Wakuu mlionitangulia hapo juu heshima zenu.
Naomba nichangie na mimi kwa mtazamo wangu .
1. Naungana na hoja kwamba Kazi kwa tanzania ni chache ukilinganisha na zalisho la vyuo vyetu kila mwaka hii kwangu haina mjadala.
2. Pamoja na hilo Napenda kurudisha lawama kwa Wa-TZ wenzangu kwamba hatuna sifa , nikisema hatuna sifa nina maana kubwa mbili tu
- Ya kwanza hatujui kutuma na kuandika ipasavyo barua na docs zinazohitajika ktk michakato ya kuombea kazi hili hakuna mtu analoliona kama ni Tatizo lakini kwanu mimi naona na nakumbana nalo sana .
Mfano : Umetangaza mtu alete Resume anakuletea CV , unamuambia alete trancript anatuma cheti , alete recommendation letters anakuorodheshea referees , jamani hili ni tatizo haswa kwenye mashirika ya Kimataifa .
- Pili WA-TZ kama kawaida yetu hatujiamini kabisa wakati wa Interview zenyewe kwahiyo chance za kukosa ni kubwa sana , na pia hatujui kujibu maswali ya interview inavyotakiwa .
Ikumbukwe mambo niliyoyataja hapo juu hakuna chuo kinachofundisha , me mwenyewe pia nilivyotoka chuo nilipata taabu kwelikweli lakini nilijifundisha mwenyewe kwa msaada wa technolojjia na pia nilipata jamaa mmoja wa Huko duniani(ulaya) ndio akanipa darasa la michakato ya kuomba,kujiandaa na kufanya interview namshukuru sana kwani najiona niko tofauti sana na nashukuru nimepata kazi na nikiomba huwa naitwa mara nyingi .
MImi ni HR , kwahiyo najua matatizo ya kazi na sisi vijana yanayotupata , najua tuna kazi sana .
@Pawaga usikate tamaa jaribu kuangalia upya applications zako na je zinaendana na hadhi ya kisasa inavyohitajika .
nashkuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia wakuu wote