Ma cashier wa mwendo kasi wana ujanja wa kuuza ticket za mwanafunzi kwa watu wazima kisha kinachozidi 450 ni chao.

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari za jioni

Kwenye mwendokasi dar ma cashier wajanja sana.

Nauli ya mwanafunzi ni 200

Nauli ya mtu mzima ni 650.

Hizi tiket za mwanafunzi na mtu mzima zinafanana kila kitu tofauti ni maandishi ya bei tu.

Ma cashier huwa wana tabia ya kuprint tiket nyingi wakiwa wenyewe.. kisha wateja wakija wanapokea hela na kuwapa tiket tu fasta.

Ma cashier hawa wanajua wa Tanzania hatuna tabia ya kusoma tiketi imeandikwa nini. Hapo ndipo wanapata mwanya.

Mtu mzima unatoa 650 yeye anakupa tiketi ya 200. Kisha 450 inakuwa yake kwenye hesabu.

Kwa siku akiwauzia watu 100 tu anaondoka zake na cha juu 45000 kwa ulaini..

Na hao 100 ni wachache sana maana mwendo kasi kwa siku inahudumia maelfu kama sio malaki ya watu.

Jana nimesoma tiketi nikakuta nimeuziwa ya 200 asubuhi.. na jioni ya leo tena kituo kingine napo nikauziwa ya 200 tena.

Nikawaza siku ambazo sikusoma tiketi plus abiria wenzangu kibao nao hawasomi tiketi jinsi wanavyopigwa
 
Mimi kama mwananchi niliye nje ya system ya upigaji ya wakubwa nipo kwenye level ya kuto-mind mambo ya watu nimeshajitengenezea kanuni ya kutom-snitch mtu kama matendo yake hayaniathiri moja kwa moja.

Mleta mada baada ya kupewa ticket ya Tsh 200/= si ulisafiri bila bugdha yoyote?kama ndiyo basi huo ndiyo mwisho wa kamba zao wasilaumiwe.
 
Ukikaa sehemu kama izo usipo kuwa milionea basi unatakiwa kuchapwa fimbo kabisa...mkuu acha wafaidi keki ya taifa na wao.
 
Jamani tuseme ukweli,maisha haya ya ajira za kibongo Kama hauna side job unadhalilika Sana..

Ndugu mwandishi nikuambie tu,hakuna watu wenye maisha magumu Kama wakata tiketi na madereva mwendokasi,wale jamaa hawanaga mishahara ya maana alafu mbaya zaidi kwa dereva yeye anakusanya abiria tu kwenye like Safina Kama alivyoagizwa na kuwapeleka destination aliyopangiwa na hapati hata buku Kama posho .. zile suti zisikutishe...
 
Kweli kbs mkuu..Alafu Wale watu wanatia huruma sn,Kama wanajilipa posho kidizaini hiyo wacha tu wajilipe kwa kweli..

Mleta mada ana hoja nzuri ila imekaa kiukuda
 
Bongo nimewavulia kofia kwa unafki.

Baadhi ya Watu wakila kwa urefu wa kamba zao watanangwa kila kona ya dunia, ila Wanangaji hao hao watabadilika ghafla kama kinyonga kuhalalisha Watu wengine wapige cha juu kama kwenye hii mada.

Wabongo hatuingiii mbinguni ng'oo labda kwa macho kodo... [emoji102]
 
Ndugu yangu apo binafsi sijaona kosa lao waache na wao wajipatie karidhiki japo kuwa haiwezi kukuathiri sio inshu
 
Si unakuwa umefika au hufiki?
 
Hiyo ndiyo slogan
 
kwa makeshia ni sawa kujilipa kwa dizaini iyo,ila kwa madereva wanalipwa mshahara mwisho wa mwezi na posho kwa day wanalipwa pia,
 
Unataka na hili wakalitazame?

Waache wale kwa urefu wa kamba zao.
 
usimamizi wa serikali ni mbovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…