Maadhimisho ya kuundwa kwa taifa la Israel

Maadhimisho ya kuundwa kwa taifa la Israel

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Madai ya Waisraeli yanaanzia katika misingi ya kidini ambapo katika Biblia (kitabu kitakatifu wa Wakristu na Wayahudi), Kitabu cha Kwanza cha Nabii Musa kiitwacho Mwanzo (sura ya 12), kinaonesha jinsi Ibrahim alivyoitwa na Mwenyezi Mungu ili kumtumikia. Eneo hilo la Palestina ambalo zamani lilijulikana kama Kaanani, ndipo chimbuko la dini tatu kuu zenye msingi wa Ibrahim zilibuka. Dini hizo ni Uyahudi, Ukristu na baadaye Uislamu. Dini ya Wayahudi yenye misingi ya Biblia ya Agano la Kale, likianza na vitabu vitano vya Musa: Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la Torati. Ukristu ukianzia misingi kwenye Agano la Kale hadi Agano Jipya na Uislamu ukishika vitabu vinne vya Tourat ya Nabii Musa (a.s), Zabur ya Nabii Dawood (a.s), Injili ya Issa bin Mariam (a.s.) au Yesu na Kurani ya Muhamad (s.a.w).

Ibrahim, mwenyeji wa Uru wa Ulkadayo (Mesopotamia), leo Iraq, wa kabila la Waebrania anahama kutoka Iraq na kwenda Haran, Syria, na baadaye kuingia Kaanani (Uyahudi), ambapo Mwenyezi Mungu anamtokea katika njozi na kumwapia Ibrahimu kuwa, ardhi yote hiyo amepewa yeye na uzao wake na kuahidiwa Baraka. Yaani, kubarikiwa kwa kila atakaye mbariki na kwamba jamaa zote za dunia zitajibarikia. Pamoja na ahadi hiyo, Mungu anamwambia nabii Ibrahimu kuwa uzao wake utakwenda utumwani, Misri, kwa miaka mia nne (400) hadi kizazi cha nne, ndipo watakapookolewa na kupandishwa Kaanani.

Mizizi ya ugomvi huo inaanzia mnamo Karne ya Kumi na Tisa (19), wakati wa vuguvugu la utaifa la Uzayuni na Uarabu. Vuguvugu la Wayahudi lilianzishwa kuwa la kisiasa, mwaka 1892, dhidi ya Urusi na Ulaya. Mkakati ulianza kwa Wayahudi wote, popote walipo, kurejea katika nchi ya Palestina ambapo walipachukulia kuwa ndipo nchi yao ya asili. Katika kutimiza azma yao, Muungano wa Kizayuni na Taasisi za Fedha za Kiyahudi walihimiza uhamiaji na kufadhili ununuzi wa ardhi Palestina, chini ya utawala wa Ottoman na Uingereza. Mgongano huo ukianzishwa na Uingereza, kupitia Mikataba mitatu: Mkataba wa McMahon (chini ya Sir Henry McMhaon-Hussein); Azimio la Balfour la Novemba 2, mwaka 1917; na Mkataba wa Sykes-Picot, chini ya mwanadiplomasia wa Uingereza, Mark Sykes na Mfaransa, Frncois George-Picot.

Aidha, tangu hapo kulifuatiwa na milipuko ya mapigano ya mara kwa mara, kati ya Wayahudi na Waarabu, katika eneo la Palestina. Hakuna asiyekumbuka jinsi kiongozi wa Chama cha Nazi, Adolf Hiltler alivyowafanyia Wayahudi maangamizi makuu ya kupitia angamizo la Holocaust, ikiwa ni jitihada ya kulifuta taifa hilo. Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1947, liliridhia kugawanywa kwa nchi ya Palestina kwa Wayahudi na Wapalestina, ambapo Wayahudi walikubali na Wapalestina wakiungwa mkono na Umoja wa Nchi za Kiarabu, wakikataa na kusababisha kuzuka vita baina yao. Vita hivyo viliwafanya Wapalestina kuhama na kukimbilia nchi jirani za Kiarabu wakiwa wakimbizi yaani Al-Naqba. Makundi kwa makundi ya Wazayuni kutoka Ulaya Magharibi na Marekani walihamia Israeli. Zikabuniwa propaganda kuwa Wazayuni walikuwa katika mateso makali, chini ya utawala wa Adolf Hitler.

