Lulu sasa abadilishiwa mashtaka

Lulu sasa abadilishiwa mashtaka

Mashitaka hayapelekwi mahakama tu bila kuwa na kosa linalolingana na kosa la kisheria. Kwa mfano huwezi kumshitaki mtu kwa kosa la wizi wa kutumia slaha wakati kweli aliiba lakini hakuna slaha iliyotumika. Huwezi kuthibitisha hilo. Makusudi ya kupeleka mashitaka mahakamani ni kushinda kulingana na kosa lililopo kwa mujibu wa vifungu vya sheria. Hii ndiyo kazi ya DPP kulinganisha kosa analotuhumiwa nalo mtuhumiwa na vifungu sahihi vya sheria. DPP hajakosea.
 
Hvi katika hali ya kawaida nani anafurahi hichi kitoto kukaaa gerezani? Wamdhamini tu aanza kuishi adhabu aliyonayo moyon mwake inamtosha sana. Wangekuwa walikuwa na uadui tungesema alifurahia kifo cha Kanumba lakini walikuwa wapenzi so kilichotokea ni mambo ya kawaida katika mapenzi hasa unapoongeza na ukweli kuwa walikuwa wamekunywa pombe tena pombe kali.

Chunga sana ndugu siku zote BUSARA haipindui SHERIA, hakuna kitu kinaitwa nia NJEMA ili kuvunja sheria, wacha haki ifuate mkondo wake kama ambavyo magerezani wamejaa ndugu na jamaa zetu wasiokuwa na majina ya kubadilishiwa mashtaka au kesi zao kupelekwa kwa speed ya Jet.Double standard ni msingi wa uvunjifu wa amani.
 
Hiyo ni issue ya kisheria jamani!!! kama uelewa wako ni mdogo kuhusu sheria c vema ukatoa maoni yako ambayo unaonekana kituko. HAKUNA SIASA HAPO.
 
Tulisema, si alikuwa anaongea na yule jamaa aliyetoa pole ya 10M, na mazishi akaudhuria lkn mazishi ya former IGP, na wakuu wengine akauchuna !!!
yametimia, muda c mrefu ataachiwa ,bongo bana naskia kuna mjombaa anamkata kulekule pa gereza
 
Nimependa mod alipoacha uzi huu kwenye jukwaa la siasa, kwa kujua wako watu wenye ufahamu wangeidadavua na at least kwa kidogo watu watapata ufafanuzi.Binafsi sioni kosa la DPP,kwa kuwa DPP ndio mtayarishaji wa kosa ambalo mshitakiwa anatakiwa kushitakiwa nalo kwa mujibu wa ushahidi uliokusanywa na kutafutwa na mashahidi wa tukio wa waliopatikana [evidence and the people who will provide the evidence in the court of law].

Kwa vigezo vya ushahidi alivyopitia DPP na kujilizisha yeye kama DPP [Ofisi ya DPP na watalamu wake wa sheria na mashitaka] wameridhika na kujirithisha kuwa kwa upande wa mauaji ambayo yametokea basi kama binti huyu atapandishwa kwenye kizimba basi apandishe kwa kosa la kuua bila kukusudia na si kosa la kuua au kosa la kusababisha kifo.

EBU VAA PICHA HII WEWE UWE KAMA DPP:[Hii ni uchambuzi binafsi ahusiani na DPP ila natengeneza picha /imagination]

Kuna file linafika mezani kwao likiwa na taarifa za kijana ambae alifariki katika mazingira ya kutatanisha akiwa na mpenzi wake chumbani.

Historia ya kiafya ya marehemu ni kama ifuatavyo kuwa, akiwa kijana anasoma shule,alipata kuanguka mara kadha,wa kadha na kuzirai katika mazingira ambayo hakukuwa na kitu chenye ishara ya kitendo kilicho ashilia kumdhuru mpaka kufikia hatua ya kuzirai,kama vile kupigwa na kitu kizito kwenye kichwa au popote pale ambako kungemletea maumivu ya kumpatia mshtuko wa kufikia kiwango cha kuzirai huku povu likimtoka.

Kinachoonekana kutokea katika tendo lake kuzirai ni bahada ya kukasirika sana na kupiga makelele kwa sauti kubwa na ghafla katika mtafaruku ule wa uliochanganyikana na hasira binafsi yeye kama yeye kijana huyu mara anadondoka ghafra na kupoteza fahamu.Tendo hili la kijana huyu kudondoka na kupoteza fahamu, limejitokeza kwa kijana huyu mara kadha katika nyakati tofautit likiwa na sura ile ile ya pale anapokuwa na hasira na kufuatana na kelele ambazo anazipiga binafsi na kwa tendo ilo upelekea tatizo la yeye kuanguka na kupoteza fahamu.Basi kwa tendo hilo sisi watu tusio wataalamu wa maswala ya magonjwa hatuna jibu ya linalomtokea kijana huyo bali madakatari kupitia vipimo vyao na utalamu wao wanacho cha kutwambia kuwa hicho nini kinachompata kijana huyo.

