Ma-doctor naombeni ushauri korodani yangu ambayo niliifanyia operesheni 2010 imevimba tena...tatizo ni nini?.

Ma-doctor naombeni ushauri korodani yangu ambayo niliifanyia operesheni 2010 imevimba tena...tatizo ni nini?.

Joined
Dec 7, 2017
Posts
41
Reaction score
27
Ma-daktari na waelevu mliojaa humu JF naomba mnisaidie coz nina tatizo, mnamo mwaka 2010 niliwahi kufanya operesheni ya korodani yangu ya upande wa kushoto baada ya kugundua kuwa imeanza kuvimba . Nilikwenda hospitali nikafanya checkup wakagundua kuwa imeanza kujaa maji hivyo madaktari wakanishauri tufanye operesheni kuondoa hayo maji nami nitakuwa sawa baada ya kupona.

Ni kweli nilifanya operesheni na nilipona vizuri kabisa na maisha kuendelea, lakini mwaka jana 2017 nilianza kuona mabadiliko tena ktk korodani zangu haswa upande ule wa kushoto ambapo ndipo nilifanya operesheni korodani ilianza kuvimba lakini haiumi kabisa nikaenda hospitali nikakutana na dokta na kumuelezea tatizo langu akaniandikia nikafanye ultrasound ili nimrudishie majibu, nilipomletea majibu akaniambia kuwa mishipa tu imevimba wala hakuna maji ila hii korodani ya upande wa kulia ndio imeonekana ina maji kidogo sana hivyo akaniandikia sindano za power safe tano akaniambia nikimaliza kuchoma hizo sindano hilo tatizo litakuwa limeisha.

Sasa nimeshamaliza kuchoma sindano hizo tano na nilikuwa nachomwa ktk mishipa lakini naona uvimbe umepungua kiasi ingawa haujaisha kabisa, na nimesafiri ningerudi kwa yule dokta kumuomba ushauri na huku nilipo sitarajii kurudi miezi ya hivi karibuni. Sasa nimekuja kwenu ndugu zangu, wataalam wa afya, madaktari, waelevu, watu wazima ambao labda mliwahi kukutwa na tatizo kama hili langu je ni nini nifanye ili niondokane na tatizo hili? ingawa kwa sasa uvimbe umepungua kiasi chake!. Naombeni ushauri nini cha kufanya...Ahsanteni.
 
Pole Sana Kwa Matatizo
Fanya Mpango Urudi Kwa Dokta Kumbuka Umeanzishiwa Dose Na Umemaliza Sasa Hapo Ulipo Unangoja Matokeo
Hapa Ushauri Utapata Japo Hospital Ndiyo Ufumbuzi
 
Kuwa na subira kama wiki tatu maana ili uoni matokeo lazima upate muda wa kujitazamia ok sio chumvi hiyo
 
Pole sana mkuu, wanaume wengi huwa tunapata hilo tatizo la hydro cell
 
Back
Top Bottom