Nimependa mod alipoacha uzi huu kwenye jukwaa la siasa, kwa kujua wako watu wenye ufahamu wangeidadavua na at least kwa kidogo watu watapata ufafanuzi.Binafsi sioni kosa la DPP,kwa kuwa DPP ndio mtayarishaji wa kosa ambalo mshitakiwa anatakiwa kushitakiwa nalo kwa mujibu wa ushahidi uliokusanywa na kutafutwa na mashahidi wa tukio wa waliopatikana [evidence and the people who will provide the evidence in the court of law].
Kwa vigezo vya ushahidi alivyopitia DPP na kujilizisha yeye kama DPP [Ofisi ya DPP na watalamu wake wa sheria na mashitaka] wameridhika na kujirithisha kuwa kwa upande wa mauaji ambayo yametokea basi kama binti huyu atapandishwa kwenye kizimba basi apandishe kwa kosa la kuua bila kukusudia na si kosa la kuua au kosa la kusababisha kifo.
EBU VAA PICHA HII WEWE UWE KAMA DPP:[Hii ni uchambuzi binafsi ahusiani na DPP ila natengeneza picha /imagination]
Kuna file linafika mezani kwao likiwa na taarifa za kijana ambae alifariki katika mazingira ya kutatanisha akiwa na mpenzi wake chumbani.
Historia ya kiafya ya marehemu ni kama ifuatavyo kuwa, akiwa kijana anasoma shule,alipata kuanguka mara kadha,wa kadha na kuzirai katika mazingira ambayo hakukuwa na kitu chenye ishara ya kitendo kilicho ashilia kumdhuru mpaka kufikia hatua ya kuzirai,kama vile kupigwa na kitu kizito kwenye kichwa au popote pale ambako kungemletea maumivu ya kumpatia mshtuko wa kufikia kiwango cha kuzirai huku povu likimtoka.
Kinachoonekana kutokea katika tendo lake kuzirai ni bahada ya kukasirika sana na kupiga makelele kwa sauti kubwa na ghafla katika mtafaruku ule wa uliochanganyikana na hasira binafsi yeye kama yeye kijana huyu mara anadondoka ghafra na kupoteza fahamu.Tendo hili la kijana huyu kudondoka na kupoteza fahamu, limejitokeza kwa kijana huyu mara kadha katika nyakati tofautit likiwa na sura ile ile ya pale anapokuwa na hasira na kufuatana na kelele ambazo anazipiga binafsi na kwa tendo ilo upelekea tatizo la yeye kuanguka na kupoteza fahamu.Basi kwa tendo hilo sisi watu tusio wataalamu wa maswala ya magonjwa hatuna jibu ya linalomtokea kijana huyo bali madakatari kupitia vipimo vyao na utalamu wao wanacho cha kutwambia kuwa hicho nini kinachompata kijana huyo.
Chukulia tukio hilo hilo linampata kijana huyo akiwa na binti chumbani au wewe mwenyewe mleta thread na hauna historia ya tatizo la kiafya la mgonjwa huyo kijana,na ikizingatia wakati linatokea hilo ni kwa kuwa uenda wewe na kijana husika mmetofautina mazungumzo [obvious ni kitu cha kawaida katika maisha ya kila siku ya mwanadamu yeyote yuke duniani kutofautina mazungumzo vinginevyo tungefanana dunia ingekuwa mahari panapo boa kuishi wanadamu].
Na wakati linatokea hilo uenda pia mazingira mengi sana yanabidi kutazamwa vitu kama nyumba, wewe binafsi mshituko wako au binti muhusika mshituko wake kwa kuliona tukio, kijana husika mwenye tukio alikuwa amekula au kunywa nini kwa vigezo hivyo, vinavyothibitishwa na wataalamu husika vinatosha kumpa DPP uamuzi wa kumpa mashitaka ambayo anastahiki kwa mujibu wa ushahidi.
