Roulette
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 5,568
- 5,386
wazazi wa siku hizi tuna mtihani mkubwa sana wa fuwafunza watoto wetu maadili (nimetafsiri maadili kama values).
Zamani ilikua rahisi sababu jamii nzima ilikua na maadili sawa na mzazi anampa mtoto yale yale maadili alipokea kutoka kwa zazazi wake mwenyewe, na mtoto akileta ubishi anarudishwa nafasi yake kwa adhabu kali sana. Ila leo tunaishi katika tamaduni nyingi sana ambapo unashindwa kumbana mtoto kama tulivyo banwa sisi. Upande mngine pia bila kumuandaa mtoto atashindwa kushirikiana na wenzie, na waalimu au na watu wasio wa familia yake.
Dunia ya leo ina mambo mengi sana na saa zingine hatujui tuchukue nini tuache nini. Mwalim akimchapa mtoto fimbo anashtakiwa polisi. Ukishangaa mtoto wa jirani anamvalia baba yake bikini waende swiming pool unaonekana mshamba etc. Nini sahihi na ni kipi cha kufanya?
Nimegawa maadili katika kundi nne na nimejaribu kuonesha ni kundi zipi zinaruhusiwa kubadilika, kwa kiwango gani, na nani anaruhusa ya kubadilisha.
Kwa wale wenye mifano ya maadili haya, au wenye aina zingine nawakaribisheni kunichangia au kunikosoa. Asanteni.

- Kwanza kuna maadili yanao kubalika na walimwengu wote, kama uaminifu, umoja, upendo, imani nakadhalika. Mwambie mtoto kua anatakiwa kutumia maadili haya kama nguzo ya maisha na kila atakapo kua katika changamoto atafute jibu litakalo husisha maadili haya.
- Pili kuna maadili ya Dini na imani zetu. Hizi zinaweza kua tofauti na maadili ya dini zingine. Mwambie mtoto aheshimu sana maadili ya dini yake ila aheshimu pia dini za wengine sababu ndio njia pekee ya watu wa dini zingine kuheshimu dini yake. Hapa sitaki kuweka mfano kama mnao naomba mnichangie. Maadili haya kwa kawaida hayabadiliki ila yanaweza kutafsiriwa na wachungaji (sheikh, paster au father)
- Tatu Kuna maadili ya nchi zetu. Mwambie mtoto kuhusu historia ya nchi yake na msaidie kuipenda nchi yake na maadili ya raia mzuri. Tofautisha propaganda za siasa au za serikali na maadili ya nchi. Maadili haya ni yale yale kwa raia wote, wanawake kama wanaume, wazee kama vijana, magamba kama manyoa... Mfano: Sisi kama raia hatutakiwi kuchoma bendera. Bendera letu ni mali na lina thamani kubwa sababu kuna mashujaa wengi walimwaga damu kwa kulilinda. Pia kama raia tunatakiwa kulipenda taifa letu na kulitetea kila tuendapo etc.
- Nne, kuna maadili ya mila, kabila na familia zetu. Haya ni maadili tuliorithi toka kwa wazee. Mwambie mtoto kua maadili haya yalisaidia ukoo kufika hapa tulipo na yalizaliwa kutokana na mazingira mbali mbali. Hivo, ikiwa atataka kujua matumizi ya maadili hayo katika mazingira fulani, asome kwanza mazingira na afanye mwenyewe tafsiri ya maadili kutokana na mazingira. Anaweza pia kuongea na wazee wa familia kwa kupata mwanga zaidi. Mfano: Babu yake alikua na wake 5, baba yake akawa na wake 2, je yeye anaweza pia kuoa mke zaidi ya mmoja? Au Mama yake alikeketwa, na dada zake pia. Je akiacha kukeketwa ni makosa?
- Alafu kuna mchanganyiko wa maadili ya nyumbani (hapo kwenu). Mzazi lazima umwambie mtoto wewe mwenyewe unatumia nguzo gani, kanuni gani, desturi gani na maadili gani kuiongoza familia yako? Katika viwango vyote hivyo chukua 2 au 3 kwenye kila daraja zinazo kuongoza zaidi kuliko zingine na zifanyie kazi. Ni muhimu sana mtoto aone kua mzazi unachukulia maadili ya familia kwa kiwango cha juu sana. Na ikiwa kwa sababu moja au nyingine unahitajika kumkaripia au kumuadhibu mwanao, kumbuka kumwambia ni adili gani la familia amevunja. Na mwambie kua akiwa mkubwa, atajenga zakwake mwenyewe (mfano wazazi wanapo mwambia mtoto kua hapo nyumbani hakuna kurudi baada ya saa 2 usiku, na kama hutaki tafuta nyumba yako. adili linalo husika hapa ni heshima na limeunda kanuni la saa ya kurudi nyumbani)
Kwa wale wenye mifano ya maadili haya, au wenye aina zingine nawakaribisheni kunichangia au kunikosoa. Asanteni.