Lulu avamiwa na majambazi

Lulu avamiwa na majambazi

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu' amekumbwa na masaibu mapya ya kuvamiwa na vibaka nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar na kumuibia simu zake mbili aina ya Iphone.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo wezi hao wanadaiwa kuruka ukuta na kufanikiwa kuvunja dirisha la chumba anacholala mrembo huyo na kumliza simu hizo huku yeye akiwa amelala fofofo.

Kwa mujibu wa chanzo makini, wezi hao walitumia mbinu za ‘kisayansi' kutekeleza zoezi lao kwani siku hiyo Lulu alirudi nyumbani mapema na akawa anachati kwa kutumia moja ya simu hizo, ghafla akapitiwa ambapo alikuja kushtuka na kukuta dirisha limevunjwa na simu zimetoweka.

"Nimemhurumia sana Lulu kwa kuwa siku ambayo ameibiwa, simu kesho yake tena akafiwa na bibi yake mzaa mama ambaye ndiye alikuwa kipenzi chake sana.

Hapo utagundua alipata majanga kiasi gani maana wakati alikuwa bado anafikiria ishu ya simu huku tena akakumbana na janga la kifo.

"Amelazimika kutafuta simu nyingine anayoitumia sasa tofauti na awali alikuwa nazo mbili," kilisema chanzo hicho.Paparazi wetu baada ya kupenyezewa ubuyu huo, alimtafuta Lulu ili aizungumzie ishu hiyo, ambapo alikiri kufikwa na masaibu hayo huku akishindwa kufafanua zaidi juu ya tukio hilo kwa kile alichodai alikuwa sehemu yenye kelele.

"Ni kweli nimepata matatizo sana mwezi huu ikiwa pamoja na hilo la kuibiwa simu, sema kwa hapa nilipo siwezi kuzungumzia lolote maana nipo katikati ya watu wengi na kuna makelele sana. Lakini itakuwa vyema nikikutafuta baadaye," alisema.

Licha ya Lulu kutotaja kiasi, simu hizo zinakadiriwa kufikia kiasi cha shilingi million tatu.
 

Attachments

  • 1439973541317.jpg
    1439973541317.jpg
    41.8 KB · Views: 2,744
Ila katoto kanazidi kuwa kama mcharo, sijui nani anazuia mzigo sasa hivi
 
Kalala mpaka wanavunja dirisha hajasikia,muda mwingine watazamia Ikulu.
 
Sidhan kama kuna ukwel hapo.Mbona Lulu hajanambia???
 
Wanajuana hao huenda hawajaiba wamechukua vyao,wewe mtu hadi dirisha linavunjwa hana habari,bora angesema wamekata wavu angeeleweka,
 
Yaaani walishindwa kuonja tunda ama waliogopa kurest in peace!
 
Nina namba yake mpya kanipa leo yani
 
Sasa hawa vibaka hawana adabu Lulu si ukawa mwenzao huyu mbona wanamfanyia hivi?
 
Hawa bongo mavi wasipoandikwa kwenye magazeti ya shigongo wanatengeneza tukio feki ili kupata media attention.
 
nimemnulia zingine tatu.milionn 4.5.kwanza zile tulikuwa na mpango wa kudispose.kama una shida nae ya kufanya show mtafute hapa.0653237866
 
Aaah siamini ile simu niliyo mnunulia chaina amepoteza walahi safari hii ni nokia tochi kwa kwenda mbele hawez nitia hasara kias ivi ntachindwa kujenda kwetu sasa
 
Back
Top Bottom