Lyrics za nyimbo za kiswahili

Lyrics za nyimbo za kiswahili

Kama wewe ulinipenda
Kwa nini kunidanganya bwana wee
Kujibandika madaraka siyo yako bwana wee we

Unadhurura mchana kutwa
Kupita kuranda randa mitaani
Kumbe hukuwa na uwezo kwa nini kunidanganya
Nikuelewe vipi?
Babu eee uaminifu wako uko wapi ?mamaaa

(Chorus)

Usinione bwege mamaaa.....Kalubandika eee
Kwa kukubali mwito wako Kalubandika ee
Hayo yote ni matatizo ya dunia mama aa

Akiingia kwenye baa kazi yake kuomba bia
Hana hata aibu sigara pia anaomba
Mitaani na kwenye masoko
Hujitangazia kuwa yeye ni kmkurugenzi wa kampuni fulani
Kumbe sio hivyooooo

Usinione bwege mamaaa.....Kalubandika eee
Kwa kukubali mwito wako Kalubandika ee
Hayo yote ni matatizo ya dunia mama aa

Nilitaka kujitumbukiza ndani ya moto ee mama
Kumbe bwana yule hana kitanda wala shuka
Pa kulala hana, analala kwenye stendi ya Basi!
Pa kulala hana, analala kwenye kituo cha uda Kalubandika yeyeee
Wacha vituko we bwana

Usinione bwege mamaaa.....Kalubandika eee.........

This is Kalubandika song right?!.....hahahahahaah! i was looking for this lyrics aisee thanks
 
gal frendi wa shemeji yangu mistari kama hii eti....

Tamu kama asali Ndefu kama mpini
Urefu nchi ishirini lazma uchoke ulimi
Wengi wanajiuliza unanipendea nini?
Hiyo ni siri yetu tu wewe na mimi
Hawajui pipi ya kijiti ndio inajenga shepu
Masugar daddy kila siku wanabugi stepu
Raha ya pipi ya kijiti kula bila maganda
Pata raha halisi usisikilize propaganda
Pipi nzuri inanukia hata siku moja hainuki
Ndio maana inafichwa haiachwi uchi
Pipi ya demu wangu mtu mwingine simpi
Ni hatari kama serikali kubinafsisha nchi

aaaaaah......unanisoma?

sijawahi kusikia huu wimbo..unless umeutunga TUU....

Ni zilipendwa?
 
Napiga mayowe, hehe
Naanza kulia, haha

Chenge, fungua njia, kitoto kaanza tambaa

Familia ya leo, nani atawaleaaa?
Watoto Wa leo, nani atawaleaa?

Chenge, fungua njia, kitoto kaanza tambaaa

atakayeniambia wimbo huu wa nani kutoka bendi gani nitaamini kweli old school
 
King Kiki mzee wa bakulutu.
 
Wanasema urudieee Kasongo
Wanasema urudiee Kasongo

Wanasema urudie, tumalizee mamboo,
Kwenu ku mujini, nyingi yolela oo.
Wako mama, eko analia sana Kasongo
Wako baba,eko analia sana Kasongo
Wanasema urudiee

Ehee mwenyewe ulienda,
Ehee, ukarudi na kiyungi
Ehee,kiyungi sio ya kwako
Ehee, ya baba o na mama

Heko bwana, muziki bila jasho
Wanasema urudie tumalize wote hoyee
Wako mama, eko analia sana Kasongo
Wako baba,eko analia sana Kasongo
Wanasema urudiee
 
Napiga mayowe, hehe
Naanza kulia, haha

Chenge, fungua njia, kitoto kaanza tambaa

Familia ya leo, nani atawaleaaa?
Watoto Wa leo, nani atawaleaa?