Miongoni mwa vitengo vilivyoundwa kuilinda Israeli, kilikuwa ni kikundi cha ulinzi na ujasusi, maarufu kikijulikana kama Shay ambacho wakati wa utawala wa Waingereza, wanachama wake walikuwa mkono muhimu wa harakati za chinichini za Mazayuni dhidi ya maeneo ya wenyeji wa asili ya Palestina. Wakazi asilia wa maeneo hayo ni Wafilisti na Wayahudi. Kitengo hiki kilipata msaada mkubwa, kutoka kwa wakala mkubwa wa Mazayuni, Zionist Congress, idara iliyoanzishwa mjini Zurich mwaka 1929.

Mara baada ya kuundwa taifa la Israeli, wahamiaji kutoka Ulaya na Marekani (Wazayuni) wakiongozwa na Shay walisuka mipango na kuendesha shughuli za kijasusi sehemu mbalimbali ulimwenguni. Kabla ya hapo, tokea mwaka 1923 hadi ilipofanikisha mpango wake, mwaka 1948, Shay ililenga kuanzisha taifa huru la Kizayuni katika maeneo ya Waarabu. Na, mbinu iliyotumika wakati ule, ilikuwa kupandikiza watawala wa Kizayuni kimya kimya, ambao kwa taswira ya nje walionekana kama watumishi wa utawala wa Kiingereza, ambapo, wakati huo huo, walitumia fursa ya utawala kuandaa programu na kupanga mikakati dhidi ya Waarabu hasa wakazi wa maeneo hayo. Kwa ajili hiyo, taarifu za kijasusi zilikusanywa ili kutumika katika udanganyifu au propaganda na mipango ya utekaji nyara maeneo hayo.

Idara ya Shay ilianza kupandikiza majasusi wake, katika makundi pinzani ya Waarabu dhidi ya harakati za Uzayuni, ndani na pembezoni mwa Palestina. Kazi kubwa ya majasusi hao ilikuwa kuchunguza na kuangalia mienendo ya wanaharakati walioonekana kuwa na misimamo mikali zaidi; hiyo ilikuwa sio tu katika makundi ya Kiarabu, bali pia, katika jumuiya za Wazayuni wapinga Uzayuni. Pamoja na kazi hiyo, Shay ilikita ujasusi wake katika kuangalia uuzwaji na uingizaji wa silaha kwa njia za magendo na kuangalia siasa za kinazi ili kuwahakikishia usalama wahamiaji wa Kiyahudi, waliokuwa wakitoroka kutoka Ulaya kabla na wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Shay iliundwa ikiwa na vitengo vitano, vilivyojihusisha pamoja na mambo mengine. Vitengo hivyo ni Ujasusi wa Kisiasa (Machlakit Medinit); Udhibiti wa Mashirika Mengine ya Kijasusi na Usalama wa Ndani (Sherut Bitachon Klalt); Ujasusi Ndani ya Jeshi (Sherut Modiin); na Polisi Maalumu Ndani ya Kitengo cha Ujasusi Jeshini (Sherut Modiin Shel Mate Arizi). Ujasusi ndiyo siri pekee na ya muhimu na ya mafanikio ya Israeli katika vita vyake dhidi ya Waarabu. Kwa kushirikiana na CIA, mashirika ya ujasusi ya Israeli yameweza kupanga na kufanikisha mazoezi yote, dhidi ya nchi za Kiarabu na zile zilizofikiriwa ni za Kiislamu.

Kamandi kuu ya ujasusi miaka ya mwaka 1950, iliitwa Vaadat, ambayo shughuli zake za msingi zilikuwa ni pamoja na kuunganisha shughuli zote za kijasusi na uangalizi wa usalama, ndani na nje ya Israeli. Vaadat inawajumuisha Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi wa Nje, Mossad; Mkurugenzi wa Idara ya Ujasusi Jeshini; Mkurugenzi wa Idara ya Ndani ya Usalama, ShinBeth; IGP na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti na Mipango, kilicho chini ya Wizara ya Mambo ya nje. Aidha, Mkuu wa Divisheni Maalumu katika Idara ya Upelelezi ya Polisi hujumuishwa katika kamati hii ya usalama, ambayo Mwenyekiti wake ni Mkurugenzi wa Mossad, anayewajibika moja kwa moja kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo. Huo ndio mfumo wa juu wa ujasusi ulioijenga Israeli, mara tu baada ya kuundwa taifa lao, baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Vaadat iliugawanya ujasusi wa Israeli katika mashirika makuu mawili, shirika la nje, lililojulikana kama Mossad na la ndani linalojulikana kama, ShinBeth, yote yakilenga mambo matatu makuu: kulinda maslahi ya Israeli; kuwaandama Waarabu na Wapalestina; na kuudhibiti ulimwengu kwa ujumla.

