Maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya Muungano, Dkt. Philip Mpango aziongoza Dodoma

Maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya Muungano, Dkt. Philip Mpango aziongoza Dodoma

Mama kaenda USA kutalii bongo hakuna nanayepapenda basi tu wapo kutunyonya..only JPM aliipenda Tanganyika.

Halafu huu utaratibu wa kuleta viongozi wa dini kila kwenye tukio la kiserikali ni utaratibu wa hovyo sana na ni wakibaguzi.

Muungano umebaki kwa ccm tu ndio wanaonufaika nao mana ni muungano wa hovyo kuwahi kutokea duniani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mtu mwoga atakuwa hajalala usingizi leo
 
Leo ni maadhimisho ya miaka 58 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na sherehe zimeshaanza kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma na anaeongoza ni makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango

Kuwa nami kwa yatakayojiri
=========

=> Viongozi wa dini zote wameshatoa sala na dua kwa ajili ya mjumuiko huu

=> Anayeongea sasa ni waziri Simbachawene na anatambulisha viongozi waliohudhuria, pia amesema sherehe zimefana.

=> Sasa ni salamu kutoka kwa waziri Suleiman Jaffo ambae anahusika na Muungano na anaaza kwa kumshukuru makamu wa Rais anaemuwakilisha Rais wa Jamhuri. Anawashukuru wote kwa kazi wakiadhimisha miaka 58 watanzania wakiwa na amani na furaha.

=> Sasa ni burudani kuhusu muungano

sherehe za miaka 58 ya Muungano Rais yuko Marekani.?​

Mwigulu itabidi apelekewe tai nyingine zenye bendera maana kabrasha aliloenda nalo keshamaliza na hakuna mfuaji
 
Mama muda huu yupo kwenye kumbato zito na mzee wa smile, chezea USA wewe
 
Hivi kweli watu wamepanga ratiba ya Rais bila kujali tuna Sherehe za Muungano ambazo Amiri Jeshi Mkuu anapaswa kuwepo?
Sherehe za kitaifa kama hizi ni za CiC na vyombo vyake. Ndio maana gwaride huwa inakuwepo na kukaguliwa na Amiri Jeshi Mkuu.

Hivi pale ukumbini kutakuwepo na gwaride mbele ya Makamu wa Rais?
 
Leo ni maadhimisho ya miaka 58 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na sherehe zimeshaanza kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma na anaeongoza ni makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango

Kuwa nami kwa yatakayojiri
=========

=> Viongozi wa dini zote wameshatoa sala na dua kwa ajili ya mjumuiko huu

=> Anayeongea sasa ni waziri Simbachawene na anatambulisha viongozi waliohudhuria, pia amesema sherehe zimefana.

=> Sasa ni salamu kutoka kwa waziri Suleiman Jaffo ambae anahusika na Muungano na anaaza kwa kumshukuru makamu wa Rais anaemuwakilisha Rais wa Jamhuri. Anawashukuru wote kwa kazi wakiadhimisha miaka 58 watanzania wakiwa na amani na furaha.

=> Sasa ni burudani kuhusu muungano
Tudumishe muungano
 
Back
Top Bottom