Uongozi wa chama cha ACT WAZALENDO Jimbo la Chato Kusini umemkabidhi Fomu ya Ubunge Lushona Mathias mkazi na Mzaliwa wa wilaya ya Chato ili kwenda kupeperusha Bendera ya chama hicho huku akiahidi kwenda kutatua changamoto za wakulima , wafugaji pamoja wafanyabiashara wa Jimbo la hilo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Fomu hiyo , Lushona Mathias amesema wakulima wanashindwa kupitisha mazao yao katika baadhi ya barabara kwa kuwa mbovu na kupelekea kushindwa kusafirisha Mazao yao ipasavyo.