MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,893
Jana huko Kivu zimevuka habari kwamba mamluki wa bwana Eric Prince wamefanyiwa shambulio zito na vikosi vya M23. Hawa mamluki siyo tu watu wa kawaida ni wale makomandoo kutoka vikosi kama SAS, Green-Beret na Navy-Seals. Wana mafunzo makali na teknolojia ya kisasa.
Jana imetoka taarifa wamepewa kipigo na mgambo wa M23, hadi mpiganaji bwana Tim Kennedy aliyewahi kuwa bondia wa UFC na komando wa Marekani kapata majeraha makubwa na kukimbizwa kwao. Sasa amekufa au yuko hai, sifahamu.
Ila taarifa zinasema kwamba M23 walitumia mbinu na teknolojia za juu kabisa kufuata ndege isiyokuwa na rubani hadi kwenye kambi ya mamluki hao na kufanya shambulio kubwa. Wanasema uwezo huo unadhihirisha kabisa kwamba M23 walisaidia na Rwanda ambaye kwasasa taarifa zinasema ndiyo mwenye jeshi imara ukanda huu.
Ndani ya miaka miwili, Rwanda na M23 wamefanikiwa kutoa kila askari aliyekuwa anaingia kupambana kwa niaba ya serikali ya Kongo. Mwaka jana Tanzania, South-Africa na mamluki wa Kigebelgiji waliondolewa Kongo baada ya kuzidiwa na M23. Mwaka 2026, mamluki wa Kimarekani wameondolwa na M23 ikisaidiwa na Rwanda.
Sasa wale wataalamu na wadau kutoka jeshi la sita kwa ubora duniani, wanasema Mgomba Mrefu hana uwezo kama wao. Ilhali tunaona Mgomba mrefu anawafurumusha hadi hawa wazungu wa Marekani. Huwa nawaza sana pale napofikiria kwamba jeshi la sita kwa ubora duniani linaongozwa na mtu mwenye uwezo mdogo mno kiakili, yaani uwezo wake wa kiakili ni finyu sana.
ENIWEI Tanganyika hoyeeee
Soma hapa: https://nypost.com/2026/10/09/world...ies-in-congo-ex-ufc-fighter-wounded-sources/a