Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani

Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Februari 4 ya kila mwaka huwa ni maadhimisho ya siku ya Saratani duniani.

Takwimu za Afrika
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), bara la Afrika hupatwa na visa vipya vinavyokadiriwa kufikia milioni 1.1 kila mwaka na idadi ya vifo ikiwa ni 700,000. Takwimu hizi zinatoa makadirio ya vifo kufikia hadi milioni 1 ifikapo mwaka 2030 ikiwa jitihada za haraka hazitafanyika kwenye kupambana na ugonjwa huu.

Mgawanyiko wa saratani hizo upo kama ifuatavyo-
  • Saratani ya matiti 186,598
  • Saratani ya Mlango wa kizazi 117,316
  • Saratani ya tezi dume 93,173

Takwimu za kidunia
Saratani ya matiti ndiyo huongoza kwa kuathiri watu wengi zaidi ikifuatiwa na saratani za mapafu, utumbo mkubwa/mpana, tezi dume na tumbo. Orodha ya makadirio ya visa vipya vinavyotokea duniani kila mwaka-
  • Saratani ya matiti (2.26 Milioni)
  • Saratani ya mapafu (2.21 Milioni)
  • Saratani ya utumbo mpana/mkubwa (1.93 Milioni)
  • Saratani ya tezi dume (1.41 Milioni)
  • Saratani ya tumbo (1.09 Milioni)

Siku hii inalenga kuongeza ufahamu na jitihada za kupambana na ugonjwa huu unaoonekana kwenye mfumo wa aina nyingi pamoja na kutukumbusha mambo kadhaa tunayoweza kufanya kama sehemu ya kujilinda.

Ili kujikinga na saratani, unashauriwa kufanya mambo yafuatayo-
  • Kuacha uvutaji wa sigara pamoja na bidhaa zote za tumbaku
  • Fanya mazoezi kuongeza utimamu wa mwili
  • Kula mlo bora
  • Kunywa pombe kwa kiasi
  • Kwa wanawake waliojifungua, nyonyesha mtoto kwa walau miaka 2 ili kujikinga dhidi ya saratani ya matiti
  • Kupata chanjo ya HPV na homa ya Ini
Pia, ni muhimu kufanya uchunguzi mara kwa mara wa afya ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa ikiwa utaonesha viashiria vya uwepo wa ugonjwa huu.

Chanzo: WHO
 
Mbona hakuna Takwimu za Tanzania za saratani
 
Back
Top Bottom