Elimu inayoongelewa ni hata ya kuwafanya wazee wetu wajue namna ya kutumia ardhi kwa uzalishaji mali. Waache utamaduni wa kulima nusu heka wakiachia ardhi imedumaa tu. Wajifunze umuhimu wa kutumia maji ya mito kwa kilimo pale yanapopatikana...wajue umuhimu wa kuwa na umoja na kuweza kuwabana viongozi wao juu ya masoko ya mazao yao...ifike mahali wao ndiyo wawe main suppliers wa agro product zilizoko super markets...ifike mahali wagome kulaghaiwa na madalali kwa bei hafifu...na ifike mahali bidhaa zao zithaminiwe na kununuliwa na wenzao walioko mjini, ili umuhimu wa kuwa na 40 million population iwe translated into a strong market base.