Chukulia tukio hilo hilo linampata kijana huyo akiwa na binti chumbani au wewe mwenyewe mleta thread na hauna historia ya tatizo la kiafya la mgonjwa huyo kijana,na ikizingatia wakati linatokea hilo ni kwa kuwa uenda wewe na kijana husika mmetofautina mazungumzo [obvious ni kitu cha kawaida katika maisha ya kila siku ya mwanadamu yeyote yuke duniani kutofautina mazungumzo vinginevyo tungefanana dunia ingekuwa mahari panapo boa kuishi wanadamu].

Na wakati linatokea hilo uenda pia mazingira mengi sana yanabidi kutazamwa vitu kama nyumba, wewe binafsi mshituko wako au binti muhusika mshituko wake kwa kuliona tukio, kijana husika mwenye tukio alikuwa amekula au kunywa nini kwa vigezo hivyo, vinavyothibitishwa na wataalamu husika vinatosha kumpa DPP uamuzi wa kumpa mashitaka ambayo anastahiki kwa mujibu wa ushahidi.

Tena sie wengine tunaona kama DPP, amemchelewesha kumuachia huru binti huyo LILY!!!Ila wengine tumepata kujifunza mengi pia kuwa ni kwa USALAMA wa binti kwa mujibu wa UMMA [Kwa sababu tatizo zima la marehemu liligeuka kuwa Public Interest kwa uzito wa jinsi marehemu alivyokuwa na umaalufu katika jamii yetu].Watanzania wengi tukiwa na mapungufu katika kuzielewa sheria na mambo mengi yahusuyo haki za makosa na mashitaka,tukio la ndugu yetu marehemu Kanumba [R.I.P] linageuka kuangaliwa katika mtizamo binafsi na sio mtizamo wa hali halisia.

Ndio maana hata ofisi ya DPP imechukua muda pia kulifanyia utafiti na kuwapa muda Watanzania kuondoa ule sintoamini kama ilivyo yako unaeamini kuwa LILY uenda anamkono wake katika kifo cha Kanumba.Lakini kabla ya wewe na Watanzania wengine kumtwisha kitanzi hicho binti huyo kwa kuwa tukio hilo lilitokea wakati LILY wakiwa naye chumbani basi ndie aliyetenda huku tukishindwa kufanya utafiti [Research] wa mambo mengine ambayo yanaweza kuwa ni sababu ya kifo chake.

Tufike sehemu pia hii tabia yetu ya vyombo vya sheria kuwa na vijimambo vya kusema ETI KITU KIKIWA MAHAKAMANI AKISTAHIKI KUONGELEWA HUU MSEMO HAKIKA BINASI NAUONA SI WA HAKI KABISA.Kwa kuwa kama waandishi wa habari wangepata nafasi na wao kujituma kufanya investigation journalism kwa swala la Msanii Kanumba Umma ungeelimishwa na hivyo kuisaidia Serikali kuwapa umma picha ya mwenendo wa tukio zima na kuondoa matatizo ambayo yamekuwa ni utamaduni wetu wa kugeuss kama vile eti ni kwa sababu mtoto yule ni chakula ya wakubwa.Hakika inakera sana na pia inachafua sifa za viongozi walioko madarakani na kuongeza wigo wa chuki isiyo ya lazima kwa kuwa viongozi nao wameshadadia tabia ya kutetea mambo yote yanayokuwa mahakamani yasizungumzwe na umma kwenye vyombo vya habari.

Lakini nani atawakataza umma kutokufikilia hivyo wanavyofikilia kuwa LILIY ataachiwa kwa kuwa ni chakula cha wakubwa [Anashiliki kimapenzi na watu wenye madaraka].Kwa kuwa Kupitia viongozi washadadiaji wa mfumo wa kuwa kitu kiko mahakamani eti kisizungumzwe kwenye vyombo vya habari, basi Serikali inawapa umma nafasi kutunga wao nani anastahiki haki ipi kwa mujibu wa yale wasiyo jua kwa kuwa anayejua amewafunga kujua ama kwa kujua au kwa kutokujua, hivyo kuwapa nafasi kutunga wale wanaona mioyo yao inatamani kuona hivyo, na sio ukweli [Reality].

Inabaki ni kwa wachache wenye ufahamu wa tukio kulipima na kwa kiwango fulani kujalibu kuweka rekodi sawa.Naaamini kwa asilimia kubwa kama ili jambo kusingekuwa na eti MIIKO YA KUTOKUZUNGUMZIA MAMBO YALIYO MAHAKAMANI KWENYE VYOMBO VYA HABARI,basi ufahamu ambao vyombo vya habari vingejituma kudadavua na kuchunguza nina hakika mamilioni ya watanzania wangenishikiza Serikali ya Tanzania kuharakisha kumuachia binti huyo huru,na pia kungekuwa na ufahamu mwingine kwa umma kujitambua na kujifunza, na si huu wa majibu ya mitaani kwa kuwa ana husiano na vigogo.