Tena sie wengine tunaona kama DPP, amemchelewesha kumuachia huru binti huyo LILY!!!Ila wengine tumepata kujifunza mengi pia kuwa ni kwa USALAMA wa binti kwa mujibu wa UMMA [Kwa sababu tatizo zima la marehemu liligeuka kuwa Public Interest kwa uzito wa jinsi marehemu alivyokuwa na umaalufu katika jamii yetu].Watanzania wengi tukiwa na mapungufu katika kuzielewa sheria na mambo mengi yahusuyo haki za makosa na mashitaka,tukio la ndugu yetu marehemu Kanumba [R.I.P] linageuka kuangaliwa katika mtizamo binafsi na sio mtizamo wa hali halisia.
Ndio maana hata ofisi ya DPP imechukua muda pia kulifanyia utafiti na kuwapa muda Watanzania kuondoa ule sintoamini kama ilivyo yako unaeamini kuwa LILY uenda anamkono wake katika kifo cha Kanumba.Lakini kabla ya wewe na Watanzania wengine kumtwisha kitanzi hicho binti huyo kwa kuwa tukio hilo lilitokea wakati LILY wakiwa naye chumbani basi ndie aliyetenda huku tukishindwa kufanya utafiti [Research] wa mambo mengine ambayo yanaweza kuwa ni sababu ya kifo chake.
Tufike sehemu pia hii tabia yetu ya vyombo vya sheria kuwa na vijimambo vya kusema ETI KITU KIKIWA MAHAKAMANI AKISTAHIKI KUONGELEWA HUU MSEMO HAKIKA BINASI NAUONA SI WA HAKI KABISA.Kwa kuwa kama waandishi wa habari wangepata nafasi na wao kujituma kufanya investigation journalism kwa swala la Msanii Kanumba Umma ungeelimishwa na hivyo kuisaidia Serikali kuwapa umma picha ya mwenendo wa tukio zima na kuondoa matatizo ambayo yamekuwa ni utamaduni wetu wa kugeuss kama vile eti ni kwa sababu mtoto yule ni chakula ya wakubwa.Hakika inakera sana na pia inachafua sifa za viongozi walioko madarakani na kuongeza wigo wa chuki isiyo ya lazima kwa kuwa viongozi nao wameshadadia tabia ya kutetea mambo yote yanayokuwa mahakamani yasizungumzwe na umma kwenye vyombo vya habari.
Lakini nani atawakataza umma kutokufikilia hivyo wanavyofikilia kuwa LILIY ataachiwa kwa kuwa ni chakula cha wakubwa [Anashiliki kimapenzi na watu wenye madaraka].Kwa kuwa Kupitia viongozi washadadiaji wa mfumo wa kuwa kitu kiko mahakamani eti kisizungumzwe kwenye vyombo vya habari, basi Serikali inawapa umma nafasi kutunga wao nani anastahiki haki ipi kwa mujibu wa yale wasiyo jua kwa kuwa anayejua amewafunga kujua ama kwa kujua au kwa kutokujua, hivyo kuwapa nafasi kutunga wale wanaona mioyo yao inatamani kuona hivyo, na sio ukweli [Reality].
Inabaki ni kwa wachache wenye ufahamu wa tukio kulipima na kwa kiwango fulani kujalibu kuweka rekodi sawa.Naaamini kwa asilimia kubwa kama ili jambo kusingekuwa na eti MIIKO YA KUTOKUZUNGUMZIA MAMBO YALIYO MAHAKAMANI KWENYE VYOMBO VYA HABARI,basi ufahamu ambao vyombo vya habari vingejituma kudadavua na kuchunguza nina hakika mamilioni ya watanzania wangenishikiza Serikali ya Tanzania kuharakisha kumuachia binti huyo huru,na pia kungekuwa na ufahamu mwingine kwa umma kujitambua na kujifunza, na si huu wa majibu ya mitaani kwa kuwa ana husiano na vigogo.
Naamini tukio la marehemu Kanumba [R.I.P] limeleta pia elimu pana kwa umma na pia kwa vyombo vya sheria kwenye misuguano kama mtuhumumiwa ashitakiwe kama mtu mzima au mtoto [Minor].Changa moto zote hizo zimeongeza ufahamu kwa watanzania.Hakika hata wewe mleta thread siku nyingine usije na lawama bali uje na thread zenye kuleta udadisi kuwa unataka kujifunza jambo ama kujua jambo.Ungekumbana na kesi ya OJ Simpson Trial hakika wewe ungelia na kugalagala ka mtoto mdogo anae lilia nyonyo.am joking by way!!!