M/Kiti wa Simba: Barbara Gonzalez anatosha kabisa kwenye uongozi wa Klabu ya Simba

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Murtaza Magungu leo Julai 1, 2022 amesema kuwa CEO Barbara Gonzalez anatosha kabisa kuwa kiongozi wa juu katika Klabu hii kubwa hapa nchini Tanzania.

Mangungu amesema kuwa wale ambao wanaosema kuwa CEO Barbara hatoshi wao hawana maono ya kuona mangapi mazuri na makubwa ambayo ameyatekeleza kwenye Klabu chini ya uongozi wake.

"Barbara anatosha kabisa kuwa kiongozi wa juu ya uongozi wa Klabu ya Simba, na hata wanaosema kuna mambo yanaenda tofauti wala mimi sijaona hayo mapungufu yanayotajwa na hakuna anayetaja ni mapungufu gani". Amesema Mangungu.

Sports HQ
 
Huyu Mangungu naye haya Wala hayamtoki moyoni anajua.
 
BERNAD MORRISON SIO GAIDI 🙌


Acha inyeshe tuone panapovuja
 
Barbra anawanyoosha waswahili Simba SC, mpaka wale wahindi.
 
Mi naona dalili za Simba kuwa timu ya kawaida zinaonekana.
Huwezi kuendesha timu ya kibongo kizungu kizungu ukafanikiwa.Ni lazima utawakwaza wengi tu.

Wachezaji wetu wengi hawajakulia academy,wengi wahuni na wavuta bangi.Sasa ukileta mambo kama ya ulaya huwezi kukaaa na wachezaji wenye vipaji ambao wengi ndio hao kama akina Morrison,Mkude n.k

Lazima uwe flexible na tayari kuishi kwa kuvumilia madhaifu ya wengine.

Huyu mwenekiti na CEO wake hawafai kabisa kwa sababu wanataka Simba iwe kama DTB
 
Huko kwenye vilabu vyote alivyoacha alama ya nidhamu mbovu vilikuwa vinaendeshwa kizungu?

Acha ujinga walau kidogo kutetea vitu vya hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…