Kwa kuwa ushirikiano umeshindikana, wanasiasa mahiri lazima waamue uwanja wao kufanya siasa-ama CHADEMA au CUF. Kwa maoni yangu sioni kwa nini Lwakatare aendelee kubaki huko alipo. Kimsingi hana sababu!
Mtanzania,
Haya ulioandika para ya mwisho ni kweli na huwa inafanyika. Ni lazima uelewe kila kitu kina wakati wake. Kuna wakati wa kufanya uliyosema na kuna wakati wa kukaa pamoja kuzungumzia yaliyofanyika. Kama unataka tukae shambani kila siku, ina maana hakuna siku tutapika na hakuna siku tutakula. Unaposema kila siku watu wanaandamana barabarani si kweli maana hujasema ni mara ngapi umeona haya yakifanyika. Nadhani na wewe umesukumwa tu msimamo wa ki si hasa.
Na pia ninakushauri uzungumze na raisi wetu MH. sana JMK na serikali yake ambao wao ziara zao haziishi mikoani na kimataifa. Tena hawa ufanya kwa gharama za kodi yetu wavuja jasho.
Mwisho hawa vijana si wajinga. Siasa ni sehemu ya maisha yao ni lazima waijadili. Maana walipojaribu kunyamaza kuijadili tu hapo wajanja wakaona ndio nafasi ya kuliibia taifa na wamepora kweli kweli mpaka nchi imebaki hoi.
viongozi wetu hawaoni haya kuita nchi yetu eti ni maskini. Wanashinda kuomba omba na wanaona fahari hata kututangazia kwa ufahari kwamba waliomba pesa na wamepewa au mara nyingine utasikia upuuzi kama niliosikia siku mbili zilizopita kwamba umaskini wa wazungu utatutia matatizoni! kwa nini? eti kwa sababu misaada itapungua. Huu ujinga ujinga tu. Vijana wasipojadili siasa hata kazi wanazofanya hazina maana. Ninachojua kuwa ni hakika maandamano hayo yalihusisha wote, vijana na watu wazima na ajabu wengi wanafanya kazi za vipato na kwa bidii kweli kweli.
Ebu nikuulize Mtanzania hata ukifanya kazi masaa 18 katika nchi hii ya wadanganyika kuna lolote utavuna? Sana sana utaishia hali ile ile ya umaskini tu. Na unajua kwa nini? Kwa sababu sisi ni wadanganyika na tunadanganywa na chama hiki cha majambazi. Hakika kama nchi itaendelea kuwa chini ya SISI M hatutapata maendeleo kamwe. Maana jitihada zetu wanazimaliza wao.
Mkuu Mchukia Fisadi,
Naelewa hoja yako hapo juu, ila nitatofautiana na wewe kuhusu kuchapa kazi. Ukifanya kazi masaa 18 una nafasi kubwa sana ya kufanikiwa kuliko hao wanaoshinda kwenye magenge ya majungu ya siasa.
Ni kama tunatumia muda mwingi mno kwenye mambo ambayo hayaongezi tija kwa mwananchi wa kawaida.
Yaani kama vile upo bongo! Huku kazi siku hizi ni siasa, na siasa ni kazi! Kila mahala ukipita mjadala ni siasa. Na inaonekana kama vile huwezi kuchangia maendeleo mpaka uwe mwanasiasa!
Hata hivyo, haya maandamano ni changamoto kubwa kwa CUF. Maana walipomtema kwenye uongozi kiaina sidhani kama walijua nguvu yake huku Bukoba. Kimsingi Lwakatare ni nguzo nzito sana ya CUF huku bara, kiasi kwamba akinyanyua mguu akautua kwingine atakuwa ameisambaratisha kabisa nguvu ya CUF huku. If I were to be a devil's advocate, can we sustain two strong opposition political parties in TZ? Kwa kuwa ushirikiano umeshindikana, wanasiasa mahiri lazima waamue uwanja wao kufanya siasa-ama CHADEMA au CUF. Kwa maoni yangu sioni kwa nini Lwakatare aendelee kubaki huko alipo. Kimsingi hana sababu!
Nami nakuelewa mtz lakini wengi wamefanyakazi sana na mwisho wamekuwa frustrated na kufanya kazi kawaida.
