Elia
JF-Expert Member
- Dec 30, 2009
- 3,425
- 568
Napenda kujiunga na watu wote katika siku hii ya wanawake, pamoja na kuwapa hongera akina mama wote. Kubwa kwa leo napenda kuwapa pongezi Ma HOUSE GIRL wote popote walipo, kazizao naziheshimu saana. Nilipokuwa ndogo, Nakumbuka mama yangu alifuata msichana wa kazi kijijini akamleta na kumtambulisha kwetu kama mama yetu mdogo,( yaani mdogo wake). Huyo ndio aliye tupikia,tufulia,tuogesha, na kutufundisha kuoga, kufua, kuvaa nguo, na mambo mengine mengi . alinipeleka shule na kunifuata mchana, alinisaidia kuvuka barabara, kunibeba, alinifundisha ukakamavu pale wazazi wangu walipokuwa hawapo kwani sikuweza kudeka mbele yake ilifika mahali wazazi niliweza wagomea(kudeka) ila yeye namtii kwani alijua aniambie nini ili nisisumbue Hakika hawa akina dada kama tunavyowaita siku hizi wanastahili pongezi. Naomba mnifikishie salamu zangu kwao huko majumbani mwenu, Hebu tuwafagilie kidogo hawa wandugu kwa leo... nawasilisha