Habari za jioni
Kwenye mwendokasi dar ma cashier wajanja sana.
Nauli ya mwanafunzi ni 200
Nauli ya mtu mzima ni 650.
Hizi tiket za mwanafunzi na mtu mzima zinafanana kila kitu tofauti ni maandishi ya bei tu.
Ma cashier huwa wana tabia ya kuprint tiket nyingi wakiwa wenyewe.. kisha wateja wakija wanapokea hela na kuwapa tiket tu fasta.
Ma cashier hawa wanajua wa Tanzania hatuna tabia ya kusoma tiketi imeandikwa nini. Hapo ndipo wanapata mwanya.
Mtu mzima unatoa 650 yeye anakupa tiketi ya 200. Kisha 450 inakuwa yake kwenye hesabu.
Kwa siku akiwauzia watu 100 tu anaondoka zake na cha juu 45000 kwa ulaini..
Na hao 100 ni wachache sana maana mwendo kasi kwa siku inahudumia maelfu kama sio malaki ya watu.
Jana nimesoma tiketi nikakuta nimeuziwa ya 200 asubuhi.. na jioni ya leo tena kituo kingine napo nikauziwa ya 200 tena.
Nikawaza siku ambazo sikusoma tiketi plus abiria wenzangu kibao nao hawasomi tiketi jinsi wanavyopigwa