Kama nchi hii tukiwa na system ya kulipwa kwa masaa hapo naweza kukuelewa. Lakini hii ya kushinda unaumia wakati hao wanasiasa wanapata pesa nyingi kuliko sisi! ni bora nikae kijiweni kuwasema🙂 Na nitawasema mpaka wanielewe.
Sasa basi mtz tuombe nchi hii tulipwe kwa kila saa unayofanya kazi pesa ya kueleweka uone kama watu watakimbilia katika siasa tena. Hao maprofesa, madaktari, mainjinia, waandishi wa habari n.k nakuambia hawatakwenda siasani. Maana siasani ndiko kuna malipo ya bure ambayo hatak ama mtu hajafanya kazi analipwa malipo manono.
Hatimaye nimekuelewa. Nitachapa kazi kwa bidii, na nitajihusisha na siasa at a go. Nitawajibika kikweli si mchezo. Nitaifukuzia shilingi kweli kweli na siasa sintaiacha nyuma. Mimi ni mjasiliamali wa wajasiliamali tangu miaka ya 1984 na najituma kweli. Niko kazini mara nyingi masaa 17 na 19 kila siku na naona hali inatisha. Sikati tamaa bali nitaongeza bidii kwa yote Kazi na siasa. 2010 nitaongeza bidii katika siasa angalau na mimi niukwae ubunge niingie mujengo maisha yatabidilika zaidi maana huko ndiko kwetu wanasema kuna chungu cha mboga ya wanaume😀Mchukia Fisadi,
Unataka ulipwe na nani? Unaweza kufanya kazi za kujisaidia mwenyewe na familia yako. Pia unaweza kusaidia kazi za kuendeleza jamii, sio lazima ushinde ofisini ukichapa kazi. Hata ukibaki nyumbani na watoto na kuwasaidia homework bado ni kazi yenye tija kuliko kwenda kuwashangilia/kuwabeba wanasiasa.
Kama ni uchaguzi mwaka kesho upo, tutapiga kelele sana, tutashangilia sana na pia tutazomea sana. Baada ya hapo turudi kuwajibika.
Sisi wenyewe tuliokubali kudanganywa na tukadanganyika ni WADANGANYIKA!
Ni ishara nzuri sana kwa Bwana Lwakatare lakini sijui ile kesi yake ya uchaguzi na mheshimiwa Kagasheki inaweza kumyima nafasi ya kugombea ubunge mwaka 2010.
Hee!!!
IMEKUWAJE TENA JAMANI! SI TULIAMBIWA HAPA KUWA LWAKATARE ANAHAMIA CHADEMA? LINI TENA KABADILI UAMUZI WA KUENDELEA KUWA CUF? PIA TUMEAMBIWA KUWA CUF NI CHAMA CHA WAPEMBA SASA HUKO BUKOBA PIA KUNA WAPEMBA!! JAMANI MAALIM SEIF WACHA KUSAFIRISHA MAMLUKI TOKA PEMBA HADI BUKOBA! SASA NA WEWE UMEANZA KUIGA TABIA ZA CCM ZA KULETA MAMLUKI WA KURA TOKA BARA HADI VISIWANI! AU HAYA YA SASA NDIO UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YENU YA CUF KUWA "NGOMA ITAKAVYO PIGWA NDIVYO MUTAKAVYO ICHEZA"?
Lwakatare alikuwa na kesi ya kujerui / kufanyafujo mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
Iwapo alikutwa na hatia mheshimiwa Lwakatare hatakuwa na sifa za kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.Ninavyojua Lwakatare alishindwa labda kama atakuwa amekata rufaa.
Surely he has fisadi's monies. Lets wait 2010 and see as I will go to Bukoba and put my name too as one of contestants, and see me, Kagasheki and Lwakatare who wins.Never underestimate Kagasheki,the guy is shrewd and well loaded!
Ni ishara nzuri sana kwa Bwana Lwakatare lakini sijui ile kesi yake ya uchaguzi na mheshimiwa Kagasheki inaweza kumyima nafasi ya kugombea ubunge mwaka 2010.
Never underestimate Kagasheki,the guy is shrewd and well loaded!