Kwa mujibu wa kitabu cha Israel Foreing Intelligence and Security Service kinaainisha kazi za Mossad, kwa kuandika yafuatato: “Pamoja na shughuli nyingine, Mossad ilihusika zaidi na ukusanyaji wa taarifu za kijasusi kutoka nje pamoja na kuandaa programu za kijasusi nje ya Israeli, hususan, katika nchi zenye Waislamu na hasa wale wa makundi yanayoonekana kuhatarisha usalama wa Israel. Kwa upande mwingine, ShinBeth ilihusika na usalama wa Waziri Mkuu na maafisa wa juu wa serikali ya Israel.”

Wakufunzi wa mafundisho ya Menejimenti ya Kiusalama, wanaeleza kuwa, ili kuweza kutatua tatizo lazima kuendane na upataji wa habari muhimu na za hakika, kupitia mbinu mbalimbali, ikiwemo ya taswira zaidi ya moja ambayo husaidia kuwakinga maafisa au mawakala, kuwa na utambulisho rasmi kimavazi, jina, kabila, utaifa, kazi, taaluma, au mahali anapoishi. Afisa au wakala huyo huweza kujichomeka au kuwapo mahali akitumia utambulisho wa uongo ama wa kiitikadi, akiwa mweledi mzuri wa itikadi hiyo, mahiri wa lugha ya mahali fulani, mila na tamaduni za watu wa sehemu anayoifanyia ujasusi, akiwa jasusi mshiriki kama walivyofanya majasusi maarufu wa Kiingereza, Bw. Humphrey Key Aitrafat na jasusi mwangalizi Bw. Lawrence of Arabia, huko Hijaz-Saud Arabia, ili kupata taarifu muhimu kwa muda mrefu. Wakati kwa KGB, ujasusi wa kada hii ulikuwepo chini ya kurugenzi isiyo rasmi, ambayo ni kurugenzi maalumu ndogo kuu ya kurugenzi kuu ya kwanza. Pamoja na kurugenzi hiyo, pia zilikuwapo idara maalumu, zilizohusika na ujasusi wa habari na uzuiaji wa mitandao mingine ya kijasusi, chini ya vitengo vya upotoshaji na hatua za kiutendaji.

Katika andiko la kijasusi, liitwalo, Intelligence Gathering Devices (Mbinu za Kijasusi za Ukusanyaji wa Taarifu), imeandikwa ya kwamba, mashirika ya kijasusi ya Israeli yamekuwa na mbinu za hali ya juu za kupata taarifu muhimu, mipango na mikakati, ikitumia zana bora zaidi. Kwa mujibu wa andiko hilo, hivi leo, Israeli inaongoza kwa utumiajii wa kamera ndogo sana, katika uchukuaji wa picha za matukio, taswira za watu na maeneo yanayolengwa bila ya wahusika kubaini.

Ama, kunako tar. 16 Aprili, mwaka 2005, Gazeti la Suday Nation lilichapisha matini moja ya matumizi ya vifaa vya ki-elektroniki, likielezea kupiga hatua kubwa kwa sanaa ya ujasusi, ikiongozwa na wataalamu wa Israeli ambako kumesababisha ulimwengu wa siri zaidi ya mtu mmoja, usiwepo hivi sasa. Katika mada iliyopewa kichwa, Uingiliaji wa Faragha za Watu ni Jambo la Lazima kwa Ajili ya Usalama wa Taifa, imeelezwa ya kwamba katika uwanda wa kidunia, Uingereza na Marekani na kwa hakika Wazayuni wakiwa nyuma yao, wamekuwa na ushirika wa ki-elektroniki katika kufuatilia kwa karibu zaidi mambo mbalimbali. Ushirika huo wa usakaji habari, unaojitambulisha kwa alama au jina la kijasusi, Echelon, ambao ni mtandao wa mawasiliano ya satelaiti na ngamizi unaonasa taarifu, ujumbe, mazungumzo na habari za ulimwengu mzima, zinazopita kwenye vifaa vya ki-elektroniki.

