Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Katika rasimu ya katiba mpya, mswada unapendekeza elimu ya kiwango cha kuanza mtu kutafuta nafasi ya ubunge walao iwe elimu ya sekondari. Naridhika na kiwango hicho maana elimu ya sekondari Tanzania inatalii mengi ya muhimu katika kuijua Tanzania na ulimwengu.
Livingstone Lusinde ambaye ni mbunge wa bunge la Muungano na la katiba, akiwa Dodoma katika vikao vya katiba kama mjumbe amethubutu kusema hakubali kuzaliwa kwa Tanganyika. Kwa maneno mengine mpaka leo Mbunge huyu hajui kama Bara ni Tanganyika ambayo inaitwa Tanzania inapokuwa Jamhuri ya Muungano na visiwani.
Simshagai kwa vile kiwango cha elimu ya msingi alicho nacho vigumu mno kuelewa hata historia ya nchi yetu. Jambo la kushangaza Mbunge anapoongelea na kufikiria dhana ya kuzaliwa Tanganyika leo wakati taifa hilo lilishakuwepo zaidi ya karne mbili zilizopita.

