Lunyungu apata ajali

Lunyungu apata ajali

Nimeongea naye anasema hakuumia sana. Alikuwa anarudi DSM kutoka Arusha bonnet la gari likafunguka na akagonga mti na gari kupinduka. Nimemshauri akaangaliwe na madaktari kwa sababu hata kama hana majeraha ya mwili anaweza kuwa na internal bleeding.
 
Pole sana Mkuu Lunyungu........ushauri wa Jasusi ni muhimu
 
Pole sana mpiganaji mwenzetu. Mungu atakujalia upone haraka.
 
pole sana Kaka, ugua haraka upone (Bado tunakuhitaji)
 
Muda si mrefu nimeongea na mdau wa JF Lunyungu akaniarifu kuwa kapata ajali mbaya maeneo ya Bagamoyo baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka vibaya.

Kwa wale wenye kuhitaji kuongea naye naweza kuwapa namba yake katika PM.

Pole sana Lunyungu kwa majeraha yoyote uliyoyapata kutokana na ajali hiyo mbaya. Tunamuomba Mungu akupe ahueni ya haraka ili urudi katika shughuli zako za kila siku haraka iwezekenavyo.
 
I'm so sorry Lunyungu. So let's see you back , well and fit.
 
Pole sana Kamanda.
Wajua ajali watu watatafsiri mambo mengi ok wewe usijali zaidi ya watu kukupa support pole sana na uendelee na libeneke letu.
ajali ni ajali lakini Yesu yupo nawe atakulinda na damu yake utapona
 
Ninakupa pole sana kwa ajali iliyokupata, tunamshukuru Mungu kuwa umesalimika.
 
Pole sana Mkuu....Tunakuombea upone haraka urejee kwenye kusongesha gurudumu.........
 
Pole sana Mkuu Lunyungu. Naamini kuwa utapona haraka na kurejea kwenye shughuli kama kawaida
 
Pole Sana Mkuu Lunyungu;

Hii pia inatukumbusha kuwa kwa binadamu anything can happen any time. Kwa wale wenye imani ni vizuri kila siku kujikabithi mikononi mwa Muumba na zaidi ya hayo tuendelee kujitahidi kuwa waangalifu tunapotumia vyomba vya usafiri.

Get Well Soon Mpiganaji!
 
- Kamanda pona haraka urudi kwenye mapambano, maana ndio kwanza yameanza, Mungu sio fisadi kama tulivyoongea juzi ukiwa Biharamulo kwamba huu ni mwanzo tu wa vita vya kweli vya kuleta mabadiliko kwa taifa letu.

- Nitakutwangia baadaye.

Respect.

Kamanda Field Marshall Es.
 
Lunyungu Pole sana. Ninakuombea upone haraka ndugu.

SteveD.
 
Back
Top Bottom