M-wekeza kutoka Vodacom Riba 13%

Miradi ya wastaafu
Kwa wastaafu ni miradi mizuri. Kwa sisi wasaka tonge naona ni nzuri kwa ajili ya kuweka pesa kwa muda wakati unafuatilia michongo ya maana ya kufanya. Mfano umebumba ukapiga kama 7M sehemu badala ya kuziweka ndani au benki ambapo watazitafuna kwenye monthly maintenance fee na mambo mengine pia waje kukukamua wakati wa kuzitoa mimi naona ni bora uzitupie kwenye hizi account za uwekezaji lengo sio upate faida ila kipindi unajikusanya na kutafuta issue ya kufanya kwa mtaji huo ulioupata ni bora pesa ikae huku kwasababu itakuwa kuna viji percent vinaongezeka vutasaidia wakati wa kuitoa pesa isiwe imekatwa utaipata ikiwa kamili unafanyia mitikasi yako. Ila kwa swala la kupata faida tuwaaachie kina Mo
 
Wakuu mbona menu ya m wekeza haipo mpesa App??
 
Kutoa 10,000 unakatwa sh ngapi kwa wakala? Ni zaidi ya hiyo 13%
 
K
Kweli mkuu ukiwa na bilion kwa mwezi hukosi zaidi ya milion 13
 
Mkuu upo vizuri hongera. Asee app yangu naona ile icon ya m wekeza imeondoka nimeitafuta sana haipo hadi nitumie ussd
Mkuu hii ukijikusanya ukawa unavuta mil 1 per month kama faida, uzeeni hauwezi kuwa na stress ya maisha kivile
 
Mkuu hii ukijikusanya ukawa unavuta mil 1 per month kama faida, uzeeni hauwezi kuwa na stress ya maisha kivile
Kikubwa iwe na ukweli tuu maana wasije wakatupeleka halafu wakasepa na vijisenti vyetu baadae huko japo naona wapo serious
 
Hii bado sijaielewa wao wanapataje faida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…