Lundenga, miss Tanga wazichapa

Lundenga, miss Tanga wazichapa

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
KW/RB /8441 /2014 imemshikilia Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania , Hashimu Lundenga kwa madai ya kuzichapa na Miss Tanga 1997 , Mona Faraja ambaye pia ni mke wake na kumsababishia majeraha, Risasi Jumamosi lina ‘ full’ stori.

Miss Tanga 1997, Mona Faraja anayedaiwa kujeruhiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania , Hashimu Lundenga . Ishu hiyo iliyonyakwa laivu na majirani ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar , nyumbani kwa Lundenga wakati wawili hao walipokuwa wamepumzika baada ya mihangaiko ya mchana kutwa. Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, wakiwa wanabadilishana mawazo , mara simu ya Lundenga iliita na ndiyo chanzo cha mtafaruku , upi huo ?

TUJINGE NA CHANZO

Mtoa habari wetu alisema kuwa , tatizo lilikolea mara baada ya simu hiyo kuita mfululizo kwa namba ngeni iliyodaiwa kuwa ni ya ‘ kichenchede ’ cha pembeni huku bosi huyo akiwa hana mpango wa kuipokea . Hashimu Lundenga akiwa katika kituo cha poisi cha Kawe .

“Mke wa Lundenga alikuwa na shauku ya kujua nani anayepiga simu ya mumewe muda huo na kwa nini mumewe haipokei lakini wakati akiendelea kujiuliza ndipo ikaingia meseji ambapo inadaiwa Lundenga alikwenda ‘ fasta ’ kwenye inbox na kuifutilia kwa mbali .

“Kitendo cha kufuta SMS hiyo nacho kilitibua kabisa hali ya hewa , Mona akataka kujua kwa nini mumewe alikuwa hataki kupokea simu na SMS iliyoingia ilitoka wapi ? “Mona akawa mkali baada ya kuona haridhishwi na majibu ya mumewe ndipo alipoanza kutoa maneno yenye shutuma kwa mzee mzima ambapo naye uvumilivu ulimshinda kama binadamu wengine , wakaanza kutwangana ,” kilisema chanzo hicho.

MKE AWAHI POLISI

Chanzo hakikuwa tayari kuweka ‘ fullstop ’ , kiliendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi kuwa , baada ya mke kuona anazidiwa kwa kushushiwa makonde mazito yaliyomvimbisha uso, usiku huohuo alikimbilia Kituo cha Polisi Kawe, Dar kumripoti mumewe. Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania , Hashimu Lundenga .

POLISI WAMKAMATA LUNDENGA
Mara baada ya mke kumaliza malalamiko yake kituoni hapo , saa chache baadaye polisi walifika nyumbani wakiwa na difenda ambapo walimchukua mlalamikiwa huyo hadi kituoni kujibu madai hayo. “Polisi hawakuwa na maneno mengi, walipofika nyumbani walimkamata Lundenga na kwenda kumlaza kituoni kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria , ” kilisema chanzo.

MAJIRANI WANENA
Baadhi ya majirani waliolitambua sakata hilo walionesha kushangazwa huku wakimhurumia Mona ambaye alikuwa ameumia usoni, hususan mzunguko wote wa jicho la kushoto .

MKE AINGIWA NA HURUMA
Wakati gazeti hili likiwa katika hatua za mwisho kuelekea mitamboni , Mona alidaiwa kuingiwa na huruma kwa kitendo cha kumlaza mumewe kituoni hivyo alikwenda kwa lengo la kumfutia mashitaka . “Mke alimuonea huruma mumewe licha ya kupewa kipondo maana wamedumu kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10 sasa , si mchezo . Alikwenda Kawe kufuta kesi lakini polisi wakamkomalia kwamba ishu lazima ifike mahakamani, ” kilisema chanzo.

Mwandishi wetu alifika kituoni hapo na kukuta polisi na Mona wakiendelea na mazungumzo lakini hadi tunakwenda mitamboni , Lundenga alikuwa bado
anashikiliwa kituoni hapo.

Chanzo:GPL
 
Lundenga katika hili amejishushia heshima kabisa!
 
Ivi kama alimtongoza yeye enzi zile akiwa miss tanga anashindwaje ss kwa mamiss wengine???mzee inaonekana hajiwezi kwa mamiss.....
 
Ivi kama alimtongoza yeye enzi zile akiwa miss tanga anashindwaje ss kwa mamiss wengine???mzee inaonekana hajiwezi kwa mamiss.....

Ndo apo sasa hili zee ovyo kabisa, lazima mamiss wote kashawatafuna, sasa linaaibika
 
Ndo apo sasa hili zee ovyo kabisa, lazima mamiss wote kashawatafuna, sasa linaaibika

Nasikia hadi ndege john wema alishampitia ndio maana alimpa umiss ambao jokate ndo alistahili au lisa
 
UDAKU na UKUDA una wenyewe! Sasa hapo kampiga mkewe au kampiga miss TANGA?
 
Hivi samahani wakuu hivi hiko Cheo cha huyo mzee Lundenga hakuna kustaafu au kuwapisha wengine naona kama udikteta flani hivi maana toka niko mdogo namsikia yeye tuu anavyo wafaidi nataka kama kuna uchaguzi na sisi tutangaze nia ili tujilie mema ya nchi hii kama huyu Mze kumbe hadi kaoa uko uko. OMBI LANGU NA SISI VIJANA TUPEWE NAFASI TUTUMIE FURSA HII KWANI SUALA LA AJIRA NI TATIZO KUBWA. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Warumi hv ww ni shoga au..mwanaume gani mbea km nn kutwa kufatilia ya watu
 
huyu mzee ana laana ya mke wake wa ndoa aliyemtelekeza huko kimara ,yeye ana hangaika na watoto wadogo ona sasa anaaibika
 
Back
Top Bottom