kwa maoni yangu, mtu anayefaa kusuluhisha mgogoro fulani ni lazima awe na aina ya uzoefu/haiba wa kuwashawashi wale anaowasuluhisha kwamba anaweweza kusuruhisha mgogoro huo.
mfano Marehemu Mwalimu JKN alikuwa anafaa moja kwa moja kusuluhisha mgogoro wa burundi kwa sababu ya haiba yake na uzoefu wake katika migogoro ya rhodesia, msumbiji,uganda n.k na pia alivyoirithi kazi ile Mzee mandela baada ya kifo cha Mwalimu ni dhahiri mtu mwingine mwenye haiba na uzoefu alikuwa amepewa kazi muafaka.
Nikija kwa watu kama BWM, ambaye anashutumiwa chini ya utawala wake kuona vote rigging zikitokea huko zenji lakini hakufanya kitu, hii inaondoa credibility yake kuwa msuluhishi MAKINI WA wa mgogoro wa Kenya, lakini pia, BWM angeweza kupewa benefit of doubt kama asingekuwa katika tuhuma hizi za utumiaji ofisi ya wananchi kujinufaisha, kwa sababu usuluhishi wakati mwingine unategemea "how morally strong you are to tell others that this is wrong". Je BWM ana moral authority ya kuwaambia Raila na Kibaki kwamba hiki na kile ni kibaya kwa hivyo wasikifanye?. akiwaambia hivyo si watamcheka kwa kujisemea kimoyomoyo kwamba mzee mbona na wewe una boriti katika jicho lako?
Kwa mtu kama Museveni huyu naye anashutumiwa vikali kwa kumtendea vibaya Besigye, yaani kutumia mabavu kumbana mpinzani wake. sasa kweli Raila atamwamini mtu kama huyu waketi pamoja ilhali ni watu wa aina ile ile ya kibaki?.je Museveni ana haiba ya kutosha kuweka uzito katika usuluhishi?.
kwa maoni yangu mtu kama koffi anaan, Salim ahmed Salim, Jimmy carter na joachim Chissano hao ni watu ambao wanaweza kuusuluhisha mgogoro huo, Nimemuweka Jimmy Carter ili kuongeza uzito wa usuluhishi kwa sababu atawakilisha mataifa ya magharibi ambayo yana influence kubwa katika mambo ya afrika ,pia kutokana na historia ya mafanikio yake ya kihistoria ya ule mkataba wa amani kati ya misri na israel ni sababu ya yeye kuwemo katika wasuluhishi wa mgogoro wa kenya