Njimba,
Mponjoli hakuwa mjinga kama unavyofikiri. The guy was actually smarter than most of his agemate. Issue ni kwamba alichagua kutumia akili zake kwenye masuala ya wizi. Na alikuwa damn good at it. Otherwise, he could have been whatever he wanted to be.
Alikuwa fast mno....yeye kila kitu kwake ni fasta fasta tu. Na alikuwa very accurate na dili zake. Nakumbuka alipokuwa Dallas, alishawahi kuchonga dili ya kuibiwa gari. Na alifanikiwa kuvuta check kutoka insurance bila ya kubumburuka. Na hata dili za kwenda upfront bank, alishazifanya sana na kufanikiwa (ninazungumzia ya kati ya $1000 - 20,000). Alichokosea step ya dili ya bank iliyomkamatisha ni kiasi cha $ alichotaka kuvuta, plus nafikiri tayari alishakuwa kwenye survilliance by then. Na mwenyewe alishajua kuwa tayari yuko kwenye survilliance, kwa hiyo alitaka kuvuta hela kubwa na kuingia mitini kurudi bongo kimoja.
Kuna vitu viwili vikubwa ambavyo vilikuwa vinamwangusha Mponjoli. Wanawake na wapambe. Jamaa alikuwa anapenda mambo ya chumbani sijawahi ona. Mshikaji yaani alikuwa akiona demu anatetemeka kwa uchu. Na ikibidi hata afunge baa kwa kujaribu kum-impress yule demu, atafanya hivyo. Mambo mengine aliyowahi kuyafanya kukiwa na mwanamke around ni mpaka aibu kuyaelezea. Nafikiri mpaka anaondoka U.S. alishakuwa na watoto kama watatu (not sure)wenye mama tofauti. Mwenyewe alikuwa anakiri kuwa uzinzi amechukua kutoka kwa baba yake. Alikuwa anasema kwao wako wengi kinoma.
Wapambe ni issue nyingine. Jamaa alikuwa anawapambe wengi mno. Yaani Dallas bila ya Mponjoli ilikuwa haiendi. Alikuwa kama baba yao vile. Alikuwa akienda kwenye zile party za kibongo (Houston, DC, na Columbus) na wapambe wake, atawalipia airline ticket, rent a car, mpaka hotel fair. Yaani jamaa alikuwa celebrity fulani huko Dallas. Alipokamatwa, wabongo wengi Dallas walikuwa kama wamemwagia maji kwa kunywea. Dallas bongo community has never been the same ever since. Hata kukamatwa kwake kunahusishwa na whistleblow kutoka kwa baadhi ya wapambe wako aliokosana nao kwa namna moja au nyingine.
(Disclaimer - baadhi ya mambo niliyoyaandika hapo juu ni hearsay. So don't hold a gun on me)