M23 yaua wanajeshi 3 wa Tanzania huko Goma DRC

Inaonekana vita ya Congo ni kwa sababu ya misinformation kama hizi, matatizo mengi Africa ni ujinga kama huu
Huo ndo ukweli...kila siku M7 anasema jinsi Nyerere alivyowasaidia,watu ambao kidogo washaongea na ndugu wa karibu wa Nyerere wanasema wao ni watusi
 

Kwahiyo hapo Watanzania wanakuwa hawajauawa au
 
Aidha wewe ni mbumbumbu hujui unachokiongea, au unafanya makusudi kujifanya hujui. M23 inatokea kwenye kundi la wa Congo ambao wanaongea Kinyarwanda. Wanapatikana kwenye maeneo ya Kivu kaskazini na Kusini kwa zaidi ya miaka 400 sasa. Haya maeneo wanayoishi kabla ya mkutano wa Berlin ulioigawa Afrika yalikuwa ni sehem ya Kingdom ya Rwanda chini ya mfalme wa Rwanda (King Rwabugiri)huyu ndie alikuwa anatawala Kingdom ya Rwanda wakati huo 1845-1896 wakati wa ujio wa wakoloni, Himaya yake ilikuwa ni kubwa sana kwenye maeneo haya ya maziwa makuu. Eneo lote la Rwanda leo, eneo lote la kusini mwa Uganda(Kabale) mpaka Lake Edward, Eneo lote la Kivu kusini na Kaskazini, hapa pote waliishi Raia wake wakiongea Kinyarwanda. Ikumbukwe wakati huo hapakuwa na Congo wala Tanzania au Uganda, palikuwa na chiefdom ndogondogo tu, Lakini Rwanda ilikuwepo ikiwa ni Kingdom kubwa tu mara kibao ya Rwanda ya Leo. Wakoloni hasa hasa Wajerumani, Wabelgiji na Waingereza Waliikatakata hii Kingdom na kuifanya iwe ilivyo leo. Walikubaliana ku share mirima ya Volcano kwani walijua kwenye hiyo milima kuna Utajiri mwingi sana wa madini ya chuma. so kila mmoja alisqueez Kingdom ya Rwanda mpaka kwenye hii milima. Muingereza akapush upande wa Kaskazi na Mbelgiji akapush upande wa magharibi. Hii Milima amabayo inapatikana kaskazini mwa Rwanda maeneo ya Ruhengeri,Gisenyi,Goma/Rutshuru na Kikunguri Upande w Uganda Kabla ya Wakoloni ilikuwa inapatikana katikati mwa Kingdom ya Rwanda Mfalme Rwabugiri alikuwa akiitumia kama observation point yake. So haya maeneo yalipokatwa Raia waliokuwa ndani ya hii mipaka hawakuwa Wanyarwanda tena japo lugha yao ilibaki Kinywanda. Waliokatiwa uganda wakawa waganda, waliokatiwa Congo wakawa wa Congo. Sasa Viongozi wasiokuwa na sera ndio wanawatumia kisiasa kuleta machafuko ili waendeleze utawala wao. Lakini kwa kweli hawa watu kamwe hawawezi kuwa Wanyarwanda unles kama Mwalimu Nyerere alivyosema ukiwafukuza wafukuze na Ardhi yao, Sio uwafukuze halafu ubaki na ardhi yao. Kwa bahati mbaya sasa hiyo Ardhi yao is very rich in minerals and fertility.
 
Ombi langu Kwa Askari wetu Shupavu kama mbinu hii ya Vita Haiwezekani!
👇👇
A scorched earth tactic, or a scorched earth policy, is a military strategy that has been used throughout history. If a nation, region, or army is under threat, one way that the military can hurt their enemies is by destroying anything that enemy forces could possibly use as a resource.

RUDINI WANANGU!
HERI YA KICHEKO KULIKO KILIO!
 
Kitu ambacho mi sielewi inawezekana vipi jeshi la DRC, South Africa na TPDF combined tunashindwa kuwadefeat hawa m23 mtu anieleweshe vizuri mana jeshi letu limekaa zaidi ya nusu mwaka huko
 

Naomba nijibu a very simple question M23 unauhusiano wowote na RDF au vipi?
 
Kitu ambacho mi sielewi inawezekana vipi jeshi la DRC, South Africa na TPDF combined tunashindwa kuwadefeat hawa m23 mtu anieleweshe vizuri mana jeshi letu limekaa zaidi ya nusu mwaka huko
Hili swali huwwzi kujibiwa zaidi utaanza kutukanwa na kuitwa mtusi.

Kwa mtu mwenye akili sawasawa utaona kuwa vikosi vya sadc,jeshi la serikali pamoja na makundi yote yanayoiunga mkono serikali wamewashindwa m23 inayo ongozwa na RDF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…