M23 wasema hawaondoki Goma waapa kuendelea kusonga mbele kuelekea mji mkuu Kinshasa

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Kundi la waasi wa M23 Alhamisi limeapa kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, huku wapiganaji wake wakisonga mbele zaidi katika eneo la mashariki mwa nchi lenye utajiri wa madini.

Kundi hilo kuchukua udhibithi wa sehemu kubwa ya Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, ni ishara ya kuongezeka kwa mzozo mbaya katika eneo ambalo limekumbwa na miongo kadhaa ya mizozo inayohusisha makundi mengi yenye silaha.

Rwanda inasema nia yake ya msingi ni kutokomeza wapiganaji wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, lakini inatuhumiwa kujinufaisha na akiba ya madini ya eneo hilo yanayotumiwa katika soko la vifaa vya kielektroniki duniani.

“Tutaendelea kusonga mbele katika vita vya ukombozi hadi Kinshasa,” Corneille Nangaa, kiongozi wa muungano wa makundi ya waasi ikiwemo M23, aliwaambia waandishi wa habari mjini Goma.
“Tupo Goma, hatutaondoka wakati wote masuali yaliyosababisha tuchukuwe silaha yatakuwa hayajapatiwa jawabu,” alisema.

Nangaa alisema M23 itarejesha umeme na usalama mjini Goma katika siku zijazo na kuweka njia salama kusaidia watu waliotoroka makazi yao kurejea nyumbani.

Chanzo: VOA
 
Ok ..kumbe Cornele Nangaa yuko ktk hili? Hahahaha basi Kuna jambo ,Felix achukue Hatua Kali haraka sana...
 
Sipo hapa kubishana na Watoto wadogo km wewe...ila tushajua nyuma ya Cornelle Nangaa yuko nani na inatakiwa nn, uzuri kajitokeza
Bora Mimi mtoto ila wewe ni kubwa jinga umekua umri na mwili tu kichwani empty eti tushajua inatakiwa nini yaani we kikaragosi ndio ujue kinatakiwa nini congo ukiwa hapa jamii forum
 
Rwanda imeweka wanajeshi wake laki moja mpakan na congo I jiandae kwa hali yoyote
 
Back
Top Bottom