Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Luteni Jenerali wa ngazi ya juu Igor Kirillov ambaye ni Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi cha Nyuklia, Biolojia, Kemikali (NBC) katika Jeshi la Urusi na Msaidizi wake wameuawa katika mlipuko uliotokea mjini Moscow.
Jenerali huyo alikuwa akiondoka kwenye makazi mapema Jumanne wakati kifaa kilichofichwa kwenye skuta (Scooter) kilipolipuka, Kamati ya Uchunguzi ya Urusi.
Vyanzo vya usalama vya Urusi vililiambia Shirika la Habari la Serikali Tass kuwa kifaa hicho kililipuliwa kwa mbali.
Siku ya Jumatatu, huduma ya usalama ya Ukraine ilimshtaki Kirillov bila kuwepo mahakamani, ikisema kwenye Telegram kwamba "alihusika na matumizi makubwa ya silaha za kemikali zilizopigwa marufuku". Serikali ya Ukraine bado haijatoa maoni yoyote kuhusu kifo cha jenerali huyo.