Naamini tukio la marehemu Kanumba [R.I.P] limeleta pia elimu pana kwa umma na pia kwa vyombo vya sheria kwenye misuguano kama mtuhumumiwa ashitakiwe kama mtu mzima au mtoto [Minor].Changa moto zote hizo zimeongeza ufahamu kwa watanzania.Hakika hata wewe mleta thread siku nyingine usije na lawama bali uje na thread zenye kuleta udadisi kuwa unataka kujifunza jambo ama kujua jambo.Ungekumbana na kesi ya OJ Simpson Trial hakika wewe ungelia na kugalagala ka mtoto mdogo anae lilia nyonyo.am joking by way!!!
 
Kulya, kwani umeambia DPP ametoa Nolle au amemshtaki kwa kosa dogo la bila kukusudia? Kuna maamuzi ya kesi nyingi ambayo yanasema kuwa iwapo kutatokea kifo baada ya ugomvi kosa ambalo mtuhumiwa anastahili kushtakiwa nalo ni la kuuwa bila kukusudia. Sijasoma jalada lakini kutokana na taarifa za magazeti zinaonyesha kuwa kukikuwa na ugomvi kati yao. Pia DPP asinge mshitaki Lulu kwa bila kukusudia kama ushahidi usingekamilika.
Nakiri kutofatilia shauri hili, ila nafikiri ni mapema sana DPP kufanya hivyo, japo kuwa sheria inamruhusu na kumpa mamlaka hayo, still iko kwenye committal proceedings... Anyways, labda ushahidi umekamilika na hautoshi kumtia hatiani...ila naona ni mapema sana!! Na kuna mashauri mengi tu ya vifo vya utata, ila hayatolewi nolle mapema hivi...
 
Ila majaji hawaku mfungulia lulu mashtaka + sio kazi yao ni kazi ya waendesha mashtaka


Kwani nini kazi ya majaji? Kama hakuna ushahidi tosha kesi si inafutwa? This is a public interest case na majaji wanajuwa hivyo, there's no point kumweka Lulu ndani wakati there's no apparent reason ya yeye kufungwa. Hii ni kazi ya majaji kusema kwamba there's no enough evidence huyu mtoto aachiliwe au la wampangie siku tu ya kurudi (akiwa nje tayari) baada ya kupata ushaidi tosha lakini si kumfunga na kumpangia kalenda zisizo na sababu wakati they know the truth.
 
Kulya, kwani umeambia DPP ametoa Nolle au amemshtaki kwa kosa dogo la bila kukusudia? Kuna maamuzi ya kesi nyingi ambayo yanasema kuwa iwapo kutatokea kifo baada ya ugomvi kosa ambalo mtuhumiwa anastahili kushtakiwa nalo ni la kuuwa bila kukusudia. Sijasoma jalada lakini kutokana na taarifa za magazeti zinaonyesha kuwa kukikuwa na ugomvi kati yao. Pia DPP asinge mshitaki Lulu kwa bila kukusudia kama ushahidi usingekamilika.
Ndio mkuu, its through entering a nolle prosequi, that discharges the accused from the respective charged offence... na hapo ndo wakaingiza charge mpya ya manslaughter....refer sect 91 CPA.

Mkuu, nilisema ni mapema kwani uchunguzi na upelelezi murder ni complex...mathalani, huenda ilikuwa ni trick tu...kwambakuwe na ugomvi, muwe mmelewa, halafu umsukume...kulikuwa na nini kwenye pombe?...anyways,kuna vingi vya kuchunguza na kupeleleza kwa makini, thats why nikasema ni mapema sana kwa DPP kuishia hapo.
 
Kwani nini kazi ya majaji? Kama hakuna ushahidi tosha kesi si inafutwa? This is a public interest case na majaji wanajuwa hivyo, there's no point kumweka Lulu ndani wakati there's no apparent reason ya yeye kufungwa. Hii ni kazi ya majaji kusema kwamba there's no enough evidence huyu mtoto aachiliwe au la wampangie siku tu ya kurudi (akiwa nje tayari) baada ya kupata ushaidi tosha lakini si kumfunga na kumpangia kalenda zisizo na sababu wakati they know the truth.

You said it all man!
 
