Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Gerva Bernard Lyenda amesema kuwa siyo sawa kuzungumzia uchaguzi ujao wakati ule uliopita haukufanyika kwa misingi sahihi.
Lyenda ameeleza kuwa CHADEMA inaendelea kusimamia msimamo wake wa "No Reforms, No Election" (Bila maboresho hakuna uchaguzi) kwani yaliyotokea Oktoba 29 hayakuwa uchaguzi halisi kutokana na ukosefu wa mageuzi ya kisheria.
Soma: PostGE2025 - Wakili Madeleka: "No Reforms, No Election" haiwezi Kufanywa Uhaini
Ameongeza kuwa hata aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Warioba, ambaye ni kada mwenye heshima kubwa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), alikiri kuwa uchaguzi haukufanyika, hivyo hakuna sababu ya kuitambua michakato hiyo kuwa halali.
Katika kufafanua athari za msimamo huo, Lyenda amesisitiza kuwa msimamo wa chama chake utadumu kwa muda mrefu ujao, hata ikibidi hadi mwaka 2030, iwapo hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya maana katika sheria za uchaguzi. Ametilia shaka pia takwimu za matokeo yaliyompa ushindi Rais Samia kwa kura milioni 32, akisema kuwa idadi hiyo haiingii akilini ukilinganisha na idadi ya jumla ya Watanzania na namna watu walivyoshiriki kupiga kura siku hiyo.