Marie Antoinette
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 426
- 412
Msemaji mkuu wa M23, Lawrence kanyuka, ametangaza kukamatwa kwa watu 5, 3 wakiwa wanajeshi wa FARDC(jeshi la Congo) na 2 wengine wakiwa wanamgambo wa FDLR. Watu hawa walikamatwa na bunduki 4 na mambomu ya kurushwa kwa mkono. Katika kuhojiwa, walisema walikuwa katika kambi ya MONUSCO mjini humo, na kwamba wameachiwa kwa lengo la kuvuruga amani mjini humo.
Amesema kwamba, watu hao ndo walioeleza azimio lao na idadi ya walioachiwa huru, huku akitangaza kwamba msako mkali mjini unafanyika kuhakikisha wanakamatwa.
Awali, M23 iliongeza wanajeshi wapatao 500 mjini Goma, lengo likiwa ni kuimalisha usalama na kuhakikisha wanajeshi na wanamigambo waliojificha mjini humo wanakamatwa, pamoja na wafungwa waliotoroka gereza la Goma.