Luqman Maloto: Wataalam ni chukizo kwa wanasiasa

Luqman Maloto: Wataalam ni chukizo kwa wanasiasa

Johnny Sins

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
2,537
Reaction score
3,873
FEBRUARI 7, mwaka huu, China ilimpoteza daktari bingwa wa macho (ophthalmologist), jina lake ni Li Wenliang. Alikuwa kijana mdogo. Oktoba 12, mwaka huu, angetimiza umri wa miaka 34.

Wenliang alikuwa anahudumu kwenye Hospitali Kuu ya Jiji la Wuhan. Desemba mwaka jana, alikuwa mtu wa kwanza kuushitukia mlipuko wa ugonjwa mpya unaosababishwa na virusi hatari. Ni baada ya kushuhudia, vilevile kushiriki kuhudumia wagonjwa waliokuwa na alama pamoja na dalili za tofauti.

Kuhakikisha anaokoa wenzake, Wenliang aliwajulisha wafanyakazi wenzake 30 kwa njia ya mtandao wawe makini na wagonjwa wapya, maana ilionekana wana alama na dalili zenye kushabihiana na homa ya SARS, iliyoua watu 774 barani Asia kati ya mwaka 2002 na 2004.

Tahadhari hiyo ya Wenliang kwa wafanyakazi wenzake wa Hospitali Kuu ya Wuhan, ilivuja mpaka kwenye mitandao ya umma. Ikawa si siri tena. Hilo lilimponza Wenliang mbele ya hukumu za wanasiasa.

Mamlaka za China zilimfungulia mashitaka Wenliang kwa kutoa habari za uongo mitandaoni. Kisha, Wenliang akafutiwa leseni ya udaktari. Akazuiwa kuhudumia. Wenliang akakosa ajira.

Kisha, taarifa za Wenliang zilikifikia Kituo cha Kimataifa cha Udhibiti wa Magonjwa na Kinga (CDC), kisha CDC kwa kushirikiana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), waliwezesha kubaini sifa ya virusi husika na kuviita SARS Coronavirus 2.

Wenliang alisema wagonjwa waliofika au kufikishwa Hospitali Kuu ya Wuhan, walikuwa na alama na Dalili kama za SARS, ugonjwa ambao huenezwa na virusi SARS Corona.

Baadaye WHO walitangaza kuwa ugonjwa uliolipuka Wuhan, China, Desemba mwaka jana na unaoitikisa dunia hivi sasa unaitwa Covid-19 na unasababishwa na maambukizi ya virusi vya SARS Corona 2. Yaani virusi vya Corona vyenye kusababisha SARS, toleo la pili ndilo linasababisha Covid-19.

Jiulize; Wenliang alikuwa muongo?

Kisha, Wuhan ilipozidiwa na wingi wa wagonjwa wa Covid-19, ikabidi Wenliang arejeshwe hospitali kuokoa maisha ya wagonjwa.

Kisha, Wenliang aliambukizwa Corona katika harakati za kuokoa maisha ya wagonjwa wa Covid-19. Kisha, Wenliang alifariki dunia akiacha mke na mtoto mmoja.

Kumbuka; Karne ya 17, Galileo Galileo alikufa dhalili kwa kutengwa, sababu alisema dunia hulizunguka jua. Alizichukiza mamlaka zilizoamini kuwa jua ndio huizunguka dunia. Leo, sayansi rasmi inakubali ugunduzi wa Galilei.

Yalimkuta Dk Mwele Malecela aliposema Tanzania kuna vimelea vya Zika. Yamemkuta Dk Nyambura Moremi kwa kuruhusu majibu 'mengi' chanya kuhusu Covid-19.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Analysis nzuri sana Kiasi hata Kupinga Inakuwa Ngumu... Hata Wapambe Wenye Elfi A...B...F na Z .. Umewaguza Kiasi Hawana Cha Kuchangia naamini Wote Watakuwa wanaandika neno moja tu nalo ni "SAWA". Hii Inahitwa Mkuki Makalioni na ni Chungu Kumeza,
 
Back
Top Bottom