Chenge, fungua njia, kitoto kaanza tambaaa

atakayeniambia wimbo huu wa nani kutoka bendi gani nitaamini kweli old school

Marquiz
 
Iiiiba, umelibeba Pendo languu eeeh, kama mwana na mbelekooooo
Iiiiba, umelibeba pendo langu eeh, kama mwana na mbelekooo

Inamana kukwambia, mchana usiku silaliii, natafuta pesaaa
Inamaana kukwambia, mchana usiku silalii, natafuta peeesaaa

Ili tuishi vizuri, na kujenga familia boraa, yenye thamani na penzi
Ili tuishi vizuri, na kujenga familia boraaa, yenye thamani na penziiii

Inamana kukwambia, mchana usiku silaliii, natafuta pesaaa
Inamaana kukwambia, mchana usiku silalii, natafuta peeesaaa

Ibaa ooh Ibaa, imekuwaje Ibaa
Ibaa ooh Ibaa, nielezeeee
Ibaa ooh Ibaa, imekuwaje Ibaa
Ibaa ooh Ibaa, nielezee

Sikitiko la penzi lako, lanitia wasi wasi
Kipi kilichokuudhi oohh Iba ooh Iba
Sikitiko la penzi lako, lanitia wasi wasi
Kipi kilichokuudhi oohh Iba ooh Iba

Ninapozungumza, hutaki kusema nami Iba
Ninapozumgumza, wewe unanunanuna tu
....

Na huyu muimbaji gani na bendi gani?
 
Unanikumbusha mbali na bakulutu hizi!

Ni Hiba mazee na sio Iba
 
Unanikumbusha mbali na bakulutu hizi!

Ni Hiba mazee na sio Iba

Hapo najua kuna sehemu sehemu nitakuwa nimechapia, si unajua nyimbo hazina CD yenye booklet ya lyrics wala website ya fanbase, kwa hiyo unakumbuka ulivyosikia tu.

Halafu miaka kibao imepita.
 
Na huyu nani? Bendi gani?

Baba Anna eee

Ni lini utarudia nyumbani

Uje uwaone watoto wako

Uje uwaone baba na mama kwenu.......

(repeat)

[Lead]

Najua kazi nyingi zimekuzonga...

Huko uliko nako ni mbali sana baba Anna eeeee

Hata hivyo ufanye kila njia.....kwani kuna matatizo matatizo matatizo kwenu eeee

(Chorus)

[Wote]

Watoto wako wanakukumbuka...kila siku haweshi kukuuliza

Na mama naye ananung'unika....kwani miaka mingi imepita

Baba amekuwa mtu mzima...hawezi kuhangaika huku na kule

Kwa hiyo bwana ufanye haraka...matatizo yametuzidi mno yooooo

Fanya uje eeee

[Lead]

Leo nasema aaa......mimi naomba.....niko peke yangu.....

Maisha ya tabu.....kila kitu ni pesa.....chakula ni pesa....

Mavazi ni pesa.....ufanye haraka...bwana naomba eee

[Wote]Fanya uje eeee
 
Walah Kiranga hizi nyimbo zinanikumbusha enzi zile za radio tanzania mchana leo show.....enzi hizo watu wanasikiliza kutumia boom box....unatafuta idhaa huku unasikilizia na sikio....

Au upo unasubiria ugawaji...foleni ndefuuuuuuu hadi unafika unaambiwa sukari imekwisha...ukifika home ugali wa njano unakusubiria.
 
Iiiiba, umelibeba Pendo languu eeeh, kama mwana na mbelekooooo
Iiiiba, umelibeba pendo langu eeh, kama mwana na mbelekooo

Inamana kukwambia, mchana usiku silaliii, natafuta pesaaa
Inamaana kukwambia, mchana usiku silalii, natafuta peeesaaa

Ili tuishi vizuri, na kujenga familia boraa, yenye thamani na penzi
Ili tuishi vizuri, na kujenga familia boraaa, yenye thamani na penziiii

Inamana kukwambia, mchana usiku silaliii, natafuta pesaaa
Inamaana kukwambia, mchana usiku silalii, natafuta peeesaaa

Ibaa ooh Ibaa, imekuwaje Ibaa
Ibaa ooh Ibaa, nielezeeee
Ibaa ooh Ibaa, imekuwaje Ibaa
Ibaa ooh Ibaa, nielezee

Sikitiko la penzi lako, lanitia wasi wasi
Kipi kilichokuudhi oohh Iba ooh Iba
Sikitiko la penzi lako, lanitia wasi wasi
Kipi kilichokuudhi oohh Iba ooh Iba

Ninapozungumza, hutaki kusema nami Iba
Ninapozumgumza, wewe unanunanuna tu
....

Na huyu muimbaji gani na bendi gani?

Wimbo huu umepigwa DDC Mlimani Park ila sikumbuki mwimbaji.
 
