Luteni Jenerali wa ngazi ya juu wa Urusi, Igor Kirillov auawa kwa bomu lililotegwa kwenye ‘scooter’

Luteni Jenerali wa ngazi ya juu wa Urusi, Igor Kirillov auawa kwa bomu lililotegwa kwenye ‘scooter’

Tuangane kuombea Aman dunian maana wanaoumia ni wale wanyonge na masikin

Fikiria kuhusu maisha ya wapalestina na Lebanon ndugu zetu Sudan na Kongo inatia huruma sana Sudan wanateseka aisee huku mabomu huku mafuriko

YESU KRISTO afanye Aman kwa watu wote
Yesu Kristo kamwe hatafanya Amani kama wahusika hawaihitaji amani hiyo. Halizimishwi mtu hapa. Yani waathirika wenyewe hawana ushirikiano, hawamsikilizi huyo Yesu na wala hawaoneshi juhudi zozote za kuisaka hiyo amani. Sasa kwa nini kumsumbua Yesu eti afanye amani? Njia walioichagua wao kwa hiiari yao, Yesu hawezi kuwalazimisha kitu tofauti. Sana sana atawaacha na muda ukipita ndo watajifunza na kuighairi njia hiyo. Ukisoma Mathayo 7: 7-8 inamaanisha lazima zifanyike juhudi za makusudi (binafsi au jamii) ili kukipata kile tunachahitaji. Ukilala au ukilaza damu utabaki kama ulivyo.
 
Luteni Jenerali wa ngazi ya juu Igor Kirillov ambaye ni Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi cha Nyuklia, Biolojia, Kemikali (NBC) katika Jeshi la Urusi na Msaidizi wake wameuawa katika mlipuko uliotokea mjini Moscow.

Jenerali huyo alikuwa akiondoka kwenye makazi mapema Jumanne wakati kifaa kilichofichwa kwenye skuta (Scooter) kilipolipuka, Kamati ya Uchunguzi ya Urusi.

Vyanzo vya usalama vya Urusi vililiambia Shirika la Habari la Serikali Tass kuwa kifaa hicho kililipuliwa kwa mbali.

Siku ya Jumatatu, huduma ya usalama ya Ukraine ilimshtaki Kirillov bila kuwepo mahakamani, ikisema kwenye Telegram kwamba "alihusika na matumizi makubwa ya silaha za kemikali zilizopigwa marufuku". Serikali ya Ukraine bado haijatoa maoni yoyote kuhusu kifo cha jenerali huyo.

View attachment 3178789
Nawabs hii issue ingetokea Iran sifa Za Mossadi zingemiminika kila Kona
 
Upuuzi ya kujipa matumaimi hewa
Upuuzi upi!?
Hizo ndio lugha zinazotumika kwa makamanda Though matokeo ni yale yale.
Kwa mfano huwezi kusema binadamu amekufa
Au ng'ombe amefariki
Binadamu anafariki
Ng'ombe anakufa
Jitahidini kielewa hv vitu vidogo vidogo
 
Back
Top Bottom