maada mtoto hapati usingizi kama awali

Norshad

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2013
Posts
5,211
Reaction score
12,538
habari za mchana

niende moja kwa moja kama nilivyoeleza hapo juu,

leo ni siku ya tatu kijana wangu hapati usingizi na amekuwa mlizi tofauti na siku za nyuma, huku mtoto ni wa kiume na sasa ana miezi 6 na siku kumi na tisa, leo ni siku ya tatu huyu mtoto mfano akiamka asubuhi saa kumi na moja anaweza asilale tena hadi saa tano za usiku na ikitokea kalala hamalizi dakika tano kaamka na akiamka anakuwa analia sio kile kilio za watoto wachanga ni kilio kama cha kudeka hivi, sasa ninaomba anayefahamu tiba ya hili tatizo anisaidie ufumbuzi maana sasa mama yake anakonda kila kukicha ananyonya muda wote, yaani nusu saa anataka kunyonya akimaliza ukimuweka chini usiondoke ukae nae ukiinuka tu kilio anyonya tena, ni hivyo siku nzima....pia kuna harufu nilikuwa naisikia katika kinywa chake kwa zaidi ya siku mbili ni kama harufu flani ya utomvu wa papai, ila muda si mrefu nimempigia simu mama yake na kumuulizia kuhusu hiyo harufu ameniambia imekata....msaada tafadhali..


natanguliza shukrani
 
Mlikwenda kwa dak wa watoto na kufanya wa developmental check ups. Kunakuwa na six weeks from birth, 18 weeks, 24 weeks, one year two years na 3.5 years ..kama hajakwenda tafadhali fanya hima muone wataalamu kuna tatizo hapo
 
Ndugu yangu alipoteza mtoto mchanga kutokana naa kupuuzia dalili ndogo ndogo kama hzo.. Nakushauri nenda kwa specialist.
 
kuna wakati niliwahi kuja hapa kuomba ushauri, kuhusu mtoto huyu huyu kulia sana usiku na kukohoa, nilipata ushauri wa kila aina lakini nashukuru mwisho nilifanikikiwa, nilienda hospital nyingi tu na nakumbuka nilitumia gharama karibia 600000 katika kuhangaika na tatizo hilo mtoto akajaribiwa kila dawa niliumia sana, lakini nilipata bahati nikaelekezwa kwa mama mmoja wanamwita mama ima, ni daktar wa watoto alinipatia dawa na sindano na aligundua mtoto alikuwa na fangas ktk koo, na gharam ilikuwa ni 6000 tu mtoto akapona....sasa katika hili nimempeleka tena kwake akanipa vidonge flani vilisaidia mwanzo lakini sasa hamna kitu, na hata nyumbani amani imepungua maana hakuna anayelala usiku nikitoka kazini nimechoka naingia katika kazi hii mpya ya kuimba na kubeba mtoto mama nae ananyonyesha hadi maziwa yanaisha,, chakula anakula vizuri ila akimaliza kunyonya na usingizi hakuna ukimuwrka tu kitandani kaamka na hapo hesabu kusinzia tena hadi yapite masaa hata manne na hatolala
 
madaktari wa watoto awali alikuwa na tatizo hilo la fangas kama dokta wa mwisho alivyonambia, nilishaenda kwa madaktar wanoitwa bingwa huku nilipo...moro...kila daktar ananipa dawa zake mwisho nikawa nabeba madawa naenda nayo lakini wanakwambia hizo hazifai chukua hizi...sasa huyu mtoto kila siku ni madawa tu jaman? inaniumiza sana hii hali
 
Mkuu usijali gharama ikiwezekana tinga Muhimbili onana na daktari wa watoto fanya vipimo vyote umalize kazi
 
nashukuru kwa ushauri huu naona hicho ndicho nilichobakiza, ahsante sana
 
na ndio sababu nimekuja huku maana kuna wakati unafikiria hadi uwezo unafika mwisho ila ukiwa muwazi ni rahisi kupata mawazo mapya na ufambuzi kipi uache kipi kifanyike, hapa nipo job, macho yamevimba kwa usingiz na nikiulizia huko home naambia afadhali ya jana...ila lipo jambo hapa tayar naanza nalo, ntaleta mrejesho InshaAllah
 
anakula, ndizi laini, supu zote kuku na samaki kila siku, anapenda machungwa sana tena akaliminya lile hadi halitoi hata tone, pia ugali mwepesi na mrenda ama maharage anakula, tikiti anakula...yaani kuhusu kula hasumbui na hapo asipolala nakwambia ndani ya usiku mmoja huwa nafanya shughuli za numbani zaidi ya beki tatu maana akilia utahisi ana njaa labda utamsagia ndiz na uchemshe supu, au upike uji hapo labda ni saa nane usiku na wakati huo saa nne alishatoka kula na akaonesha dalili zote za kushiba....dogo ananinema mno
 

Attachments

  • IMG-20170815-WA004_edit_edit1.jpg
    41 KB · Views: 34
Alishapimwa vipimo vyote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…