Uchaguzi 2020 Lusinde: Mimi nilikuwa na Lissu Bungeni, hajawahi zungumzia maendeleo ni malalamiko tu na ndiyo maana nilikuwa namuita Malalamiko FC

Uchaguzi 2020 Lusinde: Mimi nilikuwa na Lissu Bungeni, hajawahi zungumzia maendeleo ni malalamiko tu na ndiyo maana nilikuwa namuita Malalamiko FC

Duh, hoja za CCM ni full futuhi
CCM wanatapa tapa, huko CCM wana watu hujiita ni wasomi lakini hawathubutu kuwatumia humtumia mwimba taarabu ndipo ujue CCM hawana hoja tena wamebakia kutengeneza propaganda za kijinga kishamba na kishetani
 
Huyo mropokaji wenu hawezi kufikia hata kura za membe! Mark my words Mkuu
Kama kura ni zile za kugawiwa na NEC, sawa. Kwa kura za wananchi, habari yake mtaisikia. Safari hii natabiri matokeo yatachelewa kutangazwa kwa sababu ya kupika matokeo kama 2010!
 
Ndicho mnacho Jifariji nacho sio! Mna waweza Mabeberu!?
CCM wakienda ulaya kuomba omba misaada huwaita wazungu wafadhili wahisani lakini hao hao wazungu wakikataa Upumbavu wa CCM hugeuka na kuwaita wanaume wenzao mabeberu utazani CCM ni mbuzi jike
 
Matokeo yatakuwa live na hakuna atakayeibiwa kura

Kupata kura sio kwenda sokon na stend kuhutubia ili kumfurahisha robertison wa Amsterdam
Kama kura ni zile za kugawiwa na NEC, sawa ...... Kwa kura za wananchi, habari yake mtaisikia. Safari hii natabiri matokeo yatachelewa kutangazwa kwa sababu ya kupika matokeo kama 2010!!
 
Mkuu kumbe Hilo unalijua hata wewe.
Unaona je ukiandika waraka kwa chadema kuwashauri wasitishe Kampeni zao njiani ili wasiendelee kupoteza HP za mwili angali mshindi anajulikana.

Mshindi hajulikani, ila Magufuli ndio anashurutisha kutangazwa mshindi, acha cdm washiriki ili ifahamike kuwa ccm iko madarakani,iwapo itatangazwa bila ridhaa ya wananchi. Kama mlitegemea kushinda bila kushindana basi imekula kwenu.
 
Mmeanza kuweweseka hata wiki mbili za kampeni hazijaisha
Tutawatandika kipigo cha mbwa mwizi huu Uchaguzi

Sio kwa kura boss, hilo mtasubiri sana. Labda kutandika kama ule uchaguzi wa SM.
 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Lusinde amewaonya wagombea wa vyama vya upinzani waache kutumia muda mwingi kueneza uongo na kumshambulia mgombea wa CCM, John Magufuli...
Great thinkers tunapelekea kuwajadili wapuuzi kama Lusinde?

So JF has gone that much low? Acheni kutuaibisha bwana! Hapa sio mahali pa kujadili asemacho MTU kama Lusinde ambaye amejipambanua mbele za hadhira kuwa ni mbumbumbu
 
Mlipewa nguvu na Lowasa mkajiona mnaweza kushinda Uchaguzi

Mrudi kwenye chama cha familia

Lowassa alileta nguvu gani, kwa taarifa yako Lowassa ndio alitukia nguvu ya cdm, vinginevyo angeenda chama kingine nje ya cdm, angekuwa kama Membe hivi sasa. Narudia tena, chini ya Magufuli hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Mbona unaanza kuinua mikono mapemaaaaaaa kunani?

Niinue kwa kipi, hapa nakueleza ukweli hakuna uchaguzi chini ya Magufuli, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Mbona hili liko wazi.
 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Lusinde amewaonya wagombea wa vyama vya upinzani waache kutumia muda mwingi kueneza uongo na kumshambulia mgombea wa CCM, John Magufuli.
ndiyo kampeni zenyewe. Yeye anatakaje sasa ? Ngoja waje kumshukia na yeye sasa
 
Mshindi hajulikani, ila Magufuli ndio anashurutisha kutangazwa mshindi, acha cdm washiriki ili ifahamike kuwa ccm iko madarakani,iwapo itatangazwa bila ridhaa ya wananchi. Kama mlitegemea kushinda bila kushindana basi imekula kwenu.
Hata ueleweki unachokiamini.
 