Nadhani hujaelewa sheria zinasemaje. DPP anaweza kukushtaki kwa kuua makusudi au bila kukusudia kulingana na ushahidi anaokusanya. Ukweli ni kwamba kutokana na taarifa zilizotolewa baada ya tukio zilionyesha kuwa Lulu hakuua makusudi ila zile purukushani walizokuwa nazo ndizo zilisababisha kifo. Daktari wa marehemu alieleza vizuri sana. Mi naona DPP yuko sahihi. Kosa la Lulu kuwepo mahali ambapo hakutakiwa kuwepo. Ukilinganisha umri wake na mambo aliyokuwa anayafanya ndiyo yaliyomponza.
Vichwa vya magazeti habari kubwa ya leo ni kwa msanii wa filamu nchini Lulu kubadilishiwa mashtaka kutoka kuua kwa kukusudia hadi kuua bila kukusudia.

Wanajamii, DPP kwa kufanya hivo tayari ameishatoa hukumu kwa mtuhumiwa. Hili suala lipo beyond judicial descretion power. Mahakama ndiyo yenye power ya kutafiti km mtuhumiwa aliua kwa kukusudia ama la.

Tunavyopeleka mashtaka mahakamani ya mauaji huwa hakuna shitaka la kuua bila kukusudia "manslaughter". Je ikitokea ushahidi ukapatikana mahakamani kwamba Lulu aliua kwa kukusudia! Sina haja hapa ya kumkandamiza Lulu ila napinga ukiukaji wa sheria alioufanya DPP. Huu ni ukiukwaji wa utawala wa sheria.

Ni ukiukwaji pia pale watendaji wa serikali wanapoingilia mamlaka za mahakama.
 
Kulya waonekana kuwa ni mwanasheria. Hivi si lazima ijulikane motive ya muuaji? Binti kasababisha kifo cha mpenzi wake kutokea, haikuonekana motive ya muuaji.
Umeongelea kuwa ni mapema sana,je una wasiwasi kuwa kuna samples au vidhibiti vingi kwenye idara ya mkemia mkuu vinavyosubiri uchunguzi kama vina kitu cha kudhuru au namna gani?
Nisaidie majibu.
 
Last edited by a moderator:
Hujui kazi za mahakama wala waendesha mashitaka..
Kujaribu kukuelimisha,ni kujitafutia sononi na jioni mbaya ya leo..
lengo langu sio kufundishwa utendaji wa mahakama ila ni kuomba watu wapunguze ushabiki na kujifanya kujua wakati jambo lenyewe ni tata.jioni yangu haiwezi kuharibiwa na wewe.
 
Kulya waonekana kuwa ni mwanasheria. Hivi si lazima ijulikane motive ya muuaji? Binti kasababisha kifo cha mpenzi wake kutokea, haikuonekana motive ya muuaji.
Umeongelea kuwa ni mapema sana,je una wasiwasi kuwa kuna samples au vidhibiti vingi kwenye idara ya mkemia mkuu vinavyosubiri uchunguzi kama vina kitu cha kudhuru au namna gani?
Nisaidie majibu.
Ndio, lazima kuwe na ill-will (mens rea),kama haitathibitika ndio inarudi manslaughter... ila kwa kesi za mauaji ku-establish whether or not ill-will on the perpetrator existed ni complex...uki-be moved emotionally utapoteza haki...inaweza kuwa ni organized crime (inahusisha watu wengine wengi) hivyo upelelezi inabidi ufanyike kwa makini na inahitaji muda mrefu kujiridhisha, huennda hata muuaji mwenyewe alitumika bila hata kujijua....

Kuhusu samples, nikiri sijafatilia hili shauri...so sina info kama kuna samples bado ziko kwa mkemia...na of course lazima kuna samples zilipelekwa kwa mkemia, kama za ile pombe, na vitu vingine vilivyokutwa eneo la tukio ikiwa ni pamoja na corpus kufanyiwa postmortem... Hadi DPP anafuta charge ya murder basi ujue hizo sample zimeshaleta majibu na hazina la zaidi kuthibitisha kosa.
 
DPP Feleshi ni janga la taifa! Wala sio udini, yule jamaa hata cheo hicho alikipata kwa kubebwa na............... He is incompetent, ama kweli haya ni mojawapo ya maajabu mengi ya Tanzania, kwamba AKILI NDOGO KUONGOZA AKILI KUBWA!
 
"Honest is very expensive gift do not expect it from cheap people"
 
Nafikiri, narudia, nasema nafikiri sio busara wala hekima kupandikiza hisia za kidini kwenye masuala ya kisheria.

istoshe suala la imani ya dini ni suala mtambuka sana ambalo sio rahisi kulipima kama vile kupima furaha na raha
 
Mkono wa Riz 1 huo amemis uhondo wa ile mtoto.
 
hawa wote ni watuhumiwa lakini tayari mahakama ya ubongo wako imeshawabandika makosa kabla ya upelelezi haujakamilika na ushahidi kupatikana beyond reasonable doubt

ngumbaru bana
 
Back
Top Bottom