mrdocumentor
Member
- Nov 27, 2021
- 45
- 56
Mikoa ya kusini imekuwa kwa kiasi kikubwa ikijishughulisha na kilimo. Lakini aina ya kilimo wanachofanya si aina ya kilimo ambacho kimekuwa kikiwanufaisha kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na jitihada wanazowekeza.
Mazao mengi ya chakula kama vile mahindi, mtama, na mengineyo yamekuwa yakizalishwa kusini mwa Tanzania hasa katika mkoa wa Ruvuma ambao nafaka nyingi zimekuwa zikizalishwa uko.
Ni Ipi Lulu ya kusini?
Lulu ya kusini inayozungumziwa hapa ni Zao la korosho.
Korosho limekuwa ni zao ambalo limekuwa kama lulu kwa wananchi wa mikoa ya kusini mwa Tanzania. Kwa sababu ndio zao pekee ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa na kuboresha maisha ya wananchi wa kusini na Taifa kwa ujumla ukilinganisha na mazao mengine ya biashara ambayo yamekuwa yakizalishwa uko kusini kama vile Ufuta.
Picha kutoka Mtandaoni
Kwanini ni Lulu?
Lulu ni kito chenye thamani sana ambacho hata upatikanaji wake unahitaji jitihada na umakini wa hali ya juu mno. Richa ya upatikanaji wake kuwa ni mgumu na kuwa na vikwazo vingi sana ikiwemo kuchimba mchanga uliopo ndani ya bahari . Lakini baada ya jitihada zote hizo ikiwa utafanikiwa kuipata basi matunda yake ni makubwa pia.
Korosho ina thamani sana na ina siri ya utajiri mkubwa ambao umejificha. Mfano kupitia korosho watu hupata tunda aina ya bibo ambalo huweza kutumika kama chakula lakini pia hutumika kutengeneza pombe aina ya Gongo ambayo pia hutumika kutengeneza “spirit”. Pia kwenye korosho kuna korosho yenyewe ambayo ni chakula na malighafi ambayo hutumika kutengeneza aina zingine za vyakula mbalimbali ikiwemo Biskuti. Lakini pia kwenye korosho kuna ganda la korosho ambalo hutumika kutengeneza Mafuta lakini pia hutumika kutengeneza urembo.
Kwanini imefunikwa na Mchanga?
Licha ya thamani ambayo korosho ipo nayo lakini serikali ya Tanzania bado imekuwa kipofu katika kuuona utajiri uliopo ndani ya korosho.
Takwimu zinasemaje?
Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo duniani (FAO) iliitaja Tanzania kama nchi ambayo imekuwa na wastani mzuri wa uzalishaji wa korosho hadi kufikia mwaka 2012. Hiyo ilikuwa kabla ya zao hilo nchini kukumbwa na changamoto mbalimbali za kiuzalishaji na usimamizi mbovu wa zao hilo.
Benki kuu ya Tanzania (BOT) mwaka 2017 ililitaja zao la korosho kuwa lilingiza pato la taifa Dola milioni 346.6 sawa na bilioni 773 za Kitanzania kwa wakati huo. Hayo yalikuwa maendeleo makubwa zaidi kwenye zao hilo ukilinganisha na mwaka 2016 ambapo zao hilo liliingiza dola milioni 184.9 sawa na bilioni 411 za kitanzania kwa mujibu wa viwango vya wakati huo.
Picha kutoka Bodi ya korosho 2022
Takwimu ndio msema kweli. Kwa mujibu wa takwimu hizo inaonesha wazi kuwa zao hili lina mchango mkubwa sana katika kuongeza pato la taifa na pesa za kigeni nchini, lakini pia zao hili linaweza kuboresha maisha ya mtanzania kwa kiasi kikubwa mno ikiwa litasimamiwa vyema na kuwekewa mikakati mizuri kwa manufaa ya nchi.
Ipo wazi kuwa serikali kwa kushirikiana na bodi ya korosho Tanzania imefanya kazi kubwa sana kuhakikisha zao hili linanufaisha taifa la Tanzania.
