Ma-jobless thread

Point,
 
Huyu ni mm kabisa sema umeruka e fm akina jemedari na kuwapondea yanga
 
Baada ya kuflashiwa kwenye ajira na kukosa pa kwenda nilianzisha utaratibu wa kutembelea kwenye masoko


Nilikua naenda kwenye soko husika natafuta sehem nakaa na km kuna story najumuika nazo kinomanoma


Ktk kuzurura nikaangukia kwenye soko la karume, baada ya kushinda nao nikagundua wanakopa kila kitu kuanzia chai au supu asubuh,msos wa mchana hadi maji ya kunywa


Nikaona nijiongeze kwa kununua katon tano za maji na kuzikalia km kigoda


Washkaj wakawa wanaulizia km nauza na huo ndio ukawa mwanzo wa kuwa msambazaj wao wa maj


Baada ya wiki kadhaa nikawa nasambaza hadi katon mia kwa siku na jion napitia mauzo


Km huna ajira usilale ndan jichanganye mtaan huwez kosa la kufanya
 
Sio kweli stori haina uhalisia
 
Sio kweli stori haina uhalisia
Swala la wew kuamin au kutokuamin hayo ni matatizo yako,lkn unapokua jobless usilale ndan zurura tu kwenye vijiwe vya kazi au masokon baada ya muda utapata tu la kufanya na kukuingizia kipato walau kidogo kikubwa usiwe na mbwembwe kwa kujiona una degree huwez uza mifuko au maji
 
Basically kwenye nguo na decorations. Nitakuelekeza Kona zote. Ila ni ngumu kupiga winga kwenye hardware. Ila ni rahis kwenye nguo kama unataka nikuelekeze Kona Kona hapa useme tu. Mana mm hiyo kazi jmos napataga mpaka 40k
Kaka naomba contact na wewe
 
Naelewa wadau mnachopitia. Msife moyo! Ila ukiwa jobless jichanganye, usikae nyumbani.

Kuwa jobless ni mzigo sana. Ila kuwa jobless huku sehemu unayoishi wakijua kuwa una kazi, ni ngumu zaidi. Unateseka kimwili na kisaikolojia. Nilishawahi pitia hili. Nitawapa kisa hiki changu siku moja.
 
Ideas ni nyingi ila tunaanzia wapi sasa kuzieleza
 
Usiruhusu nafsi ya kukata tamaa ikushinde.

Mimi kuna mdogo wangu mwaka wa nne huu tumempambania kazi lakini mambo hayatiki. Vihamsini laki vya nauli kwenda kufanya interview unavitoa hadi unahisi kutupa hela. Basi ikabidi njia ya kujiajiri ifuate napo kuna masongombingo yakatokea, maana kuanzisha biashara si rahisi. Basi jana usiku kanipigia Mungu kamuona. Kapata 'mchongo wa kudumu' sehemu. Wakati kazi hiyo alifanya usaili toka mwaka jana, na tulishaikatia tamaa.

Usingizi ulinikata kwa furaha. Mungu ana wakati kwa kila mtu. Kamwe usikate tamaa kwa hali unayopitia. Chuma lazima kiunguzwe ili kitengenezwe chombo.
 
Majira kama haya mwakani,Mungu atakuwa ametenda kwa wote
Amini na upokee Baraka za Bwana

Bwana akampe kila mmoja haja ya moyo wake.

Kikubwa application za kusaza
Imani bila matendo imekufa.
Ili kazi ipatikane ni lazima interview zifanyike,na ili interview zifanyike ni lazima application zitumwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…