Lwakatale, Silinde na wenzao wameonewa sana na kudhalilishwa sana

Hizi sio nyakati za kina sultani na mwinyi kwamba amri inatoka sehemu moja tu,inatekelezwa...Karne ya 21 hii.Hadi Iran anamvimbia Marekani....Wakati wa amri amri ushapita.
Naam, CHATO ikisha-amua hakuna wa kupinga, iliamuru washughulikiwee bungeni na nje yeye atawashughulikia, ikawa, mtu akala 37 za mguu na kiuno.
Aliagiza matajiri waishi kama mashetani na maskini waishi kama malaika, na ikawa.
akaagiza, upinzani ufutwe by 2020, unafutika, kama si yeye atafutika.
 
"Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashtaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashtaka kwa maandishi"

EGOS, UMWAMBA, UMIMI, KUONYESHANA nani Kidume zaidi etc vimetumika kwenye sakata zima na hili halihitaji kuwa sugar-coated. Kama kanuni za chama zinasema mtu lazima apewe wito wenye makosa yake na aitwe kujieleza, no matter what, lazima hilo lifanyike. Huwezi kusema "ooh, hakukuwa na haja ya kuwaita kwa kuwa walikuwa wanatoa kashfa hadharani". Chama makini kilipaswa kuonyesha njia mbadala.
 
Huyo anayewapa jeuri hana chama...CCM ina wenyewe mtadhalilika sana kisiasa msipokuwa makini

Alishasema Jiwe kuwa wakienda huko ccm watakuwa sawa na ng'ombe waliokatwa mikia!!!
 
Hawajaonewa
Watu wanafanya mzaha na maisha ya WaTz
Mbowe yupo sahihi 💯
Ondoa wahuni wapo wengine watakuja
 
mbona unarukaruka.yani wewe na elimu yako ndo unamawazo ya namna hii!!.aibu sana.
nimekuuliza swali kwa nini mtu akienda kinyume na mwenyekiti mnasema kanunuliwa ?
rwakatare kanunuliwa shilingi ngapi ?
mwenyekiti anakivuruga chama kwa speed kali sana watu makini wametoka woote yamebaki makapi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu walifanya kile wanachokiona kinafaa kama watu wazima,na Chama chao kikafanya kinacho wafaa ngoma drop,Acha wengine katika majimbo yao wachukue fulsa na watachukua kweli,uchaguzi Mkuu sio mchezo kipindi hicho kila MTU anakua anapambana na hali yake.Na tabiri mwaka huu kesi za washiriki ubunge za kupinga matokeo mahakamani zinaweza kua nyingi hadi kuvunja record maana hakuna mgombea atakae kubali kuporwa ushindi wakati ana ushahidi wa kutosha na ushindi wake moto utawaka.
Na ndo maana huwa nashangaa mdau humu jamvin akisema wabunge wa chama tawala watarudisha majimbo yote.Hakuna kitu kama icho maana wakati unapanga ili kwamba tiyari umemaliza kazi mwenzako anakua tiyari ana mipango zaidi ya iyo.
SISI wengine tunasubili mgombea binafsi sijui itakua lini sijui mpaka yesu akirejea!!
 
Mtoa nada nyumbani kwako mmekubaliana wewe na familia yako(mkeo na watoto) kwamba hakuna kutoka nje kwa Nia njema. Mara paap mkeo katika nje Tena we umekaa barazani kwako unamuona akitoka.

Kisha anamkuta jirani yako anasema " huyu fala kaamua tu nisitoke, mi nimeamua kutoka".... Utafanya maamuzi gani?

Lakini pia tumeona waliotoroka quarantine walifuatwa na polisi na kukamatwa.

Hayo yalikuwa maamuzi ya wote hivyo wote walipaswa kuyatii pasipo na uvunjifu wa taratibu Kama wanavyokubalianaga kutoka bungeni pale kuliwa na Jambo lililokuwa na maslahi mapana ya taifa.

Chadema are right.

Mbona hata CCM wamemfukuza MEMBE
 

KUNYA anye kuku akinya bata KAHARISHA
 
“Nimepokea maamuzi ya Kamati Kuu CHADEMA na imenitaka nitoe malezo (ya kuingia Bungeni kinyume na agizo la Chama), niseme kwa hatua ya sasa nimepokea agizo la Chama, na ni kwanini nilifanya hivyo nafikiri Chama nitakiambia, kama nitaona kuna sababu ya kuwaelezea jamii au wapiga kura wangu hiyo itakuwa hatua nyingine”-Peter Lijualikali, Mbunge Kilombero.
 
Ni kweli Wamekikosea Chama na viongozi. Tatizo ni TARATIBU za kikatiba hazikufuatwa. Wataalam wa Sheria wanasema " unfair termination"
Watarudishiwa uanachama kwa sababu TARATIBU hazikufuatwa.
 
Unfair Termination
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…