elmagnifico
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 8,261
- 9,733
Mwaka 1989 ndugu wawili wajulikanao kama Lyle ambaye kwa sasa ana miaka 49, na Erik ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 46, waliowaua wazazi wao kwa kuwapiga risasi sehemu mbalimbali za miili yao.
Mauaji hayo yalitokea katika jumba lao la kifahari lililokuwa Beverly Hills, na kipindi hicho Lyle alikuwa na umri wa miaka 21 na Erik miaka 18.
Lyle ndiye aliyepiga simu ya dharura 911 kutoa taarifa kuwa wamerudi nyumbani na kukuta wazazi wao wameuawa.
Siku hiyo ilikuwa siku ya Jumapili ya mwezi wa nane mwaka 1989.
Baada ya polisi kufika eneo la tukio walikuta maiti mbili za watu maarufu waliokuwa wakijulikana kwa kila mtu, yani Bwana Jose na Mkewe Bi Kitty.
Polisi hawakuwa na wazo kabisa kuwa mauaji hayo yanaweza kuwa yamefanywa na vijana hao hivyo walibaki wakiowaonea huruma kwa kufiwa na wazazi wao.
FAMILIA YA LYLE NA ERIK
Lyle na Erik walizaliwa katika familia ya kitajiri yenye ukwasi wa kutosha. Baba yao Jose alikuwa kati ya wakurugenzi wa juu kabisa Hollywood, huku mama yao Kitty aliwahi kuwa mshindi wa taji la urembo, ambaye kwa muda huo alikuwa akijishughulisha na upambaji wa makazi pamoja na shughuli za kusaidia jamii.
Baba yao yani Jose, inasemekana alikuwa mkali sana, asiyependa masikhara hata kidogo linapokuja suala la masomo.
Pia inasemekana alikuwa na matumaini makubwa sana juu ya watoto wake akiwa anategemea waje kuwa watu wakubwa na maarufu huko mbeleni.
Lakini Lyle na Erik mara zote walishindwa timiza ndoto ya baba yao kwa kutofaulu vizuri katika masomo yao, pia walijihusisha na makundi ya wavuta bangi na madawa ya kulevya huku wakiwa wadokozi kwenye majumba ya watu jambo ambalo lilimkosesha amani baba na mama yao.
NINI LILITOKEA 20/08/1989
Lyle na Erik waliwatwanga risasi wazazi wao wakiwa kibarizani, kisha wakatengeneza mazingira yaonekane kama vile lilikuwa tukio la uvamizi.
Baada ya hapo waliondoka nyumbani wakiacha maiti za wazazi wao, wakaelekea kwenye sinema wakanunua tiketi ya kuangalia movie ili kutengeneza ushahidi kuwa hawakuwepo wakati wazazi wao wakiuawa.
Baada ya movie walikutana na marafiki wakazurura nao mpaka usiku wa manane ndipo waliporejea nyumbani kwao.
Lyle alipiga simu 911 akipiga kelele nankulia kuwa wazazi wao wameuwa.
Polisi walipofika waliwakuta wakiwa wanalia na kupiga kelele jambo lililowatia simanzi na hawakuwashuku kabisa kama wao ndiyo wauwaji.
Hata hawakupwa mikono wala nguo zao kipimo cha kuonyesha kama wana mabaki ya vumbi la risasi.
Na ajabu ni kwamba bunduki walizotumia kuwaua wazazi wao walikuwa bado wanazo kwenye gari lap lakini polisi hata hawakulipekua.
SIRI YAFICHUKA
Baada ya mauaji hayo vijana hao ndiyo walibaki kama warithi wa mali za wazazi wao, nao bila kuchelewa walianza kuzotumbua kwa kununua magari ya kifahari na vito vya thamani.
Yale majonzi waliyoyaonuesha siku ya tukio yalipotea ghafla wakaanza kula maisha.
Inasemekana ndani ya mwezi mmoja walikuwa wametumia kiasi cha dola 500,000-700,000.
Tabia yao ya kutumbua pesa iliawashtua polisi na kuwafanya waanze kuwachunguza.
Kwa upande mwingine Erik alisumbuliwa sana na tukio walilofanya yeye na kaka yake, akawa anatafuta mtu wa kumwambia, na ndipo akaamua amwambie rafiki yake aitwaye Craig.
Hakuishia hapo alimfuata mwanasaikolojia aitwaye Jerome na kukili juu ya mauaji hayo.
Lyle alipojua kuwa Erik kakili kwa mwanasaikolojia alimfuata Erik akamaambia waongozane kwa huyo mwanasaikolojia, na wote walikiri mbele yake ila Lyle akamtishia kuwa akisema tu atamuua.
Lakini kumbe muda huo alikuwepo kimada wa Jerome maeneo ya ofisini hivyo wakato yuko nje ya ofisi alisikia mazungumzo yao na akawarekodi.
Huo ushahidi alibaki nao wala hakuupeleka polisi mpaka baada ya miezi saba aliposikia kuwa wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuwaua wazazi wao ndipo naye akapeleka ushahidi.
Wote walifungwa vifungo vya maisha magereZa tofauti na toka kipindi hicho hawajahi kukutana zaidi ya kuandikiana barua.
Na wote wamefanikiwa kuoa wakiwa gerezani.