Richa ya Jitihada zote hizo ambazo serikali imefanya bado kuna maeneo muhimu na nyeti ambayo ndipo zilipo funguo za mafanikio ya zao hilo bado hayajakaa sawa kiufupi yanahitaji usimamizi mkubwa na wa hali ya juu Mno. Maeneo hayo ni kama yafuatayo:-
Pembejeo
Katika shughuli ya kilimo cha zao lolote lile kwa matokeo mazuri pembejeo ni kipaumbele. Katika zao la korosho hapa kipaumbele zaidi ni Viuatilifu. Kuhusiana na suala zima la pembejeo, Bodi ya korosho Tanzania (CBT) imekuwa ikitoa mwongozo kila msimu juu ya upatikanaji na usambazaji wa Pembejeo kama ni miongoni mwa majukumu yao kwa mujibu wa sheria. (Rejea sheria ya tasnia ya korosho Na.18 ya mwaka 2009 na kanuni zake za mwaka 2010).
Hapa tatizo halipo kwenye kutoa mwongozo. Tatizo ni Je, huo mwongozo unafuatwa?
Msimu wa korosho 2021-2022 kama kawaida ya bodi ya korosho ilitoa mwongozo wake wa upatikanaji na usambazaji wa pembejeo. Lakini zipo changamoto zilizojitokeza richa ya muongozo kueleza kila kitu kuhusu aina gani za Viuatilifu vitumike na namna ya upatikanaji wake. Mfano wa Changamoto hizo ni hii ifuatayo:-
Sakata la usambazaji wa Viuatilifu feki
Gazeti la jamhuri chapisho la Mei 10 2022 liliripoti uwepo na usambazwaji wa Viuatilifu feki na likiwashuku baadhi ya viongozi kuhusika katika usambazaji wa Viuatilifu hivo aina ya “MAKONDE” ambavyo inasemekana Mamlaka ya afya ya mimea na udhibiti wa Viuatilifu Tanzania (TPHPA) iliamuru Viuatilifu hivyo kutosambazwa kwa wakulima kwakuwa havikukidhi vigezo.
Lakini baadae mkurugenzi wa bodi alikanusha taarifa hiyo kabla ya mkuu wa mkoa kugundua kweli kuna hilo tatizo na wahusika kufikishwa mahakamani.
Picha Kutoka Mtandaoni
Kutokana na sakata hilo utaona kuwa kuna kufeli kwa usimamizi na kukosa ushirikiano baina ya taasisi zenye mlengwa mmoja jambo ambalo linaweza kuhatarisha uzalishaji wa korosho kwa sababu hadi Viuatilifu hivyo vinakamatwa tayari vilikuwa vimesambazwa maeneo ya Tandahimba na Newala.
Mfumo wa ulipaji wakulima
Kupitia sheria hiyo hiyo ya tasnia ya korosho Na.18 ya mwaka 2009 na kanuni zake 2010. Bodi ya korosho ina jukumu la kutoa mwongozo wa masoko. Kwa kiasi kikubwa pia wamejitahidi kusimamia hili. Lakini yapo yapo madhaifu machache yanayohitaji kufanyiwa kazi, Nayo ni kama yafuatayo:-
•Wakulima kucheleweshewa malipo yao au kukosa kabisa.
Kumekuwa na kawaida ya wakulima wa korosho kucheleweshewa malipo yao hali inayowafanya wakulima hao kushindwa kuiona thamani ya zao hili ukilinganisha na jitihada wanazofanya katika uzalishaji wa zao hili. Lakini pia baadhi ya wakulima wakati mwingine hukosa kabisa malipo yao na kushindwa waanzie wapi kufuatilia. Mfano baada ya soko la dunia la korosho kuyumba mwaka 2018 serikali ilichukua jukumu la kununua korosho za wakulima katika msimu huo wakulima wengi hawakulipwa na wengine korosho zao zilirudishwa majumbani kwa madai kuwa hazikukidhi vigezo.
•Wakulima kushirikiana akaunti za benki.
