Ma HOUSE GIRL

Ma HOUSE GIRL

Elia

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Posts
3,425
Reaction score
568
Napenda kujiunga na watu wote katika siku hii ya wanawake, pamoja na kuwapa hongera akina mama wote. Kubwa kwa leo napenda kuwapa pongezi Ma HOUSE GIRL wote popote walipo, kazizao naziheshimu saana. Nilipokuwa ndogo, Nakumbuka mama yangu alifuata msichana wa kazi kijijini akamleta na kumtambulisha kwetu kama mama yetu mdogo,( yaani mdogo wake). Huyo ndio aliye tupikia,tufulia,tuogesha, na kutufundisha kuoga, kufua, kuvaa nguo, na mambo mengine mengi . alinipeleka shule na kunifuata mchana, alinisaidia kuvuka barabara, kunibeba, alinifundisha ukakamavu pale wazazi wangu walipokuwa hawapo kwani sikuweza kudeka mbele yake ilifika mahali wazazi niliweza wagomea(kudeka) ila yeye namtii kwani alijua aniambie nini ili nisisumbue Hakika hawa akina dada kama tunavyowaita siku hizi wanastahili pongezi. Naomba mnifikishie salamu zangu kwao huko majumbani mwenu, Hebu tuwafagilie kidogo hawa wandugu kwa leo... nawasilisha
 
wanafanya yote hayo na bado wanalazwa jikoni kama paka:rain:
 
Namjali sana Hg wangu kwa mfano sasa hivi wife hayupo ananisaidia sana.
 
Big Up ndugu Elia kwa hii post! Ni kweli kabisa wadada hawa wanahitaji kupongezwa na kuthaminiwa kama binadamu yeyote yule. Siwaelewi wale wanaowanyanyasa hawa wasichana??!!!. Binadamu wote ni sawa na kila mtu anahitaji kuheshimiwa na kuthaminiwa. Thamani ya mtu haitokani na elimu yake, wala kazi yake!
Mbarikiwe
 
kwa kweli nawapa pongezi za dhati kabisa asa wangu niliyenae nikiwalaani wale wote wanaowarubuni na kuwaaribia maisha yao kwakweli nampongeza wa kwangu nafikiria chakumpa kama shukrani
 
Na kweli tena cku hz wanasaidia kweli na nyie kina mama mnavyojisahau wanachukua majukumu yenu yote. Kina mama m take care kwa hawa ma housegarl
 
Kweli hawa watu ni muhimu sana ila wapo baadhi ya watu hawawapi treatment nzuri kwa mfano kweli unamlipa TSHS 10,000/=?,wamwisho kulala wa kwanza kuamka Mungu atusaidie
 
Kweli Elia...you are very considerate...hawa ndo wanaolea watoto na familia zetu....wanawake wengi sasa tumebaki status tu,majukumu mengi yanafanywa na ma housegals.....Big Up Yourself!!
 
wanafanya yote hayo na bado wanalazwa jikoni kama paka:rain:

Sheria. Lazima wafanyakazi wa majumbani waweze kulipwa kutokana na kazi wanazozifanya, hii ni sawa na utumwa haiwezekani waonewe kiasi hiki na hakuna sheria ambazo zinawalinda. Ni aibu kubwa kwa taifa katika karne hii kuona kuna watu ambao wanawatumia wenzao kama watumwa.
 
Kweli Elia...you are very considerate...hawa ndo wanaolea watoto na familia zetu....wanawake wengi sasa tumebaki status tu,majukumu mengi yanafanywa na ma housegals.....Big Up Yourself!!

Umeona eeeh
 
:A S 13:.Angalia tu asije akafanya mpaka zile huduma za mke wako kwako....:rain:
Keren tukisema ukweli vijana wengi wanaokulia mijini mwanamke wa kwanza kujamiiana nao ni mahasigeli wa nyumbani kwao na mimi nikiwa mmoja wapo,wana kazi nyingi sana hawa viumbe.
 
Kweli kabisa kuna wakati nikiwatazama huruma hujaa moyoni mwangu wana kazi kubwa na ni watu wa kuwaheshimu sana tuwe tunafikiria hata kuwaendeleza watoke hapo walipo na kuwa watu wengine kwenye jamii.
 
Keren tukisema ukweli vijana wengi wanaokulia mijini mwanamke wa kwanza kujamiiana nao ni mahasigeli wa nyumbani kwao na mimi nikiwa mmoja wapo,wana kazi nyingi sana hawa viumbe.

Khaaa jamani wewe uporoto??!!!, ilitakiwa umuoe huyo binti.....:rain::rain:
 
Back
Top Bottom