Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
LWAKATALE, SILINDE NA WENZAO WAMEONEWA SANA NA KUDHALILISHWA SANA
Sitaki kujadili juu ya uhalalia ua kutokuwa halali kwenda au kutokwenda Bungeni hili lingeitimishwa na sheria na Miongozo ya CHADEMA kama ingefuatwa wakati wa kuhitimisha jambo lenyewe. Mimi nitajikita kwenye sheria na kanuni zenyewe.👇🏼
KATIBA NA KANUNI ZA CHADEMA ZINASEMA NINI?
Kwanza niweke usahihi kuwa katika chama cha Siasa Katiba ndiyo sheria mama ndiyo maana marekebisho yoyote yanapofanyika hayawezi kufanywa na mtu mmoja.
Lakini kanuni ni muongozo wa chama na marekebisho yaweza kufanywa na mtu yeyote anayeruhusiwa kufanya hivyo. Mfano CHADEMA sheria inampa nafasi katibu mkuu kufanyia marekebisho kanuni za chama pale anapoona inaleta tija. Pamoja na hayo yote hakuna mtu yeyote awe kiongozi au Mwanachama mwenye mamlaka ya kwenda kinyume na ama Katiba au Kanuni.
KWANINI LWAKATALE, SILINDE NA WENGINE WAMEONEWA?
Katiba ya CHADEMA toleo la Mwaka (2019) ibara ya 5.4 na vifungu vyake inazungumzia "kukoma kwa uanachama"
Nitaweka hapa ili twende pamoja.
5.4.1. kwa kujiuzulu mwenyewe kwa hiari yake.
5.4.2 kutokana na kufariki.
Msingi wa hoja yangu ni hapa;
👇🏼
"5.4.3 Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya chama,kwa mujibu wa katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo usioendana na Itikadi,Falsafa,Madhumuni,Kanuni,Maadili na Sera za Chama. Mwanachama atakuwa na haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na adhabu hiyo."
Yawezekana kabisa pasipo chembe ya shaka kuwa Lwakatale, Silinde na wenzao wamekiuka hicho kifungu cha katiba na kupelekea kukoma uanachama.
Nini kilipaswa kufanyika kwa mujibu wa katiba hiyohiyo ya CHADEMA?
👇🏼
Ibara ya ;
5.4.4 Bila kuathiri kifungu cha 5.4.3 cha Katiba Kamati Kuu inaweza kumuachisha ama kumfukuza mwanachama yeyote kwa mujibu wa Kanuni za Chama
Nikweli Kamati kuu inayomamlaka kamili na nguvu zote kuwafukuza Lwakatale, Silinde na wenzao na imefanya hivyo. Tatizo kubwa nini hasa? Kwanini waendelee kulalamika? Kwanini jamii inawatetea? Ni kosa la Spika wa Bunge? Nikweli kosa ni CCM? Hapana hayo yote hayawezi kuwa matatizo.
TATIZO NI KAMATI KUU CHINI YA MWENYEKITI WANGU MH FREEMAN MBOWE
Tuone Kanuni za Chama CHADEMA zinasemaje kuhusu kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa Kiongozi kama Lwakatale, Silinde na wenzao;
👇🏼
Kanuni za chama
6.5.6 Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashtakak wa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashtaka kwa maandishi.
6.5.7 kiongozi muhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi,atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidham
6.5.9 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya msingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ilik umuwezeaha kuamua kukata rufani au la.
Sasa ndugu zangu!
Hapo Lwakatare , Silinde na wenzao wanakosa gani? Tusijadili masuala haya kishabiki na kuweka kanuni na miongozo yetu pembeni. Kwanini tunaacha kutoa boriti kubwa kwenye mboni za macho yetu na tunakwenda kuhangaika na kibanzi kidogo pembezoni mwa jicho la Spika? Hivi kama tungefuata taratibu stahiki na miongozo ya chama katika kuhitimisha safari ya wenzetu ndani ya chama kulikuwa na tatiz gani?
Ndugu yangu Tundu Lissu nakuheshimu sana sana kiongozi kwanini hukushauri hili jambo la kisheria wakati wewe ni muumini mkubwa wa kuchukia matumizi mabovu na uvunjwaji wa Sheria? Kaka yangu Lema utu wa mwanadamu na kheshima kwa hawa wenzetu waliokiuka maagizo na tamko la chama kwanini hujawatetea?
Ndugu zangu, zamani tulikuwa tunaanza na Mungu kisha tunamaliza na Mungu kwenye hili la akina Lwakatale, Silinde na wenzie mlipata hasira kiasi gani hata mlishindwa Kuanza na Mungu kisha kumaliza na Mungu ili kuweka kumbukumbu sahihi? Kaka yangu Mchungaji Msigwa hapa neno la kichungaji katika ugawaji wa haki linasema nini hasa,tumeamua kufanya yaleyale ya akina Pilato enzi za kesi ya Yesu? Dada yangu Halima hapo vipi, Mbona kama hapajakaa sawa? Myika kaka wewe ni katibu Mkuu cheo ambacho najua unakimudu maana umekulia hapo lakini unawezaje kujitokeza kutangaza maazimio ambayo kwadhamira ya dhati kabisa unajua yanahila ndani yake? Hata kama ni kuwachoka wenzenu kwanini msifuate sheria mbona bado ninyin diyo wenye mamlaka na madaraka ya kuhitimisha hayo hofu ya nini?
Mshaurini Mwenyekiti vizuri hizi frastruations za kisiasa zisifanye muumizane kwa namna hii. Tanzania bado tunahitaji upinzani makini na wenye weredi ili kujenga na kuendeleza siasa za ushindani.
Baraza la vijana Bavicha kisima cha tafakuri lilifutwa? Au ndiyo kila jambo litakalo fanywa na kuamriwa na kamati kuu linakuwa sahihi? Wale ni wanadamu waambieni hii fukuzana bila kufuata taratibu utakua mchezo utawanogea kesho yenu itakua ngumu sana hasa kufikiri tofauti na wakubwa.
Hawa tunao washughulikia leo bila kufuata taratibu na kanuni zetu niwenzetu tumeumia pamoja, tulilala pamoja na tulimaliza pamoja. Siyo lazima kuwatunza wanapokosea lakini kufuata sheria kuna shida gani ili kuhitimisha vyema?
Haya, sasa leo tunawezaje kufungua katiba ili kumzodoa Spika wakati tumejaa Uchafu na dhurma kwenye mikono yetu? Kuna pahala hapajakaa sawa.
WAPENDA DEMOKRASIA KEMEENI HILI KWANI KIMYA CHETU NI HATARI KWETU NA KWADEMOKRASIA YETU, KULIKO KELELE ZA MAADUI WA DEMOKRASIA YETU.
Philipo Mwakibinga
0758910403