Lundenga: Sina mahusiano na Sitti Mtemvu

Lundenga: Sina mahusiano na Sitti Mtemvu

ruanganyi

Senior Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
115
Reaction score
34
Ludenga%20.jpg

Mkurugenzi wa Lino Agency akichat Live na mashabiki wa EATV kupitia ukurasa wa facebook wa EATV

Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na aliyekuwa mshindi wa kwanza wa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu. Lundenga amefunguka hayo leo alipokuwa akichata Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita mchana mpka saa nane mchana.

Mbali na mahusiano Watu wengi walitaka kujua ni sifa zipi zilizompelekea mrembo Sitti Mtevu kutwaa taji hilo kama si upendeleo kutoka katika kamati na crew inayohusika kuandaa mashindano hayo kwani watu wengi wamekuwa wakisema kuwa mrembo huyo alikuwa hastahili kushinda taji hilo ukilinganisha na warembo wengine ambao walikuwa wakichuana nae, kufuatia hali hiyo Ludenga ikabidi aweke wazi sifa tano ambazo zinamfanya mtu kushinda taji la Miss Tanzania kuwa ni lazima awe na sura nzuri, umbo zuri, mvuto, haiba, ufahamu wa kutosha wa mambo mbali mbali.

SITI HANA SIFA YA KUWA MISS TEMEKE:
Kutokana na maamuzi ambayo Sitti Mtevu aliamua kujivua taji la Miss Tanzania 2014 hivyo mrembo huyo amejifutia sifa zake zote alizopata katika kusaka taji la Miss Tanzania hivyo si Miss Chang'ombe wala si Miss Temeke tena.


Hashim Lundenga amesema kuwa kitendo cha Sitti kujivua taji hivyo automaticaly amevua mataji yake yote aliyopata katika ngazi ya wilaya mkoa na hata Taifa kama ambavyo ilivyotangazwa.

"Hashim Lundenga: Automatimacally anakuwa amejivua na mataji mengine pia...."

Kufuatia sakata la Mrembo Sitti Mtevu kudanganya UMMA juu ya umri wake na kumgharimu kulivua taji hilo la Miss Tanzania 2014. Ludenga amesema kuwa hali ya udanganyifu wa umri wa warembo hao huwa ni suala la kawaida na lipo kila mwaka ila kwa kuwa huwa wako makini ndiyo maana wanagundua hivyo haoni sababu ya yeye na kampuni yake kuwajibika kisa Sitti Mtevu alidanganya umri.

"Hashim Lundenga: sio sahihi, tupo makini na ndio maana tumegundua, fahamu ya kwamba kila mwaka washiriki wengi tu hutudanganya kuhusu umri wao na ndio maana tupo makini.. tuwajibike kwa kosa gani?"

NIPO TAYARI KUKABIDHI KIJITI KWA MWINGINE:
Kufuatia kuzuka kwa kashfa mbalimbali zinazohushisha mashindano ya Miss Tanzania na waandaaji wake mashabiki wa Eatv walitaka kujua kama Mkurugenzi huyo wa Lino Agency Hashim Lundenga yupo tayari kuachia nafasi hiyo ili watu wengine waweze kuendeleza pale wao walipoishia lakini Lundenga aliweka wazi kuwa yeye kama Mkurugenzi yupo tayari kuchagua mtu mwingine ili asimamie nafasi yake lakini si kuwaachia watu wengine kuendesha shindano hilo.


"Hashim Lundenga : Lino International Agency ni Kampuni ya mtu binafsi na inayo Directors wake, hivyo tunaweza kuteua Mkurugenzi mwingine wa kufanya kazi hiyo.."

MISS TANZANIA HAIWEZI KUFUTWA:
Kutokana na baadhi ya watu kutooana umuhimu wa uwepo wa mashindano ya Miss Tanzania na kuyahusisha na kumomonyoka kwa maadili hususani kwa warembo wa Tanzania watu wamependekeza mashindano hayo yafutwe kwani yamekuwa hayana tija na hayana haki kwani kumekuwa na upendeleo na udanganyifu na vitendo vya rushwa ambavyo hupelekea wasichana wengi kuvunja utu wao kwa sababu ya kutaka kushinda au kufikia hatua fulani katika mashindano hayo.


"Hashim Lundenga: Sitty bado ni msichana mrembo na ataendelea kuwa mrembo....haya mashindano hayawezi kufutwa kwa sababu wananchi wanaelewa faida zake, wewe usiyejua faida zake, baki hivyo hivyo..."