We mkali.

Huo wa Baba Anna mmmhh, sina hakika kama nimewahi kuusikia au sijawahi kuusikia.

Baba Anna uliimbwa na Marijani Shaaban Marijan (Jabali la Muziki) wakati akiwa na Dar International, Super Bomboka.
 
Leo ni siku ambayo Father Nelly alifariki kwa kuchomwa kisu na hii ni miongoni mwa kazi zake za mwisho
Title:NINI DHAMBI KWA MWENYE DHIKI
Artist:The late FATHER NELLY-XPLASTAZ

All my people
East Africa
Tanzania, Uganda and Kenya
Dar es Salaam, A town
Wherever you are
Piga magoti, tuombe Mungu
Hii ni siasa, dini, vita, ubwana, utwana, au kiama ghalika, sodoma na gomora?
Simama imara, zunguka kila kona, kila anga angaza
Kushoto, kulia, mbele, nyuma kote pitia
Na hapo ulipojishikiza g'ang'ania, sikilizia, vumilia baadae usije jutia

Hii ni mahususi na maalum kwa watu wangu
Walemavu, vipofu, zeruzeru na wendawazimu
Watoto wa mitaani, fukara, masikini na wenye akili zao timamu

Hii kamba ngumu
Mjue tunavutana na wenye nguvu
Vitambi na mashavu
Hakuna tena fair game
Refarii kauzu
Uwanja wenyewe mkavu
Ujira mgumu, malipo finyu
Kilichobaki kucheza rafu
Tumechoshwa na ukabaila, ubepari na ubeberu
Wakati ndo huu
Ukombozi ndo huu
Na sasa naamuru mliopo chini wote mpate divai ya vinibu
Mtetezi wenu nikaze gidamu
Nimwage sumu ya upupu juu yao
Wajikune bila aibu
Kwanza saluti kwa waliyotangulia kuzimu
Pili tuombe Mungu
Baba yetu, utupe mkate wetu wa kila siku
Utujaze nguvu
Tupate kudumu ndani ya game
Tutakapofika kuzimu siku ya hukumu
Utupe nafasi tupate kutubu
Kwani tunajua tunatenda maovu
Tunakula haramu
Tunatumia kila mbinu
Juju, uhalifu, upanganyifu
Ili tuweze kujikimu
Lakini isiwe kisingizio kwa wanadamu wengine kunyimwa haki zetu
Kutuzibia riziki zetu
Kutuita makafiri, dharau na kutukashifu
Kwani nini dhambi

Chorus :
Nini dhambi kwa mwenye dhiki,
Kipi haram, kipi halali,
Kila mmoja anaitaka hii riziki
Kitendawili, vurugu mechi
Huwezi tabiri

Kwa nini ? Uliza swali, kama sote tungekuwa wasomi, matajiri
Ni nani angelifanya kazi za kutisha na hatari mfano ya mochwari

Kila mmoja wetu hapa mjini kaja kwa dili
Kila kitu, kila mahali
Na hata ngozi ya mtu dili
Wengine wachawi, waganga feki
Matapeli, wasafiri kafiri

Wakati wengine wapole kama walokole
Mchana pirika nyingi maofisini
Kumbe night kali, kahaba

Shuga, jambazi, mengine ya kusitiri
Ah!
Wapo waliopoteza maisha katika kufight life
Kumbukumbu zao zimebaki makaburini

Na wapo waliopoteza kabisa tumaini la kuwini
Hao roho zao utadhani wamezitoa rehani
Wakikutight mahali fulani
Inabidi uwakabidhi mshahara wote wa mwisho wa mwezi

(Chorus)

Kweli Bongo kutafuta braza
Utajajuta utakapojikuta huna hata bukta
Shauri yako we tegesha tu kama golikipa
Na hao unaowategemea mwishowe watakutosa
Huna elimu, huna fani
Lakini nguvu, ulimi, uchumi unao unaukalia
Kumbuka
Kupata au kukosa yote ni kawaida
Sometimes unalala unaota unakula
Unakunywa, unapiga denda
Na kula uroda na demu bomba
Ukikurupuka tu unakuta patupu
Hakuna kitu

***************
RIP FATHER NELLY
 
Last edited:
Back
Top Bottom