Katika kitabu chake, The Way of the General Zhuge Liang ameandika kuwa, kimaumbile, si kawaida kwa juha kuweza kumpiku mwerevu, bali ni mwerevu mwenye fursa ya kumzidi juha kwa uwerevu wake. Bali, ili mwerevu aweze kumshinda mwerevu mwenziwe, hana budi kutumia vizuri, mianya na fursa muhimu. Walioitazama taaluma hiyo, kwa kuihusisha na historia ya mwanaadamu, wamejaribu kuonesha jinsi ilivyo kongwe, ingawa wanakiri kuwa awali haikuwa rasmi kama ilivyo sasa. Kwa mujibu wa vitabu vitakatifu, mmoja wa manabii, Suleiman, Mwana wa Daudi, ametajwa kutumia ujasusi kupata taarifa juu ya nchi jirani, kwa kumtumia ndege, maarufu kwa jina la Hudi Hudi.

Nabii huyo anayesekana kuwa ana uwezo wa kufahamu lugha mbali mbali za wanadamu, majini, wadudu na wanyama, alipewa taarifu na ndege Hudi Hudi, kutoka nchi ya Sabaa ambayo sasa inajulikana kama Yemen. Katika Sura ya 27, aya ya 20 mpaka 22, Mwenyezi Mungu anaufahamisha ulimwengu juu ya habari hiyo ya kijasusi kama ifuatavyo: “(…) imekuwaje mbona simuoni Hudi Hudi au amekuwa miongoni mwa wasiokuwa hapa (...). Kwa yakini, nitamuadhibu adhabu kali au nitamchinja au aje na habari muhimu. ‘Basi hakukaa sana (Sulaymaan) mara Hudi Hudi akafika akasema nimegundua usilogundua, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabaa na habari yenye yakini (…).” .........inaendelea......

Kutoka katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, Bei ni 80,000/=

+255715865544
+255755865544

IMG_20180514_210222_486.jpg
FB_IMG_1526321554919.jpg
 

Attachments

  • IMG_20180514_210042_414.jpg
    IMG_20180514_210042_414.jpg
    8.7 KB · Views: 74
Kitabu cha thamani ya 8000 unauza 80000
 
Wapalestina ni waarabu,uzao wa ibrahim pia,kwa nini wanang'ang'ana kuwafukuza wenzao,lakini pia tuna uhakika gani kuwa kweli netanyahu ni uzao wa ibrahim na sio mzungu wa ulaya mashariki!?
 
Huu mziki tuwashauri ndugu zetu Palestine wawe na subira.Hakuna namna kugawana mji wa Jerusalem.
 
Yericko you have lost touch now days bro. find something else to do
Zamani ulikuwa ukiandika thread ilikuwa hatari. sasa umechuja kwanini?
 
Punguza bei chif tumwagike manake usawa huu wa mzee wa chato themanini sio mchezo
 
Unapotaka kuilezea israel msichanganye .mtambue israel inamaelezo ya mtazamo mitatu.
1:israel kwa mtazamo wa ukristo
2:israel kwa mtazamo wa uislamu
3:israel kwa mtazamo wa kimataifa.
Wengi mnatuchanganyia mtazamo wa dini na mataifa na chaajabu ya dini hamyaelewi.Yeriko mwenyewe haamini dini alafu anakuchambulia israel kwa mtazamo wa dini ya kikristo
 
Kuwa muwazi unataka kutuuzia vitabu, hao wahuni walivamia ardhi ya watu kwa habari za kufikirika. Watu wako kimya na dunia kwa ujumla watu wakifanyiwa uhuni kwa kigezo cha historia yenye mashaka, Dini za mashariki ya kati zinaua watu wengi kuliko mabudha na sie mnao tuita wapagani
 
Kuwa muwazi unataka kutuuzia vitabu, hao wahuni walivamia ardhi ya watu kwa habari za kufikirika. Watu wako kimya na dunia kwa ujumla watu wakifanyiwa uhuni kwa kigezo cha historia yenye mashaka, Dini za mashariki ya kati zinaua watu wengi kuliko mabudha na sie mnao tuita wapagani
Kule Myanmar mabudha wanaua sana na sri Lanka mabudha ni wauwaji wakubwa
 
Back
Top Bottom