Serikali na wadau wa fedha wamefanya jitihada kubwa sana kuwaelimisha wakulima kuhusiana na umuhimu wa kuwa na akaunti za benki kila mmoja. Lakini hili suala bado linaonekana kuwa ni changamoto kwa baadhi ya maeneo hasa yale maeneo ya vijijini sana. Bado wapo wakulima ambao wanatumia akaunti ya mtu mmoja ili malipo yao yakiwa tayari wayapate kutoka kwa huyo mwakilishi wao. Jambo hili linaweza kupelekea migongano na utata mkubwa katika jamii ikiwa mambo yataenda tofauti.
Kutokuwa na Masoko ya uhakika
Zao la korosho limekosa soko la uhakika hivyo kupelekea zao hili kutokuwa na muendelezo mzuri.
Mfano Msimu wa mwaka 2017 bei ya korosho ilipanda hadi mkulima aliuza kilo 1 kwa sh.3000 na zaidi lakini mwaka 2018 bei ya korosho ilishuka hivyo kupelekea wafanyabishara kuhitaji korosho inunuliwe kwa kilo 1 bei ya Sh. 1900- 2700 jambo ambalo lilipelekea wakulima kugoma kuuza mazao yao kwa bei hiyo. Hivyo serikali iliamua kununua zao hilo. Uamuzi ambao wengi waliathirika kutokana na kukosa malipo yao na wengine korosho zao kukataliwa.
Nini Kifanyike?
•Serikali iwekeze Zaidi kwenye viwanda vya ndani.
Ili kuondoa manyanyaso yote wanayopitia wakulima wa korosho ni lazima serikali iwekeze zaidi kwenye viwanda. Mfano mwaka 2019 serikali iliingia mkataba na viwanda vinne vya kubangua korosho ambavyo kwa ujumla vilikuwa na uwezo wa kubangua zaidi ya Tani 7500 kwa msimu ule. Ikiwa kama mwanzo tu wa hivyo viwanda vilikuwa na uwezo wa kubangua tani zote hizo vipi kwa misimu iliyofuata? Vipi kama Vingekuwa vingi?.
picha kutoka Mtandaoni
Majibu ni kwamba matunda ya uwekezaji huo yangekuwa makubwa zaidi na thamani ya korosho ya Tanzania ingependa na vijana wengi wangeajiriwa kwenye viwanda hivyo. Kwahiyo serikali inatakiwa kuchukua hii kama changamoto kwa kujenga viwanda vingi zaidi na kukaribisha wawekezaji wengi zaidi.
•Bodi ya korosho isiishie kutoa mwongozo wa usambazaji wa pembejeo na upatikanaji wa masoko tu.
Kutoa mwongozo tu sio tija; ikiwa muongozo huo hautasimamiwa hauwezi kufanya kazi ambayo italeta matokeo chanya. Ni lazima kama bodi ambayo imepewa mamlaka ya kusimamia korosho nchi nzima ihakikishe muongozo ambao umetolewa unafuatwa kama ambavyo wao kama bodi wanahitaji.
Mfano kwenye suala la pembejeo wahakikishe hatua kwa hatua hadi zinafika kwa mkulima vivyo hivyo kwenye utaratibu wa masoko na ulipaji.
Sehemu inayohitaji elimu ni lazima washirikiane na wadau wafanye hiyo kazi kwa ufanisi mkubwa. Kwa kufanya hivyo kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa na kukusudiwa kwenye muongozo.
Lakini bila kufanya hivyo muongozo utatolewa kila msimu na bado utabaki kama kumbukumbu tu kwenye makaratasi huwenda hata kusomwa usisomwe.
Hitimisho
Wito wangu kwa mamlaka zinazohusika kwa upekee wake Bodi ya korosho Tanzania (CBT) kuhakikisha wanatekeleza kwa ufanisi mipango mizuri wanayoipanga kuhusiana na zao hili kwa kushirikiana na wizara ya kilimo ili kuhakikisha zao hili linaleta manufaa na tija kwa wananchi wa kusini lakini pia linanufaisha Taifa zima la Tanzania kwa kuongeza pato la taifa. Hayo yote yatapatikana ikiwa Lulu hii itatazamwa kwa jicho la pili lenye umakini.
Ahsanteni.

Upvote
17