Mungu

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Kwa ufupi

Asema atakuwa huru baada ya kutumikia adhabu hiyo kwa sababu ni mipango ya Mungu
By Kalunde Jamal, Mwananchi

Imeelezwa kuwa baada ya msanii Elizabeth Michael kusomewa hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela, aliwaambia ndugu zake wasikate rufaa kwa kuwa kilichotokea ni mipango ya Mungu na yupo tayari kukabiliana nayo.

Msanii , Muhsin Awadh maarufu Dk Cheni ambaye amekuwa karibu na mwigizaji huyo katika kipindi chote amesimulia hali ilivyokuwa muda mfupi baada ya jaji kutoa hukumu hiyo.

“Kusema ukweli Lulu alijua lolote linaweza kutokea ila la kufungwa ni kama hakulipa kipaumbele sana, jaji alipomaliza kusoma hukumu alishtuka kama sisi wengine wote lakini ajabu alikuwa wa kwanza kurudi katika hali ya kawaida na kutoa kauli za ujasiri,” anasimulia Dk Cheni

Lulu alisema: "Sipingani na maamuzi ya Mungu, haya ni maamuzi yake na nimekubaliana nayo. Ana makusudi yake kunipa hiki kilichotokea leo".

Anasema kingine alichowaambia ni kuachana na masuala ya kukata rufaa kwa sababu bado hatakuwa huru: "Acheni miaka miwili siyo mingi, sitaki kupingana na mahakama , naheshimu maamuzi ya mahakama, acheni nitumikie kifungo changu. "

Mapema wiki hii mwigizaji huyo alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake Steven Kanumba, Aprili 7,2012.

CHANZO: Mwananchi
 
Wewe ni msafi?
Kwahiyo yeye kwenda jera ni mapenzi ya shetani?
Ulitaka aseme nakubariana na mapenzi ya shetani?
Kuna kosa mtu kubadirika na kuanza kumtegemea Mungu?
 
sahihi mkuu... Wanaharibu kila kitu
 
Mwenyenzi Mungu Mkuu..ndie aliyemtuma akafanye ngono bado mdogo..aende Night club bado mdogo..mwambieni achaa upumbavu mkubwa wakumshirikisha Mwenyenzi Mungu na uchafu wake
 

This is nonsense, inaweza kuwa ni mpango wa Mungu yeye kufungwa ili amrudie Mungu!
 
Imeelezwa kuwa baada ya msanii Elizabeth Michael kusomewa hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela, aliwaambia ndugu zake wasikate rufaa kwa kuwa kilichotokea ni mipango ya Mungu na yupo tayari kukubaliana nayo.

Msanii Muhsin Awadh maarufu Dk Cheni ambaye amekuwa karibu na mwigizaji huyo katika kipindi chote amesimulia hali ilivyokuwa muda mfupi baada ya jaji kutoa hukumu hiyo.

"Kusema ukweli Lulu alijua lolote linaweza kutokea ila la kufungwa ni kama hakulipa kipaumbele sana, jaji alipomaliza kusoma hukumu alishtuka kama sisi wengine wote lakini ajabu alikuwa wa kwanza kurudi katika hali ya kawaida na kutoa kauli za ujasiri", alisimulia Dk. Cheni.

Lulu alisema: "Sipingani na maamuzi ya Mungu, haya ni maamuzi yake na nimekubaliana nayo. Ana makusudi yake kunipa hiki kilichotokea leo".

Amesema kingine alichowaambia ni kuachana na masuala ya kukata rufaa kwa sababu bado hatakuwa huru: "Acheni miaka miwili siyo mingi, sitaki kupingana na mahakama, ninaheshimu maamuzi ya mahakama, acheni nitumikie kifungo changu". alisema Lulu
 
Sisi wengine tumekaa jela miaka sita kwenye shule za boarding za serikali! Tukila ugali wa dona na maharge yasiyo na ushirikiano ila mwisho wa siku tulitoka. Tulifanya kazi ngumu ikiwa ni pamoja na kusoma vitabu vigumu vya mzungu kwa lugha isiyoeleweka eti wanaiita kiingereza. Hakuna marefu yasiyo na ncha. Cha muhimu awe strong, miaka miwili sio mingi kivilie!
 
Mkuu wewe hunaga dhambi
 

Mungu anaonewa sana asee, hata ktk mambo yakujisababishia wenyewe
 
Mungu pia huwa anashiriki kwenye mambo ya uzinzi namna hiyo? Au alikuwa anamaanisha miungu
 
Mungu pia huwa anashiriki kwenye mambo ya uzinzi namna hiyo? Au alikuwa anamaanisha miungu
Mipango ya Mungu kaamua kumwadhibu kwa aliyoyatenda kwa kumweka gerezani miaka miwili ili akitoka awe amebadirika.
Au umeelewaje wewe?
 

I love this little sister. she will be fine.
 
ndugu umefikiria sana aisee, yaani boarding za miaka hiyo daah, kazi ngumu, ukija kwenye kula harage lina funza na kama halina funza unakula harage kama unakula karanga, ukija dona limejaa funza na nyuzi nyuzi, aisee yale yalikuwa ni mateso kwa kweli, asubuhi kuamshana mchakamchaka, we acha tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…