Panda gari ya Newala, ukishuka newala stand utachukua boda boda ziendazo Nkunya.
Boda boda itakuchukua mpaka mpakani, utagonga paspoti upande wa Tanzania, hivyo safari ya boda boda Itaendelea mpaka Ruvuma.
Ruvuma utapanda mtumbwi utakao kuvusha mpaka ng'ambo ya mto.
Ng'ambo ya mto utaikuta magresheni ya Mocambique, hapo napo utagonga paspoti yako.
Hapo Magresheni ya Mocambique utakutana na gari za mpakani, itakayo kupeleka mpaka Mueda (wilaya ya kwanza, ya mkoa wa Cabo del Gado ukitokea newala)
Mweda ukimuuliza mtu yeyote kua unakwenda Shapa kwa mzee LUPATU, hata mtoto mdogo atakupeleka.