MISS TANZANIA HAKUNA FAIDA YOYOTE:
Hashim Lundenga ameweka wazi kuwa katika mashindano hayo hakuna faida yoyote anayopata zaidi ya yeye mwenyewe kufahamika na kutembea nchi nyingi duniani, watu walitaka kujua kwanini miaka yoye amekuwa aking'ang'ana yeye tu katika kuandaa na kusimamia mashindano hayo na je anafanya kwa masilahi ya nani na hayo ndiyo yalikuwa majibu ya
Lundenga
:

Hashim Lundenga: hakuna faida yeyote, zaidi ya kufahamika, kutembea nchi nyingi duniani, n.k."

KASHFA YA NGONO KWANGU FITINA TU:
Hashim Lundenga amekana leo wakati akichat Live na mashabiki wa ukurasa wa wa EATV kuwa hana kashfa ya kuomba ngono au kuwalazimisha warembo hao kutoka na yeye kingono ili waweze kushinda au kushiriki mashindano hayo, Lundenga anasema hizo ni fitina tu za watu fulani wenye lengo la kumchafua na kuchafua mashindano hayo.


Hashim Lundenga: Hakuna kashfa kama hiyo..........hiyo ni fitna.............."

Lakini pia Lundenga aliwaambia Watanzania kuwa kutokana na Sitti kujivua taji na kumpa nafasi mshindi wa pili kuchukua taji hilo hivyo wasitegemee tena sherehe za kumkabidhi taji hilo Miss Tanzania namba mbili kwani shehere watafanya wazazi wake pamoja na wakala wake wa mkoa alipotokea.

Hashim Lundenga: akuna sherehe yeyote, sherehe huandaliwa na wazazi wake na wakala wake wa mkoa alipotokea"

Hashim Lundenga alimaliza kwa kusema kuwa tunaoomba radhi sana kwa wale wote ambao hatukuweza kujibu maswali yenu yote kutokana na ufinyu wa muda.

Chanzo:
EATV

 
Haya mambo ya sura na bodi na mapaja ni kichefu chefu na kinyaa tuu labda yana masilai ya wafadhili kwa kutoa mapesa ya maana maana hata kile kingelio chake huwa kikubwa sana na wala la maana hakuna
 
Sidhani kama ni busara kuanza kumtukana lundenga tujenge hoja zetu, mimi naamini mtu ukianza kutukana maana yake umeishiwa hoja
 
Hivi kwanini wasiwaachie vijana kufanya hili shindano maana mie naona kamati ya miss tz wote wazee
 
Huyu mzee huyu amekula ujana bado anakula na uzee....!!!!
 
Dawa ya giza ni nuru,ulimtetea "siti" kwa giza (sifa azizostahili) ila nuru (ukweli) ukamuumbua.
 
HASHIM lUNDENGA: "sio sahihi, tupo makini na ndio maana tumegundua, fahamu ya kwamba kila mwaka washiriki wengi tu hutudanganya kuhusu umri wao na ndio maana tupo makini.. tuwajibike kwa kosa gani?"
Samahani kidogo Wenye fani ya uhandishi wa habari, hivi huyo mtu aliwezaje kusema yupo makini ndio maana tumegundua alafu mkamuacha hivi hivi ilihali Outsiders ndio waliopiga kelele juu ya hili? Wakati Sitti anaenda kutetea kuwa ana umri sawa Lundega alikuwa pembemi akisaidia kueleza kuwa ana umri sawa kulingana na cheti. Pili hiyo taasisi yao inaonesha wazi haifanyi kazi sawa sawa juu ya sifa za kuwa miss, hawachukui muda kujiridhisha vigezo vyote vinavyohitajika kuwa Miss na ndio maana watu wanakuja na kuongopa kisha wao kuwaruhusu (May be kuna ka rushwa wanapewa)
Mwisho muundo mzima wa kuwa Miss Tanzania uratibiwe upya. Haiwezekani mtu aongope kitongojini, wilayani hadi taifa alafu wahusika wa kitaifa waone hakuna mapungufu hasa yanayowahusu wao. Hivi, hili taifa ni lenu au ni letu? To me muundo ufumuliwe na uangaliwe upya na taasisi za juu zinazohusika na masuala haya.
 
Back
Top Bottom