Hii kampuni ya M-kopa ilikuwa inafanya kazi hapa Tanzania mwaka 2015 to 2018 makao makuu yake ni Nchini Kenya.
Wao walikuwa wanakopesha Solar kwa watu wa vijijini kwa mkopo nafuu tu. Ambapo ilikuwa unalipia kidogo kidogo mpaka unamaliza mkopo wako.Ila baadae waliacha kufanya hizo shughuli za kukopesha hizo Solar na kubaki tu na shughuli ya kuhudumia wateja waliokuwa wamekopa yaani kutengeneza na kubadilisha vifaa vya Solar kwa wateja waliokuwa wamekopa.
Hivyo, hicho ulichofanyiwa umetapeliwa kwa sababu M-kopa hawajihusishi tena na huo ukopeshaji.