Lyimo naye... is he serious?

Elimu inayoongelewa ni hata ya kuwafanya wazee wetu wajue namna ya kutumia ardhi kwa uzalishaji mali. Waache utamaduni wa kulima nusu heka wakiachia ardhi imedumaa tu. Wajifunze umuhimu wa kutumia maji ya mito kwa kilimo pale yanapopatikana...wajue umuhimu wa kuwa na umoja na kuweza kuwabana viongozi wao juu ya masoko ya mazao yao...ifike mahali wao ndiyo wawe main suppliers wa agro product zilizoko super markets...ifike mahali wagome kulaghaiwa na madalali kwa bei hafifu...na ifike mahali bidhaa zao zithaminiwe na kununuliwa na wenzao walioko mjini, ili umuhimu wa kuwa na 40 million population iwe translated into a strong market base.
 
Je, yafaa tupendekeze thread hii iondolewe kwa sababu tu imeshaandikwa na kusemwa sana hapa JF?

hapa issue sio kuondolewa kwa thread ila issue ni kuwa hakuna cha kushangaa kuwa is Lymo serious? Sio vibaya ikikaa watu waendelee kujikumbushia mambo ya nchi yao. Kukumbuka hakuna ubaya.
 

Samahani Mkuu lakini kwenye hili nakubaliana na kilitime. Elimu tunayohitaji si ya Ph.D au madigrii mengine. Tunahitaji elimu basic inakayomwondoa mtanzania kwenye dhana kama bibi kizee mwenye mekundu anastahili kufa, pepo punda haitibiwi hospitali, mke ni mali ya mwanaume kumfanyia atakalo n.k. Elimu itakayomwezesha mtanzania wa kawaida kuhoji hali aliyokuwa nayo na kudai maendeleo halisi. Elimu itakayowafanya watanzania wa kawaida kuwa wa dadisi na kukataa dhana kuwa hali yake duni ni mapenzi ya mwenyezi mungu. Elimu itakayomfanya mtanzania wa kawaida kuwa na wivu wa kimaendeleo, kuwa na uchungu kutokana na hali yake. Elimu itakayomfanya mtanzania wa kawaida kudai kutoka kwa viongozi wake maelekezo yanayoeleweka yatakayomtoa kwenye umasikini aliokuwa nao. Elimu hii itamfanya adai kuambiwa ukweli badala ya platitudes kutoka kwa viongozi wake. Elimu itakayomwezesha mtanzania wa kawaida kuthamini mazingira yake akitambua kuwa yeye ni custodian tu kwa vizazi vijavyo. Elimu itakayomfanya mtanzania wa kawaida kutambua kuwa maendeleo yake yatatokana na yeye mwenyewe na si mwengineyo. hakuna donor country itakayotuletea maendeleo. Hizo Ph.D ni icing on the cake. Kwanza watanzania wa kawaida waelimike. Wapewe elimu itakayowawezesha kukabliliana na ulimwengu wa sasa. Bila kuwekeza katika elimu hatutatoka hapa tulipo kamwe. Inabidi tuangalie mfumo mzima wa elimu na si kuangalia idadi ya madarasa tuu. Quality ya elimu nayo ni muhimu kama si muhimu zaidi!
 
Wandugu,

Raisi wetu JK hajui kwa nini Watanzania ni masikini...sasa naona 2010 ni MUHIMU sana ya kuwa na Midahalo kabla ya kupiga kura.
 
Fundi Mchundo,

majibu inabidi yawe mengi, usijizuie hata kama hoja imejibiwa...nawe kwa mafumbo, imejibiwa wapi? Nisaidie tafadhali.
 
Fundi Mchundo,

majibu inabidi yawe mengi, usijizuie hata kama hoja imejibiwa...nawe kwa mafumbo, imejibiwa wapi? Nisaidie tafadhali.

Mkuu, wewe ni mmoja wa waliofafanua vyema sana kuhusu elimu ya aina gani ambayo Mheshimiwa Kilitime alikuwa anaongelea! Mimi nimejazia jazia pale ulipoanzia. Asante sana, mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…