Hatuwezi kususia Nchi wahuni tumewapa miezi miwili ya kuropoka

Baada ya October nidhamu itawale na yule jamaa enu arudi ubeliginyi[emoji3]
Mafisi takataka haya badala ya jibu hoja,hayajibu yanatangatanga tuu,jibuni nani alimpiga Risasi au mkamateni dunia ijue,alafu anachhongea Lissu ni kuwa watu maisha yamekuwa magumu sasa jibuni hoja kama kweli sio magumu,wafanyakazi wa serikali hajapandishwa mishahara miaka 5,jibuni kweli au uwongo,watu wameporwa hela zao na kufilisiwa Semeni ni kweli au uwongo,nchi wananchi hawana furaha wamekuwa waoga semeni kweli kwa nini sio ohhh Lissu kafanyaje,mmeshikwa kubaya Mavi nyie wauaji.
 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Lusinde amewaonya wagombea wa vyama vya upinzani waache kutumia muda mwingi kueneza uongo na kumshambulia mgombea wa CCM, John Magufuli.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dodoma, Lusinde alimnyoshea kidole mgombea wa urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu akimweleza kuwa anapaswa kuzungumzia sera na kuwaelezea atawafanyia nini wananchi badala ya kutumia kampeni kumshambulia Magufuli.

Alisema ili kuondokana na hali hiyo, katika Bunge lijalo atapendekeza Sheria ya Uchaguzi ibadilishwe ili kuthibiti vyama vinavyoacha kunadi sera na kushambulia wengine.

"Haiwezekani kuwa na mtu muda wote analalamika tu, mimi nilikuwa na Lissu (Tundu) bungeni hajawahi zungumzia maendeleo ni malalamiko tu na ndio maana nilikuwa namuita Malalamiko FC, kimekuwa chama cha malalamiko na kuzungumza kashfa na kejeli.” alisema na kuongeza;

"Wana bahati mwaka huu Mwenyekiti wetu (Rais Magufuli) ametukataza kuzungumza kashfa wakati wa kampeni. Nilikuwa nimeagiza kontena tatu hivi na zilikuwa zimefika bandarini, shughuli ingekuwa nzito, wamshukuru Rais Magufuli alivyowabeba amekemea hataki kampeni za matusi wala kashfa, lakini tunavumilia inafika mahali tutashindwa."alisema Lusinde.

Alisema Lissu alishambuliwa na linajulikana, ila si sahihi kusema serikali ilihusika na ameliomba Jeshi la Polisi limtafute muhusika ili serikali isiendelee kuchafuliwa.

"Pia Lissu amekuwa akiziimba risasi 16 je ndio ilani?, anasema wananchi wanahofu, mbona yeye tangu afike hapa nchini hatujamuona akiwa na barakoa na anatembea kila mahali bila hofu na kwa uhuru, sasa hiyo hofu ya kwa wananchi iko wapi? aache uongo na azungumzie sera kama wanazo,"alisema Lusinde.

Alisema Rais Magufuli amejipambanua kuwa ni mwadilifu na mzalendo mwenye lengo la kuifanya Tanzania kupiga hatua za maendeleo huku akifanya kampeni kistaarabu bila kumshambulia mtu na kuomba kura kwa watu wote.

"Ameomba kura hadi upinzani wamchague, hajambagua mtu, hajashambulia mtu, muda wote anapambana kuhakikisha anapata ushindi wake na chama chake ili kuendelea kuwatumikia wananchi katika miaka mitano mingine,"alisema.

Kuhusu mgombea wa nafasi ya urais wa Tanzania kwa chama cha ACT Wazalendo, Bernad Membe mgombea Lusinde alimshangaa kuendelea kupiga kampeni muda mrefu katika mkoa mmoja na kusema wagombea kama hao wanapoteza muda na kuitia nchi hasara.

"Wakati mgombea wa CCM, Rais John Magufuli akiwa amefikisha mikoa tisa kwenye kampeni zake na kukanyanga kiatu kweli kweli, mgombea wa ACT-Wazalendo bado yuko Lindi, sijui anagombea urais wa Lindi au wa kijiji cha Londo, baadaye hawa wagombea watapiga kelele kuwa wameibiwa kura, nataka Watanzania walione hili mapema."alisema Lusinde.

Alisema Mkoa wa Dodoma umeamua kura zote apewe Rais Magufuli kutokana na kuibadilisha sana jiji hilo. "Tunataka kuvunja rekodi ya kumpa ushindi wa kishindo Magufuli ili awe na deni kwa Watanzania litakalomfanya apige kazi kwa kiwango cha kutisha nchi isonge mbele. Magufuli sio mtu wa kusafiri nje ya nchi, lakini ameweza kuibadili nchi kwa kiwango kikubwa na kuifanya maeneo mengi yanafanana na nchi za nje."alisema.
Huyu leo hii angekuwa mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, muda huu Magufuli angekuwa anacheka hadi jino la mwisho bahati mbaya hila zao zimezimwa mapema sana, muda huu maccm yote yameloa jasho hadi mattercore ni
 
Back
Top Bottom