Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Akichangia katika bunge la JMT Mbunge wa Mtera Lusinde ameitaka serikali izingatie matokeo ya sensa katika ugawanywaji wa huduma za kijamii kama shule, hospitali na barabara, anasema huduma hizo lazima ziwe na uwiano na idadi ya watu katika eneo husika.
Ameshangaa kuna maeneo yenye watu wengi yana idadi ndogo ya huduma huku kuna maeneo yenye watu wachache yana huduma nyingi, ametaka kusiwepo na upendeleo wa aina hiyo.
Waziri Kitila Mkumbo amemuhakikishia Lusinde serikali inazingatia idadi ya watu kupitia sensa katika ugwaji wa huduma za jamii.
Hii ilikuwa fursa nzuri kwa wabunge wanaotaka majimbo ya uchaguzi kugawanywa au kuunganishwa kumuuliza Waziri Kitila kama pia serikali inazingatia idadi ya watu kupitia matokeo ya sensa katika ugawanyaji wa majimbo ya uchaguzi.
Lusinde, unakubali pia matokeo ya sensa kutumiwa kugawa majimbo kama ilivyo katika huduma za jamii?