Hakika hili shindano limejifia.
Huwezi kumchukua sauda mwilima na yule msoma magazeti wakae pale red carpet kuhoji watu,ilifikia kipindi kuna mdadabalikuja pale ikaonekana kama yeye ndio ana host pale maana walimshindwa akawa kama yeye ndio anawafanyia interview.
Hili shindano pia ni kweli lilikosa promotion,mimi mwenyewe nili libahatisha tuu.
Poor perfomance kutoka kwa jyde ever,hakuna alicho kifanya pale zaidi watu waliimba yahya sababu ni popular song,but nothing new done. Jyde anatakiwa abadilike hile perfomance si ya kiwango chake,kifupi alikula pesa ya bure na hakuna alichofanya zaidi ya watu kusikiliza play back. Pia michael ross alijitahidi kucheza lakini alishindwa kuimba vizuri hata ule wimbo wake unao julikana.
Pia waache kutumia cd wawe wana kodi band ili watu wapate live music na si wizi ulio fanyika majuzi hili lina wahusu waandaaji.
Pia walikosa mc mzuri na wakuchangamsha shindano ni vigumu mtu kukumbuka kama kulikuwa na mc au mshereheshaji.
Hizi ni dalili kuwa hili shindano lina kwenda kufa lakini wanayo nafasi ya kujirekebisha.